NHIF kuzindua vifurushi vipya vya bima ya afya, sasa kila Mtanzania kuzingatiwa

Mbwembwe mingi huduma hovyo kabisa, watumishi hawajapata huduma za viwango madawa na huduma wanazopewa zina limitations kibao!

Ningewaona mna akili kama mngepunguza matumizi mabaya ya fedha za wachangiaji mkaboresha huduma kwa raia badala ya kununua mashangingi kwa ajili ya matanuzi
 
Yeah je ni kwa vifurushi vyote hawatibu wala hata baada ya kuwa mwanachama?
Wamesema hawashughuliki nayo kabisa, ila baada ya mwaka utapata huduma za uzazi,huduma za vifaa tiba saidizi na vipimo kama MRI na CT Scan navyo utavipata baada ya mwaka
 
Nyie NHIF mnazungumzia masikini yupi wa Tanzania anayeweza kutoa laki 5 kwa ajili ya bima kwa mwaka?
54,000 tu ya toto afya kadi ni Kimbembe sembuse hizo pesa hasa hiyo sehemu ya familia mbaya zaidi ni mwaka mmoja
Bora hizo bei zingekuwa kama leseni unatoa pesa kubwa ila unapata guarantee ya miaka angalau 2 afu unavyozidi kuchangia bei iwe inashuka kwa kiasi fulani ila unapojiunga ndio inakuwa kubwa
Afu serikali ingekusanya maoni ya wananchi willingness and ability to pay ndo itumie kupanga vifurushi sio kukurupuka tuu bila kujua hali halisi ya uwezo wa watu kiuchumi
 
Bado hizi ni mbwembwe tu kwa watanzania kiasi kilichowekwa bado si rafika kwa Watanzania wengi, Wengi bado watazidi kuangaika juu ya swala zima la matibabu na kupelekea kushindwa kabisa kumudu gharama husika
 
Hayo magonjwa yanatibiwa baada ya mwaka mmoja wa kuwa mwanachama. Huwezi pata kadi leo afu ukaanza tibiwa saratani baada ya mwezi.

Figo pia utasubiria mwaka 1 ndo watakuruhusu utumie.

Babu yangu ana NHIF na anatumia kwenye Moyo
Kwa mujibu wa maelezo ya mdomo wa yule afisa niliyekuwa nikizungumza nae alisema kuna magonjwa ambayo hawashughuliki nayo hata ukikata kifurushi gani kati ya hivyo vitatu na akanitajia matatu Saratani, Figo na Moyo akasema labda presha sasa uenda pia kuna mengine sijui
 
Mkuu utaratibu huo bado upo kwa dar es salaam familia ya watu 6 inategemewa watalipa laki 1 na kwa mtu mmoja mmoja ni elfu 40 kwa mwaka kwa mikoani elfu 30 kwa mwaka mzima kwa huduma za kituo cha afya,hospitali za mikoa na wilaya
Wewe mtumishi ameondolewa tegemezi wake kuna unafuu gani hapo
 
Nilitegemea kuona kifurushi kitakacho tumika katika hospital za serikali tu ambacho ndio kingekuwa cha bei ya chini kuliko vyote lakini wabunifu hawakulifikilia hilo
 
Kiukweli huduma zao ni mitihani mkubwa kwa wanachama!

Watu wengi wamekuwa wakijilipia wenyewe kwa akiba ya pesa zao kimatibabu wakati wanakatwa pesa chungu nzima na hio bima!

Ukifika mtu wa bima hospitali unaambiwa kasubiri pale, kwenye vipimo unaambiwa vipimo hivi bima hawalipii inabidi ulipie mwenyewe,

Dawa hizi bima hawalipi inabidi ulipe pesa zako,

Yani ilimradi ni shida !

Hapana hawa jamaa ni mtihani hasa!
 
Halafu wengine ni mke na mume lakini wote wanakatwa,

Kwa nini?

Ukiwaambia wanakubabaisha!

Kwanini umkate mke na mume kwa wakati mmoja?
 
Back
Top Bottom