Mbowe anadaiwa au lah?Hii ni siasa 100% kataa kubali lkn ndiyo hivyo.
Taratibu tutaelewana TU.
Akili yako ndio hapo ilipogota huwezi kuelewa ,Kwani ulitaka adaiwe lini? Umesoma habari vyema? Alipewa notisi ..
Kwa sababu Mbowe ni mdaiwa Sugu...Nonsense Mwasenga, anadhani wote ni wapumbavu/ majuha kama yeye! Why start with Mbowe?
Je Mbowe anadaiwa kodi au hadaiwi??Duh! Kumbe ni kwa sababu ya kupambana na Magufuli!? ina maana asingepambana naye basi NHC wasingetumika kisiasa!!! Kweli nduli wa visasi katinga nchini!
We hushangai kuwa Mbowe kakaa kimya sana??Ukiishia kuandika hivyo huwezi kueleweka, hebu tuwekee in details ni namna gani hakufuata masharti-utuwekee mkataba baina ya hizo pande mbili na namna ulivyokuwa ukitekelezwa hadi kutokea yaliyotokea!
soma andiko vizuri, wanadaiwa wengi ila wameanza na MBOWE.Iloo shirika mbowe tuu ndo anadaiwa. Kama sio swala la kisiasa na wengine ambao hawalipi wawe ndani ya ccm au nje ya ccm wafungiwe pia.
Hakuna siasa hapo NHC wanafanya kazi Yao afu magu ajatajwa hata kidgo hapo
Kwanini iwe sept mosi?View attachment 391870
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Mbowe Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.
Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.
Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.
Ndani ya kampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.
Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.
Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.
“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.
Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.
Source: Mwanahalisi Online
Hakuna cha majungu Mimi sio chadema lakini huyu jamaa ni jipuMmeanza majungu badala ya kumchangia Mwenyekiti alipe kodi.
Mkizubaa hatua inayofuata ni kupiga mnada mali zake.