NHC: Hatujamuonea Mbowe

NHC: Hatujamuonea Mbowe

Duh! Kumbe ni kwa sababu ya kupambana na Magufuli!? ina maana asingepambana naye basi NHC wasingetumika kisiasa!!! Kweli nduli wa visasi katinga nchini!

Hakuna siasa hapo NHC wanafanya kazi Yao afu magu ajatajwa hata kidgo hapo
 
Wadeni wengi tumeamua tuanze na mbowe je hamuwezi kuishia na mbowe pia
 
September 1 ina mengi ukuta kupatwa kwa jua maazimisho ya jeshi kukusanya madeni nhc
 
Hivi tutaendelea kweli kwa style hii, shirika la umma linaacha deni kwa mtu mpaka linafikia bilioni! Shirika lina bodi, mkurugenzi na maofisa wanaoliendesha. Deni linakuwa NHC wanaliangalia tu, Magu angeanza kuwatumbua hao kwanza km anataka Tz ya wananchi wa maisha ya kati.
 
Mpaka inafika B mlikua wapi?NHC ni jipu

Hili ndilo swali. Zikimwagwa data zote za mashirika ya umma kama NHC jinsi yanavyosimamia malipo na madeni ya wateja, tunaweza kushangazwa jinsi mabilioni ya pesa ya umma yanavyohujumiwa kwa kutozingatia kikamilifu taratibu na kanuni zilizowekwa - au hata kwa kuwa na taratibu na kanuni legelege ambazo wahusika hawana utashi wa kuziimarisha kwa faida yao.

Halafu NHC wasimdanganye mtu. Hatua wanazochukua dhidi ya biashara za Mbowe zina kila dalili ya kutumiwa kisiasa. Yaani katika wadaiwa lukuki zikiwemo taasisi za serikali wanaona kusema "... pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe" ni kauli ya kawaida tu! Leo hii? That's too much of a coincidence with current events. Sisi SI wahamiaji au wageni; tunaifahamu nchi yetu vizuri sana. Na hatuwashangai kwa hilo. Ndio michezo ya nchi zetu za dunia ya tatu.
 
Tunaishi katika jamii ambayo bado ni duni kivitendo na kifikra. Kwa vitendo kama hivi ni vigumu sana nchi hii kupata maendeleo. Tunaongelea nchi ya viwanda, hivyo viwanda vitajengwa na wanachama wa CCM pekee yao? Maana siamini kwa mtu ambaye siyo mfuasi wa CCM kama anaweza kufanya uwekezaji mkubwa usiohamishika kwa kipindi hiki kutokana na hofu inayojengwa.

Ni mjinga pekee yake atakayeamini kuwa limefanyika hili bila ya sababu za kisiasa maana hata maelezo yenyewe yapo wazi kuwa, 'tumeanzia na Mbowe ....', sababu za kuanzia na Mbowe hazikuelezwa.
Kwani ulitaka waenze na nani?
 
Si kuna kesi mahakamani kuusu mmiliki halali wa hili jengo?
 
View attachment 391870
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Mbowe Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya kampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.

Source:
Mwanahalisi Online

NAONA NGOMA WANAPIGA WAO WANACHEZA WAO. MWENYE MALI HAJALALAMIKA WALA KUSEMA LOLOTE MPAKA SASA, WASIWASI WA NINI, HII TAMTHILIA SERIES ZAKE NI NZURI SANA 😀😀😀😀😀😀😀
 
Duh! Kumbe ni kwa sababu ya kupambana na Magufuli!? ina maana asingepambana naye basi NHC wasingetumika kisiasa!!! Kweli nduli wa visasi katinga nchini!
Alipe deni la pango na sio kutetea upuuzi kwa mgongo wa siasa...kama alipewa notisi kwa nini hakulipa...hii tabia yake ya udeni sugu hata NSSF anawasumbua...ngoja kesi ziishe mahakamani.
 
Mpaka inafika B mlikua wapi?NHC ni jipu
Nashikwa kichefu chefu ufanisi wa watedaji wetu wansfanya kazi kwa mazoea kweli hadi inafikia B,halafu nakumbuka kaka yangu Mbowe maneno yake katika Vilili

Tarehe 16/4/2015 mbowe alisema nanukuu "Rais JK amekaa kimya kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiolipa kodi na wengi wao ni wale wanachama wa CCM"

Tarehe 1/8/2016 NHC wanasema nanukuu"Tumempa Mbowe Notes ya kuhama kwenye jengo letu baada ya kulimbikiza deni la zaidi ya 1.5 Bil mpaka sasa hajalipa"

Ni kweli hii ni Siasa?ama anaonewa? ni viongozi wangapi wanatabia kama ya Mh Mbowe?Bg Up JPM rudi sasa ndani ya Mapapa wa CCM hapo ndio utagundua mtu amelimbikiza T sio B tena
 
mie nadhani swala hili ni la kibiashara baina ya Mbowe Hotels LTD na NHC. mbowe hotels ltd ni kampuni inayojitegemea kisheria " there are bearers of assets and liabilities" wala si CHADEMA. CHADEMA nichama cha sasa chenye usajili na malengo tofauti..you should demarcate between Mbowe a CHADEMA chairperson and Mbowe the owner of mbowe hotels ltd. vilevile, NHC ni shirika la umma wrote wa Tanzania wala so CCM peke yao. hiyo mteja yeyote bila kujali ranging, itikadi, n.k lazima alipe..kama kuna tatizo la kimkataba kwenye biashara hiyo au uonevu mahakam zipo....
 
Mbona mnajitetea sana ? Si kodi hajalipa na mnaweza pia kuthibitisha hilo ,Kelele za nini ? Mara hatujamuonea ,oh sio swala la kisiasa ,hata kama sio la kisiasa ,mmekosea timing huwezi kuniaminisha shinikizo la kisiasa halijatumika wakati ambao nchi ilikuwa kwenye homa ya Ukuta Mbowe akiwa ndio Captain
Kwani ulitaka adaiwe lini? Umesoma habari vyema? Alipewa notisi ..
 
Back
Top Bottom