NHC: Hatujamuonea Mbowe

NHC: Hatujamuonea Mbowe

Labda humu JF ili swala linaonekana la uonevu lakini kwa wapangaji wa NHC wanaweza ona huyu bwana kapendelewa sana inawezekanaje deni lifike mpaka zaidi ya billioni na kwa miaka kadhaa asilipe. Ebu waulizeni majirani walio karibu na nyumba za NHC wapangaji wakawaida deni la miezi mitatu tu alizidi ata millioni tatu utapewa notisi kila kukicha na siku wakija huo utemi wa NHC anajua mungu tu. Huyu mwenzetu deni limefika mpaka billioni kweli life is not fair na bado anawatu wa kumtetea.
 
msitake kuniaminisha kuwa hili suala halina visasi vya kisiasa even though ni kisheria/kibiashara/kimkataba..

Hapa lazima kuna kitu
Na kitu chenywet ni kupambana na mafisadi na wakwepa kodi wote
 
Mbona mnajitetea sana ? Si kodi hajalipa na mnaweza pia kuthibitisha hilo ,Kelele za nini ? Mara hatujamuonea ,oh sio swala la kisiasa ,hata kama sio la kisiasa ,mmekosea timing huwezi kuniaminisha shinikizo la kisiasa halijatumika wakati ambao nchi ilikuwa kwenye homa ya Ukuta Mbowe akiwa ndio Captain

Kamlipie basi Jemedari wenu
 
Kodi anapokea kila siku kutoka wapi kama akina Mbowe wapangaji hawalipi kodi. Mlipeni hizo bilion then mtoe malalamiko kua hajengi nyumba
Mkuu ulikuwa wapi siku zote kutujuza hayo mpaka usubiri Mbowe atolewe nje ya nyumba ?
Mmeanza majungu badala ya kumchangia Mwenyekiti alipe deni.

Mkizubaa hatua inayofuata ni kupiga mnada mali zake.
Uwezo mdogo wa mtu huyu ulishajadiliwa hapa JF miaka mingi. Mwanzo ulijadiliwa sana na ulijikita kwenye ajira yake ambayo ilikuwa ni kushikwa mkono na kuajiliwa bila sababu.

Wale wageni tafuteni mwanzo huo ambao baadhi ya wachangiaji walieleza uhusiano na ukabila wa aliyekuwa Katibu mkuu kiongozi kuwatafutia ndugu na hasa wale wa Iringa kupata kazi za juu. Huyu ni wale tunaowaita 'Bi-shoo' wakati uwezo mdogo.

Tulifika mbali na hasa baada ya kujaribu kuzungumza kiingereza kikampa kisogo. Kwa lugha hiyo tukajua ni maaamuma!

Sijui anachokiweza ni nini? naona anaanza kutetewa kwa kusingizia wadeni sungu. Nani alitakiwa kuwadai??? Let's stop this shit expectation. NHC inajenga nyumba ya bei nafuu ya sh. mil 60! NONSENSE!
 
Tutasikia mengi mwaka huu, inaweza fikia ukitaka nyumba za NHC unaulizwa chama gani, Tanzania ni yetu sote
Huo ni mtizamo wako sifhani kama unaweza kuulizwa suala kama hilo kama una sifa na utafuata utaratibu.watu wengi tunachanganya siasa na mambo ya kiutendaji sidhani mbowe ana haki ya kuachwa ktk jengo hilo licha ya kuvumiliwa tena mtu ambaye ni icon mfano wa kuigwa anapigana kwa ajili ya maendeleo anakuwa wa kwanza kutolipa kodi vipi atatuhamasisha vipi wa tz kwa mambo makubwa ya kimaendeleo .kama shirika limefuata taratibu ni haki afukuzwe
 
Sasa ndio tunaanza kujua sababu za kuanzisha maandamano, alitaka kutupotezea maisha ya watanzania kisa deni lake. Maandamano yangetokea sidhani kama hii shughuli ya kumtoa ingefanyika. Majizi ni mamtu ya hatari sana
 
Mboweeeeeee! Kashikwa na kwikwi. Tuone kama ataendelea kupambana na Magufuli
We unafikir mbowe ni tajir wa ngapi tz? , hadi anahesabika katka matajir wa tz hiyo 1b ndio imfirisi? tafta orodha uone. Hata usipotafta kuwa na deni 1bn tayari we ni tajiri mkubwa tu.
 
View attachment 391870
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Mbowe Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya kampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.

Source:
Mwanahalisi Online

" Hili si suala la kisiasa..... "wadaiwa wako wengi...., lakini tumeamua kuanza na Mbowe...."
 
We hushangai kuwa Mbowe kakaa kimya sana??
NHC washatoa deatails za madeni.
Sasa ni zamu ya Mbowe kusema alilipa lini na wapi.
Inaonekana mimi na wewe hatulielewi sakata hili kwa undani, hebu tuwaachie wenyewe!
 
Labda humu JF ili swala linaonekana la uonevu lakini kwa wapangaji wa NHC wanaweza ona huyu bwana kapendelewa sana inawezekanaje deni lifike mpaka zaidi ya billioni na kwa miaka kadhaa asilipe. Ebu waulizeni majirani walio karibu na nyumba za NHC wapangaji wakawaida deni la miezi mitatu tu alizidi ata millioni tatu utapewa notisi kila kukicha na siku wakija huo utemi wa NHC anajua mungu tu. Huyu mwenzetu deni limefika mpaka billioni kweli life is not fair na bado anawatu wa kumtetea.
Hiyo pointi uliyoitumia kujenga hoja, ndio inawapa nguvu wale wanaohoji na kutilia mashaka kilichotokea! Nadhani kwa kuwa mimi na wewe na wachangiaji wengi hapa hatulijui sakata hili kwa undani ni vizuri tukasikilizia nini kitaendelea badala ya kushambulia na kukebehi upande mmoja!
 
Mboweeeeeee! Kashikwa na kwikwi. Tuone kama ataendelea kupambana na Magufuli



kumbe ni mpango wa kutokupambana na magufuli hii ina maana ya kwamba vita vya kisiasa vinahamia ktk mali za umma kwa chuki binafsi za magufuli kutokutaka kusolewa ina maana kama unataka kutumia rasimali za tiafa hovyo hupaswi kutoafautiana na magufuli lizaboni bana.
 
Ila nakumbuka zamani wakati magu akiwa wazir Mboe na maggu walikua wanaelewana sana.
Mfano ni pale wa ufunguzi wa barabara ya kwasadala.

Mkuu aliongea mambo mengi sana mazito na ukiyasikiliza kwa makini yalikua yakitoka ndani, moyoni kabisa. Akimsifu Mboe alisema

Mboe mwanasiasa jasiri na mtu mzuri sana yaani sana wa upinzani tofauti na wanasiasa wooote. Mungu akubariki..

Hata mimi, imani yangu kwa Mbowe mpaka hata nikaja kumpa kura ya Ubunge, ilitokana na maggu alivyomsifia sana siku ile.


What noww?
 
Back
Top Bottom