NHC: Hatujamuonea Mbowe

NHC: Hatujamuonea Mbowe

Tuliposema CHADEMA ni mafisadi watu walikuwa wanatubishia. Haya sasa wanazidi kuumbuka
Nitamlinda mkwere, asiwe na wasiwasi.
Kimsingi kama tunazungumzia Mafisadi haswa, basi wengi wako kule ccm. Ndipo makontena yalipokamatiwa, sukar, wauza sembe, nk.
Hata hivyo...

Kuna msemo
.Huwezi kuchungulia uch* wa baba yakwe..
 
Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Hata wakwepa kodi Chadema waliofukuzwa Leo billicanas ipo siku watatubu na kuachana na wizi wa kuwaibia watanzania.
Mkulu anapiga goti kwa nani au nini?
CeaHiwnWIAAB2jY.jpg

Exodus 20:4 "You shall not make for yourself an image in the form of anything in heaven above or on the earth beneath or in the waters below.

Deuteronomy 5:8 "You shall not make for yourself an image in the form of anything in heaven above or on the earth beneath or in the waters below.

Hapa mkulu anavunja amri au ametunga amri mpya?
Mambo ya kupiga goti hayo.
 
Ivi zile mali zilizoshikiliwa zina thamani ya Tshs 1.3 Bilioni au tutasikia mali zilizopigwa mnada azijafikia izo pesa kwa iyo wanaenda kukamata na shamba lake apo moshi na kulitaifisha kwa wahindi, wachina, au waarabu
 
Siwezi nikatetea mkwepaji kodi hapa tuache unafiki, kama ni mdaiwa sugu ashughulikiwe bila huruma kama anaonewa atashinda na NHC itaumbuka na kulipa fidia.
Hakuna anekataa mtu wahalifu wa kutolipa kodi....
Hakuna wadaiwa sugu kama serikali waambie hao Nh... wapeleke pua zao huko. Kama ubosi wao hautaisha.... hapa wanajiavhia kwa sababu ni wapinzani...
 
View attachment 391870
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya Hampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.

Source: Mwanahalisi Online

Haya hawa NDIYo viongozi wapinzani, wanakopa shirika la umma ZAIDI ya billioni je angekuwa NI eye Rais, b basi angejikopeshs kodi zote za Watanzania.
 
Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

Hii kauli ina Usiasa anway ni Vema Mbowe alipe deni
 
Suala la Mbowe ni la kibiashara zaidi. Hakufuata masharti ya kupanga. Msichanganye masuala ya biashara na siasa
kwani wadaiwa wengine wa NHC si wa kibiashara kama mbowe,wahindi kibao wanadaiwa ila hawaguswi,hii ni mchechu anatafut kiki ya kumfurahisha bwana wake ili asitumbuliwe,huwezi fanya vile tena kwa sababu ni mpinzani then udhani kuwa wa tz ni mambumbumbu na hawataelewa dhamira yako
 
Nilikataa kuwa mfuasi mnafiki...Unafiki kazi sana!!
Leo hii watu kutokana na mahaba uchwara ya chadema wanaamua kupindisha ukweli ili ionekane kwamba Mbowe kaonewa!!

Kwahiyo wapinzani wasitumbuliwe!!wasilipe Kodi,kisa eti ni wapinzani

1.3 billion ni pesa nyingi sana... hakuna msalie mtume kwa mkwepaji kodi...Mbowe alipe Kodi

Wasijifiche kwenye kivuli cha Upinzani...Nimekataa kuwa mnafiki
 
Mbona mnajitetea sana ? Si kodi hajalipa na mnaweza pia kuthibitisha hilo ,Kelele za nini ? Mara hatujamuonea ,oh sio swala la kisiasa ,hata kama sio la kisiasa ,mmekosea timing huwezi kuniaminisha shinikizo la kisiasa halijatumika wakati ambao nchi ilikuwa kwenye homa ya Ukuta Mbowe akiwa ndio Captain

ha ha! habari ndio hiyo
 
Makamanda mchangieni Kamanda Mkuu asiaibike. Hili ni suala nyeti. Kama mliweza kumchangia yule wa Arusha aliyemkashifu Rais, mtashindwaje kufanya hivyo kwa Kamanda Mkuu?
 
Mbowe aoneshe ushahidi wa kulipa kodi.

Ndio maana hata chama hakipeleki hesabu zake za mapato na matumizi kwa msajili wa vyama ili CAG akague.....
 
Kwenye list ya magazeti ya leo kwenye Milard Ayo sijaliona Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom