NHC: Hatujamuonea Mbowe

NHC: Hatujamuonea Mbowe

View attachment 391870
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa,*anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya Hampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.

“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa.

Source: Mwanahalisi Online

Kama wapo Watu wanaosema au kudhani kuwa NHC imemuonea Mbowe nadhani wanatakiwa kwenda kuziba nafasi za wale waliopo Hospitali ya Vichaa ya Milembe Mkoani Dodoma.
 
UKUTA ulikuwa umebeba mambo mengi sana niliwahi pata kusema humu ndani!!

Yaani majipu yoote yamejificha nyuma ya UKUTA!!
Lengo lao ni kutaka Magufuli asiwatumbue,asiwalipishe kodi stahiki,walitaka waendelee kula kodi zetu bila huruma..

Magufuli safisha CHADEMA....waumbue wote na madudu yao machafu wanayoyafanya kwa mwamvuli wa Upinzani
 
Huyu jamaa naona dalili zote anajiandaa kuwa rais wa Maisha wa nchi ya kufikirika, tuombe uzima kama katiba haitabadilishwa tutaona
 
Ha haa! Tanzania hatuhitaji wacheza mieleka. Hii mieleka ya kwenye siasa inatosha sana kutuburudisha... Sasa hapa Mbowe kapigwa ngwara... Ngoja asimame naye awapige Kipepsi!
 
Back
Top Bottom