A
Anonymous
Guest
Hili Shirika letu la Umeme tumeshtoa taarifa kwao kuhusu changamoto ya nguzo kukatika lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Tumeenda mbele na kuamua kuwapigia picha kabisa ya nguzo hizo na kuwatumia kwa njia ya WhatsApp lakini hakuna chochote kilicho fanyika zaidi ya mafundi wao kuja, wanaangalia, wanasema “Tunafuata nguzo”, baada ya hapo hawarudi tena.
Taarifa ya kwanza tulitoa tarehe 29/01/2024, wakatupa namba ya taarifa 5397392, walikuja kisha wakaondoka wakisema wanafuata nguzo lakini hawakuwahi kurudi tena.
Tukarudia kutoa taarifa tarehe 06/02/2024 napo wakatoa tena namba ya taarifa 5535978 lakini paka leo hii hawajaonekana.
Hizi nguzo ni hatari kwa watu wote wanaopita maeneo hasa majirani ambao tunaona muda wowote zinaweza kuanguka na kusababisha madhara.