REA wametuwekea nguzo kisha hakuna umeme mwaka mzima, TANESCO nao wamekimbia

Maguguma

Member
Mar 13, 2023
13
6
Mimi ni mkazi wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, Kitongoji cha Mwasonge, kulikuwa na mradi wa REA wa kuunganisha umeme ambapo ilielezwa kuwa utakabidhiwa kwa TANESCO baada ya kukamilika.

Cha kushangaza ni kwamba tangu REA walipomaliza na kuwakakabidhi TANESCO hadi sasa ni watu wasiozidi 15 tu, ndio waliounganishiwa umeme.

Wengine tumeendeleza kusubiri hadi sasa unakatika Mwaka mzima.

Tumewahi kujikusanya wananchi kadhaa na kwenda kuuliza lakini hakuna jibu lolote la maana ambalo tumelipata mpaka sasa, wanaishia kutuambia tusubiri mpaka watakapokuwa tayari.

Tunaomba mamlaka za juu ziingilie, inawezekana sisi ambao tupo huku vijijini hatuna nguvu ya kuwasemea. Jamii Forums tusambazieni ujumbe huu, tunateseka Wananchi wa Kata ya Idetemya.
 
Back
Top Bottom