Nguvu ya Uingereza Ulaya ni ipi exactly?

mkunga wa jadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2025
Posts
208
Reaction score
431
Unaweza kujiuliza Uingereza ipo wapi na inafanya nini, katika huu mgogoro mkubwa wa dunia, mwisho wa siku ukagundua kwamba “power” ya Uingereza ipo Google na magazetini.

Wakati Juha anaivamia Ukraine, Rais Macron alikuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kulaani uvamizi ule, kusimama na Ukraine na kuagiza vikwazo vichukuliwe dunia nzima dhidi ya Urusi.

Uingereza sijui walikuwa bado wamelala fofofo.

Rais Macron, ambaye nyuklia zake ni za Ufaransa, tofauti na nyuklia za Uingereza ambazo rimoti ipo Marekani, Macron mpaka sasa ni kiongozi pekee duniani kutangaza vita na Juha.

Uingereza bado wapo katika usingizi mzito.

Kiongozi mkuu wa mazungumzo ya amani Ukraine kwa sasa ni Rais Emmanuel Macron. Misele mingi ya Rais Zelenskyy Ulaya ni hapa Paris ambapo analala mara kwa mara. Paris imekuwa Kyiv yake ya pili. Uingereza sijui wako wapi katika hili.

Wakati Juha na Trump wanapanga dili la kwenda kugawana Ukraine kule Alaska, kiongozi pekee duniani aliyepinga hilo dili ni Rais Macron. Akasema mazungumzo ya amani ya Ukraine hayawezi kufanyika bila uwepo wa Rais wa Ukraine ambaye Juha hajawahi kumtambua kisa kafyeka majeshi yake zaidi ya milioni moja Ukraine. Kikao kilifanyika Alaska lakini agenda ikabadilishwa, kufuatia moto wa Macron.

Bado namtafuta Uingereza katika hili.

Baada ya hicho kikao cha mchongo cha Alaska, Rais pekee duniani aliyepinga Rais Zelenskyy kupewa feedback ya kikao kwa simu, kama vile Ukraine sio nchi yake, alikuwa ni Macron.

Rais Macron ndiye alilazimisha kikao cha pili White House kati ya Trump na Zelenskyy na hakuishia hapo. Akaona ili yasitokee yale ya mwezi February kati ya Trump na Zelenskyy, akakusanya viongozi wote Ulaya kutoka Uingereza, Ujerumani, Italy, EU, etc. Wakaongozana wote White House kumpa kampani Zelenskyy.

Jamani, naanza kumtafuta Uingereza kwa tochi.

Ndani ya kikao hicho, Rais Macron akapendekeza nchi zote 32 za NATO zipeleke majeshi nchini Ukraine.

Jana dili limekamilika, Rais Macron amezikusanya nchi zote za Ulaya hapa Paris, nchi 26 kati ya nchi 31 zimeweka saini kupeleka majeshi ya ardhi, ya majini na ya angani huko Ukraine. Juha tayari ameanza kulia baada ya azimio hilo la Paris.

Hatimaye tochi yangu imezima chaji… Uingereza simuoni na siwezi kumuona tena.

Kuna watu humu, baada ya ku Google, wanakwambia eti “Uingereza ndio nchi kubwa kijeshi Ulaya.” Nguvu ya Uingereza mnaweza kuniambia ipo wapi katika yote niliyozungumza hapa?

Google hiyo hiyo inatufahamisha kwamba jeshi la Congo ni la 8 Afrika, jeshi la Rwanda ni la 42. Wakati dunia nzima imeuona ukweli hapo Congo.

Huwa nawadharau sana watu wanaofanya tafiti zao kupitia Google/Wikipedia, sijui nawachukuliaje yaani.
 
Mguse kwini au king wao uone. Hapa duniani watu watatu wenye influence na ushawishi mkubwa ni papa wa kikatoliki, kwini/king wa uingereza then rais wa marekani. Huu ushawishi haiji hivihivi unaakisi pia nguvu ya kiuchumi.
 
Mwenyewe nashangaa hawa waingereza waliwezaje kutawala eneo kubwa la dunia?
Hawa jamaa ni waoga sana
 
Google haijawahi kuwa source ya data naona umeamua kusingizia google au kutokuwa na uelewa wa namna google inavyofanya kazi
 
Mguse kwini au king wao uone. Hapa duniani watu watatu wenye influence na ushawishi mkubwa ni papa wa kikatoliki, kwini/king wa uingereza then rais wa marekani. Huu ushawishi haiji hivihivi unaakisi pia nguvu ya kiuchumi.
Amna kitu
 
Uk inatembea legacy
 
Brixt walijitoa Umoja wa Europe muda sasa.
Wako kivyao
Sababu:
Mi Gaidi inakwenda omba ukimbizi nchi yoyote Europe hasa kupitia Turkey.
Wakifika wa naleta watoto na hadi babu zao wa kufa kesho.
Anawaacha hapo Europe anahamia London kuendeleza upuuzi wake.
Waligundua hiyo hila, wakajitoa na mpaka sasa ukitoka nchi yoyote EU kwenda UK unaomba Visa.
 
Hauna chochote ulichoandika ni pumba tu brixit ndiyo nini sasa,hovyo kabisa
 
Kama Rais wa Urusi unamwita juha ila hao mashoga ya Ulaya yanamuogopa,sasa angekuwa mwerevu sijui ingekuwaje!
Nalog off Z
 
Uingereza hii hii iliyotoa Javelin,ant-tank na kama sio msaada huu wa uingereza vifaru vya Urusi vingepenya kiev
 
Unaweza kujiuliza Uingereza ipo wapi na inafanya nini, katika huu mgogoro mkubwa wa dunia, mwisho wa siku ukagundua kwamba “power” ya Uingereza ipo Google na magazetini.

Wakati Juha anaivamia Ukraine, Rais Macron alikuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kulaani uvamizi ule, kusimama na Ukraine na kuagiza vikwazo vichukuliwe dunia nzima dhidi ya Urusi.

Uingereza sijui walikuwa bado wamelala fofofo.

Rais Macron, ambaye nyuklia zake ni za Ufaransa, tofauti na nyuklia za Uingereza ambazo rimoti ipo Marekani, Macron mpaka sasa ni kiongozi pekee duniani kutangaza vita na Juha.

Uingereza bado wapo katika usingizi mzito.

Kiongozi mkuu wa mazungumzo ya amani Ukraine kwa sasa ni Rais Emmanuel Macron. Misele mingi ya Rais Zelenskyy Ulaya ni hapa Paris ambapo analala mara kwa mara. Paris imekuwa Kyiv yake ya pili. Uingereza sijui wako wapi katika hili.

Wakati Juha na Trump wanapanga dili la kwenda kugawana Ukraine kule Alaska, kiongozi pekee duniani aliyepinga hilo dili ni Rais Macron. Akasema mazungumzo ya amani ya Ukraine hayawezi kufanyika bila uwepo wa Rais wa Ukraine ambaye Juha hajawahi kumtambua kisa kafyeka majeshi yake zaidi ya milioni moja Ukraine. Kikao kilifanyika Alaska lakini agenda ikabadilishwa, kufuatia moto wa Macron.

Bado namtafuta Uingereza katika hili.

Baada ya hicho kikao cha mchongo cha Alaska, Rais pekee duniani aliyepinga Rais Zelenskyy kupewa feedback ya kikao kwa simu, kama vile Ukraine sio nchi yake, alikuwa ni Macron.

Rais Macron ndiye alilazimisha kikao cha pili White House kati ya Trump na Zelenskyy na hakuishia hapo. Akaona ili yasitokee yale ya mwezi February kati ya Trump na Zelenskyy, akakusanya viongozi wote Ulaya kutoka Uingereza, Ujerumani, Italy, EU, etc. Wakaongozana wote White House kumpa kampani Zelenskyy.

Jamani, naanza kumtafuta Uingereza kwa tochi.

Ndani ya kikao hicho, Rais Macron akapendekeza nchi zote 32 za NATO zipeleke majeshi nchini Ukraine.

Jana dili limekamilika, Rais Macron amezikusanya nchi zote za Ulaya hapa Paris, nchi 26 kati ya nchi 31 zimeweka saini kupeleka majeshi ya ardhi, ya majini na ya angani huko Ukraine. Juha tayari ameanza kulia baada ya azimio hilo la Paris.

Hatimaye tochi yangu imezima chaji… Uingereza simuoni na siwezi kumuona tena.

Kuna watu humu, baada ya ku Google, wanakwambia eti “Uingereza ndio nchi kubwa kijeshi Ulaya.” Nguvu ya Uingereza mnaweza kuniambia ipo wapi katika yote niliyozungumza hapa?

Google hiyo hiyo inatufahamisha kwamba jeshi la Congo ni la 8 Afrika, jeshi la Rwanda ni la 42. Wakati dunia nzima imeuona ukweli hapo Congo.

Huwa nawadharau sana watu wanaofanya tafiti zao kupitia Google/Wikipedia, sijui nawachukuliaje yaani.
Uingereza ni issue nyingine, mgogoro wowote ambao mwingereza anashiriki kuutatua lazima uishe. Waingereza ni wazee wa mikakati na techniques vibaya mno. Umewahi juuliza nchi ndogo kama ile iliwezaje kuitawala dunia! USA ni maguvu tu lakini haiwafikii waingereza kwa mbinu za kiutawala.
 
Google haijawahi kuwa source ya data naona umeamua kusingizia google au kutokuwa na uelewa wa namna google inavyofanya kazi
Mara nyingi watu wamefungwa na google wanalishwa kile wanachokitafuta ama kukuhitaji, na sio wanachopaswa kukipata!

Huwezi kumkuta mchina anatafuta taarifa google na kuacha kutumia Baidu

Ama mrusi atafute taarifa google aache kutumia Yandex.

Ukweli mwingi unaopaswa kujulikana umekuwa censored na google purposely!
 
Anatembelea Legacy Tu, si kwamba ni mwepesi hapana, Bali uzito ule Hana tena. Uingereza Yuko na Marekani. Anachosema US jua uingereza naye atakubaliana nacho.
 
Back
Top Bottom