Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,416
- 28,178
Kadiri miaka inavyoenda ndivyo umuhimu wa China unazidi kuonekana duniani, Mchina ana soft power moja inayokua kwa kasi sana.
China haihitaji kuanzisha unnecessary wars and conflicts duniani kama Marekani to prove how powerful it is.
China haihitaji kuanzisha unnecessary wars and conflicts duniani kama Marekani to prove how powerful it is.
Chinese strategy; do nothing and win game theory.
Tangu November 2025 hadi May 2026, viongozi wengi wa Ulaya na mataifa mengine wamefanya ziara rasmi au za ngazi ya juu kwenda China.
Na hawa ndio waliotajwa zaidi katika taarifa za habari:
1. Felipe VI – Mfalme wa Hispania, November 2025.
- Alikutana na Xi Jinping na viongozi wengine wa China ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara.
2. Emmanuel Macron – Rais wa Ufaransa, Desemba 2025
- Lengo lilikuwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Ufaransa.
3. Micheál Martin – Waziri Mkuu wa Ireland, January 2026.
- Hii ilikuwa ziara ya kwanza ya kiongozi wa Ireland nchini China katika miaka 14.
4. Keir Starmer – Waziri Mkuu wa Uingereza, Januari 2026.
- Alikutana na Xi Jinping ili kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Uingereza na China. Ilipita miaka 8 tangu Waziri Mkuu wa mwisho wa Uingereza kutembelea China.
5. Petteri Orpo – Waziri Mkuu wa Finland, Januari 2026.
- Ililenga ushirikiano wa biashara, teknolojia na mazingira.
6. Friedrich Merz – Kansela wa Ujerumani, Februari 2026.
- Ilihusisha mazungumzo kuhusu biashara, teknolojia na siasa za kimataifa.
7. Pedro Sánchez–Waziri Mkuu wa Spain, April 11-15 2026
- Alikutana na rais wa China Xi Jinping na kujadili ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya Ulaya na China.
8. Tô Lâm – Rais wa Vietnam, April 14–17 2026
- Alikutana na Rais wa China Xi Jinping kujadili ushirikiano wa kiuchumi, miundombinu (hasa reli), teknolojia na usalama
9. Donald Trump — Raisi wa Marekani, May 13-15
- Alikutana na Xi Jinping ziara ya siku 3 ililenga kudumisha utulivu katika uhusiano wa Marekani na China, ikilenga mazungumzo ya kibiashara, suala la Taiwan na Hormuz.
10. Vladmir Putin — Raisi wa Urusi, May 19-20
- Kuongeza ushirikiano wa kimkakati na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili. Kujadili masuala muhimu ya kimataifa na kikanda. Kusaini tamko/joint declaration la kuonyesha msimamo na ushirikiano wao wa pamoja baada ya mazungumzo.
Kwa sasa Xi ndiye the most powerful person in the world.