Nguvu iliyotumia CCM kujiimarisha ingetumika nusu yake tu kuimarisha uchumi wa nchi tungekuwa mbali sana kiuchumi kama taifa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Ccm inajisufu na kujitutumua kuwa ni chama kikubwa sana Afrika, kwa kuangalia historia wafuasi na mtindo wake wa kubadili viongozi wao kwa njia ya amani na utulivu.

Hata hivyo makusudi makubwa ya chama chochote duniani ni kwa ajili ya kushinda uchaguzi ili kuunda serikali na kushika dola. Lengo kuu la kushika dola ni kuiongoza serikali kuwatumikia wananchi ili kuwaletea hali bora za maisha kutokana na kodi za wananchi.

Jambo hili limekuwa kinyume sana kwa ccm ambayo imefanikiwa kutumia Kila mbinu kushinda uchaguzi na kushika dola ila nguvu inayotumika kushinda uchaguzi ni ya hali ya juu sana Kwa kiwango ambacho inaihujumu nguvu ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Linapokuja suala la uchaguzi kwa ccm ni suala la kufa na kupona yaani wako tayari kufanya chochote maadamu chama kishinde uchaguzi. Ukifuatilia historia utagundua kwamba hata kashfa nyingi za ufisadi mkubwa katika nchi yetu misingi yake ni uchaguzi.

Natamani ccm ifike mahali pa kuwa na hii commitment yanapokuja mambo ya kuletea nchi maendeleo yaani kwamba iwe iwavyo wananchi wapate maendeleo, hakika taifa letu laweza kugeuka na kuwa giant la Africa.

Nachukizwa sana na misifa ya kijinga ya kusifia chama eti ni kikongwe kina wafuasi wengi kimeshika dola kina sera zinazotekelezeka nk. Sasa kama uchumi wetu unakua Kwa mwendo wa kinyonga hizi sifa zote za nini? Hii ni sawa na kuwa na baba anajisifu kuwa kazaa mtoto tajiri sana mwenye uwezo mkubwa lakini huyu baba hana uhakika wa kula. Kwangu mimi hii sio sifa ila ni jambo la kujionea aibu.
 
Ni chama ambacho Mafuvu ni yale yale.
skeleton-head-less.gif
 
CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NCCR n.k hizi ni taka taka 🚮 .

Tanzania hatuna vyama kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake bali tuna magenge ya mafisadi yaliyo kusanya wanachama wapumbavu kwa manufaa yao binafsi.

: Siasa za Afrika ni taka taka na laana kubwa😡.
 
CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NCCR n.k hizi ni taka taka .

Tanzania hatuna vyama kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake bali tuna magenge ya mafisadi yaliyo kusanya wanachama wapumbavu kwa manufaa yao binafsi.

: Siasa za Afrika ni taka taka na laana kubwa.
Nimewaita kuwa ni "TUMBOCRASIA" au Tumbocrazier!
 
CHADEMA walipewa makombora ya 'Himaras' na mabeberu lakini wakashindwa kuyatumia kushinda uchaguzi...
Usiseme CCM walitumia nguvu nyingi.
Walitumia nguvu za dola 'ndio'
Ila hata CHADEMA nao, walitumia nguvu nyingi. Ila wao walitumia nguvu za mabeberu...
 
Back
Top Bottom