Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana
Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.
Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..
Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??