Sheria ya ulinzi inakataza raia yoyote kuvaa Mavazi yanayofanana na Jeshi lolote la Tanzania kwa rangi ama mshono. Kadhalila inakataza askari wa Jeshi A kuvaa au kufananisha uniform za Jeshi B bila kibali. Ukienda dukani au kwenye mitumba ukimkuta nguo yoyote inayofanana na Jeshi lolote Tanzania ,achana nayo tafuta nyingine inayoendana na wewe. Lengo la sheria hii ni kuthibiti matumizi mabaya ya uniform ambazo wahalifu wanaweza kuzitumia au kujitambulisha kama ni wahusika wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa watu wasiojua na kufanya uhalifu.
Ewe msanii uwe wa maigizo au wa nyimbo epuka kuvaa nguo zinazofanana na za majeshi yetu
Ewe mwanasiasa achana kabisa na mashono ya majeshi au kushona vitambaa vinavyofanana na rangi za nguo za majeshi
Ewe mmiliki WA kampuni binafsi ya ulinzi hakikisha uniform za wafanyakazi wako hazifanani na za majeshi yaliyoamishwa na sheria ya nchi
Mkuu ni rangi ngapi ambazo ni marufuku haturuhusiwi kuvaa sisi raia?
Maana ninavyojua rangi ambazo huvaliwa katika sare za majeshi yetu ni nyingi sana.
Kuna nyeupe, nyeusi, nyekundu, njano, kijani, light blue, light green, ugoro, kijivu nk nk, yaani ni yingi mno na ndiyo hizo rangi za vitambaa vya suti zimejaa madukani!
Kwa mfano mimi napenda kutinga suruali ya kitambaa ya polyster jeupe lisilokuwa na madoa, kwa hiyo Traffic Police akiniona apite na mimi?
Karibia rangi zote nilizozitaja, suruali zake ninazo kwa hiyo nikaziteketeze?!
Basi angalao tuwekeeni vifungu vya sheria vinavyotoa haki miliki kwenu ninyi wanajeshi kuhodhi rangi hizo.
Maana isije kuwa ni vita vya kibiashara ambayo mnaipigana bila kujua.
Kuna kodi ya Serikali katika biashara ya nguo ujue!