Nguo zenye rangi ya Jeshi

Nguo zenye rangi ya Jeshi

Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana

Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.

Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..

Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??

Sasa kofia ya nchi nyingine inahusiana nini na kofia la hapa kwetu!! sasa nasema hivi nitaagiza na nitavaa, just wait! Kama sijaripoti kwa mkubwa wao
 
Huku wanasheria nyingi za hovyo ni kwasababu wanajihisi wapo insecure.

Kuna jamaa nilimuona pale feli akijipiga selfie, kumbe kulikuwa na mjeshi yuko juu ya mti anaangalia watu.

Yule mjeshi akashuka akamuita yule jamaa akampigisha magoti mbele za watu, mjeshi akawa anasikika akisema "kwanini unapiga picha kwenye maeneo ya ikulu"

Jamaa kwa upole akajibu "samahani najua ikulu ipo kule juu sikujua kuwa hadi huku haturuhusiwi kupiga picha"

Mjeshi akachukua simu ya jamaa akafuta zile picha akamrejeshea, baada ya pale nikamuona yuke mjeshi anaenda kupanda juu ya mti tena kwa ajili ya kuchunguza watu.

Nilishangaa sana nikajiuliza maswali mengi, mbona kina Maulid Kitenge wanaenda hafi kwenye vibaraza vya ikulu ya Marekani na kupiga picha?

Na kuna muda unakuta anafanya mahojiano na wadau waliopo eneo hilo la ikulu na hakuna tatizo?

Sisi tumeficha nini pale ikulu kiasi kwamba kuwe na sheria ngumu hivyo?
Mkuu ikulu mbali,hata kwenye vituo vya mwendokasi wanakamata watu wanaopiga picha
 
Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana

Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.

Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..

Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??
Askari yeyote aliyehudhuria mafunzo ya kijeshi na kufuzu hutenda jambo lolote kwa amri, kinyume cha hapo ni utovu wa nidhamu ya kijeshi na huadhibiwa kijeshi kupitia MPs.
 
Unachanganya kuvaa sare ya jeshi na kuvaa nguo zenye rangi rangi kuvaa kofia au pensi wala suruali bado sio sare ya jeshi mkuu uwezi vaa kofia ya rangi ya jeshi na raia waseme ni mwanajeshi itakua wendawazimu
Kwann uvae mavazi ya mfano wa uchungaji Hali wewe sio
 
Huyo kibaka alovaa kofia ya jeshi alipaswa kuvuliwa nguo zote abaki uchi, watanzania mmekuwa viburi sana, vibaka kama hao nikiwakuta sehemu yoyote nawatia mbata nawavua nguo zote

uje ujichanganye kwangu nikukamue kinyesi hiko
 
Sheria ya ulinzi inakataza raia yoyote kuvaa Mavazi yanayofanana na Jeshi lolote la Tanzania kwa rangi ama mshono. Kadhalila inakataza askari wa Jeshi A kuvaa au kufananisha uniform za Jeshi B bila kibali. Ukienda dukani au kwenye mitumba ukimkuta nguo yoyote inayofanana na Jeshi lolote Tanzania ,achana nayo tafuta nyingine inayoendana na wewe. Lengo la sheria hii ni kuthibiti matumizi mabaya ya uniform ambazo wahalifu wanaweza kuzitumia au kujitambulisha kama ni wahusika wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa watu wasiojua na kufanya uhalifu.

Ewe msanii uwe wa maigizo au wa nyimbo epuka kuvaa nguo zinazofanana na za majeshi yetu

Ewe mwanasiasa achana kabisa na mashono ya majeshi au kushona vitambaa vinavyofanana na rangi za nguo za majeshi

Ewe mmiliki WA kampuni binafsi ya ulinzi hakikisha uniform za wafanyakazi wako hazifanani na za majeshi yaliyoamishwa na sheria ya nchi

mbona nchi nyengine wanavaa na hakuna shida? Wabongo bano tuishi 60's
 
mbona nchi nyengine wanavaa na hakuna shida? Wabongo bano tuishi 60's
Ukiona mtu anaanza sentensi na neno " Mbona" ujue ana tatizo kubwa kwenye ubongo wake ( defect in reasoning) na yeye hajijui. Changamoto za kiulinzi za Kila nchi zinatofaitiana. Sheria za nchi zinatofaitiana. Tanzania tumepakana na nchi nyingi zenye political instability.
Ukiruhusu raia kutumia VIFAA vya Jeshi lolote duniani ndani ya jamhuri ya muungano utaleta maafa. Swali ni kwanini nguo za majeshi tuu?

Kwa nini usivae nguo za maiti ( sanda)?

Kwa nini usivae nguo za wafungwa wa kunyongwa ( condemn)?

Kwa nini usivae nguo za wagonjwa waliolazwa hospitali?

Kwa nini usivae uniform za manesi ? Mbona za Jeshi Kuna nini?
 
Kimsingi sio kudai kitambulisho tu,bali ni kumdai kitambulisho cha Askari jeshi yani MP,ndio mwenye mamlaka chini ya kifungu cha sheria kumkata mtu yoyote hata akikuhisi tu kuwa unaweza leta shida yoyote..Mwanajeshi kama sio Askari Jeshi (MP) huyo hana mamlaka ya kukamata
Nakazia
 
Kimsingi hairuhusiwi...

Kitu pekee kilichozua zogo hapo labda ni mjeda kukosa hekima ya namna ya kumsanua huyo aliyevaa kwamba kakosea...
 
Majeshi karibia yote duniani nguo zao zinafanana, zinatofaitiana tu kwenye maichorl ya mabaka ila zote kwa mbali zinaonekana kama zinafanana. Nyingi za za nchi kavu huwa na mabaka ya kijani, kwa nchi za jangwani ndio huwa na rangi kama ya maziwa.

Lengo la sheria ya kuthibiti raia kuvaa Mavazi ya Jeshi au yanayofanana na majeshi yetu ni kuepuka abuse ambapo mtu anaweza kujitambulisha kwa raia WASIOELEWA kuwa ni askari na kufanya uhalifu. Pili ni kuepuka abuse ya nguo hizo kwani hata uvaaji wake una mafunzo yake.

kwani jeshi ameruhusika wapi kufanya abuse?
 
Huku wanasheria nyingi za hovyo ni kwasababu wanajihisi wapo insecure.

Kuna jamaa nilimuona pale feli akijipiga selfie, kumbe kulikuwa na mjeshi yuko juu ya mti anaangalia watu.

Yule mjeshi akashuka akamuita yule jamaa akampigisha magoti mbele za watu, mjeshi akawa anasikika akisema "kwanini unapiga picha kwenye maeneo ya ikulu"

Jamaa kwa upole akajibu "samahani najua ikulu ipo kule juu sikujua kuwa hadi huku haturuhusiwi kupiga picha"

Mjeshi akachukua simu ya jamaa akafuta zile picha akamrejeshea, baada ya pale nikamuona yuke mjeshi anaenda kupanda juu ya mti tena kwa ajili ya kuchunguza watu.

Nilishangaa sana nikajiuliza maswali mengi, mbona kina Maulid Kitenge wanaenda hafi kwenye vibaraza vya ikulu ya Marekani na kupiga picha?

Na kuna muda unakuta anafanya mahojiano na wadau waliopo eneo hilo la ikulu na hakuna tatizo?

Sisi tumeficha nini pale ikulu kiasi kwamba kuwe na sheria ngumu hivyo?

waafrika ni watu wapumbavu sana
 
Back
Top Bottom