Nguo zenye rangi ya Jeshi

Nguo zenye rangi ya Jeshi

Kuna mdada mmoja alikutwa mtaani kavaa kipedo chenye rangi za kombati za jeshi wakamvua kibabe. Askari magereza nao waliwahi kuleta za kuleta kwa makonda wa daladala wakidai wamewaiga sare zao. Polisi nao waliwahi kuliamsha dude wakipiga mkwara sare zao zisivaliwe na raia hata kwenye sanaa

Ndio tofauti kubwa ya nchi za dunia ya tatu na zilizoendelea! Mambo ya msingi hatuna muda ila vitu kama hivyo ndio unashangaa mtu anapigwa!
 
Tatuzo makuruta mnahasira sana mbona maofisa wenu hawana habari au ugumu wa maisha mkuu Yani uachane na ratiba zako uanze kugombana na watu?
Ni ujinga tu mkuu si unajua hawa wa vyeo vya chumvi hata shule ni zile za super glue pana dogo mmoja yeye ni shule na yeye yeye na shule za kijeshi ukimwambia hizo mambo anacheka anakwambia mambo za JKT hizo vijana wetu hakuna mjeda anaeweza kufanya hivyo...
 
Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana

Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.

Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..

Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??
Ni ushamba, ulimbukeni na ushamba tu hakuna kingine

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana

Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.

Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..

Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??
Dogo nilikusamehe halafu umekuja kuninanga hapa jeiefu. Ningejua ningekufyatua tu
 
Kutokana na Ugumu wa, maisha kila mtu anatafuta Mnyonge wake ili aweze Kuonesha umwamba wake na kumaliza stress zake.

Jambo kubwa ni kuacha tu kuvaa hizo nguo
 
Huyo kibaka alovaa kofia ya jeshi alipaswa kuvuliwa nguo zote abaki uchi, watanzania mmekuwa viburi sana, vibaka kama hao nikiwakuta sehemu yoyote nawatia mbata nawavua nguo zote
Nawapendaga wajeda njaa kama wewe niwadhalilishe kwa kipondo hevi maana najua medal akiwa mwenyewe huwa Ana maajabu ndio maana mjeda akitandikwa anakimbilia kambini kwao kuomba msaada wa wenzie.

Mjeda akiwa alone anakuwaga kama kolo tu, jichanganye siku moja uingie mkenge wangu nikukande boksi za kiume nikuadhiri mbele ya umma.

Awatakiwi wasio raia kuyavaa sababu wengine wanafanyia uhalifu

Unachanganya kuvaa sare ya jeshi na kuvaa nguo zenye rangi rangi kuvaa kofia au pensi wala suruali bado sio sare ya jeshi mkuu uwezi vaa kofia ya rangi ya jeshi na raia waseme ni mwanajeshi itakua wendawazimu
 
Katika umri wangu huu nimeshuhudia sana askari magereza, Polisi, uhamiaji, zimamoto wanapenda sana kuvaa nguo zenye rangi za JWTZ wakiwa nje ya majukumu, ila sijawahi kuwaona wakiwa nje ya kazi wamevaa nguo zinazofanana na mgambo, JK hata za zile magereza hivi kwa nini wakivaa za JWTZ wanajiona superior?
Ni kinyume na sheria, ushamba na ulimbukeni kwa anayefanya hivyo
 
Habari za muda huu Wana Jf..
Leo katika pitapita zangu mitaa ya "Daslamu" nmekutana na tukio ambalo limenifikirisha sana

Ni hivi nmekuta kijana kavaa kofia yenye rangi za Jeshi,kakamatwa na mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mwanajeshi",kofia aliyeivaa kijana ni kweli Ina rangi za Jeshi lakini ni Jeshi la china,Ina alama ya nyota hapa mbele, na maneno haya "Chieng Du, aviation school" huku pembeni ikiwa na maneno ya kichina.

Sasa utata huyu bwana aliyejitambulisha kwamba yeye ni "mjeda" akawa anataka kumuweka chini ya ulinzi kijana,kijana akadai id ya huyu mjeda apo ndo zogo likaanza,mjeda ID hatoi,kijana hakubali kuwa chini ya ulinzi..

Sasa apa wajuzi wa Mambo mnisaidie je Kuna Sheria hio ya "wajeda" kumvua mtu vazi na kuchukua Sheria mkononi?na Kama haipo ikitokea mtu anapaswa aende wapi kupata haki yake??

Kimsingi sio kudai kitambulisho tu,bali ni kumdai kitambulisho cha Askari jeshi yani MP,ndio mwenye mamlaka chini ya kifungu cha sheria kumkata mtu yoyote hata akikuhisi tu kuwa unaweza leta shida yoyote..Mwanajeshi kama sio Askari Jeshi (MP) huyo hana mamlaka ya kukamata
 
Huyo mjeda si angetoa tu kitambulisho ili mjadala unoge vizuri
 
Kama zinafana na jeshi la kolombia
Majeshi karibia yote duniani nguo zao zinafanana, zinatofaitiana tu kwenye maichorl ya mabaka ila zote kwa mbali zinaonekana kama zinafanana. Nyingi za za nchi kavu huwa na mabaka ya kijani, kwa nchi za jangwani ndio huwa na rangi kama ya maziwa.

Lengo la sheria ya kuthibiti raia kuvaa Mavazi ya Jeshi au yanayofanana na majeshi yetu ni kuepuka abuse ambapo mtu anaweza kujitambulisha kwa raia WASIOELEWA kuwa ni askari na kufanya uhalifu. Pili ni kuepuka abuse ya nguo hizo kwani hata uvaaji wake una mafunzo yake.
 
Majeshi ya zamani alafu wengi wao ni wanajeshi wale Darasa la saba sasa mtu kavaa kofia ya kufanania tu we unamuogopea nini? Hajui silaha hana kozi yoyote.
Madhala ya kukosa vita hata vya kirafiki kunasababisha wanajeshi wetu kuanza kutafuta ma timberland trousers mtaani.
 
Huyo kibaka alovaa kofia ya jeshi alipaswa kuvuliwa nguo zote abaki uchi, watanzania mmekuwa viburi sana, vibaka kama hao nikiwakuta sehemu yoyote nawatia mbata nawavua nguo zote

Tafuta ela Mkuu ukiwa na mawazo ya kijinga kiasi hicho ni kwamba huna ela.

Wajeda wanaojielewa humkuti anafanya huo upuuzi, kwanza akitoka job anawahi mishe zake muda wa kugombana na vijana wa mtaani anapata wapi?

Kuna wale askari PT na Cpl wachache ndo wenye huu upuuzi hawana majukumu wala kazi ya kufanya nje ya jeshi
 
Zinauzwa mitaa za nini?

Si zingeuzwa jeshini huko ambako ndio wavaaji maalumu walipo?

Kama nguo za jeshi ni biashara ya magendo basi iwekee wazi watu wajue hata wakiwa huko china wasijisumbue kununua nguo hizo.

Kabisa ,ni huku bara la giza ndiyo wana mawazo migando ,yaani kigezo chao eti mtu akivaa nguo zinazofanana na jeshi eti akifanya uhalifu atalichafua jeshi mbona wanajeshi wanafanya mambo ya ajabu kitaani,jana msoja kapandishwa kwa pilato kwa kuhujumu miundombinu ya tehama ,kuna komandoo aliua kisa raia alimtongoza demu wake ,kuna msoja mwingine alienda kunyang'anya TV kisa simu.

Uhalifu hauhusiani na mavazi ,mtu akitaka kufanya uhalifu anafanya tu bila kuvaa mavazi hayo ,US kitaani raia wanavaa hayo mavazi bila kuwa na shida yeyote.
 
Huku wanasheria nyingi za hovyo ni kwasababu wanajihisi wapo insecure.

Kuna jamaa nilimuona pale feli akijipiga selfie, kumbe kulikuwa na mjeshi yuko juu ya mti anaangalia watu.

Yule mjeshi akashuka akamuita yule jamaa akampigisha magoti mbele za watu, mjeshi akawa anasikika akisema "kwanini unapiga picha kwenye maeneo ya ikulu"

Jamaa kwa upole akajibu "samahani najua ikulu ipo kule juu sikujua kuwa hadi huku haturuhusiwi kupiga picha"

Mjeshi akachukua simu ya jamaa akafuta zile picha akamrejeshea, baada ya pale nikamuona yuke mjeshi anaenda kupanda juu ya mti tena kwa ajili ya kuchunguza watu.

Nilishangaa sana nikajiuliza maswali mengi, mbona kina Maulid Kitenge wanaenda hafi kwenye vibaraza vya ikulu ya Marekani na kupiga picha?

Na kuna muda unakuta anafanya mahojiano na wadau waliopo eneo hilo la ikulu na hakuna tatizo?

Sisi tumeficha nini pale ikulu kiasi kwamba kuwe na sheria ngumu hivyo?
 
Back
Top Bottom