Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Serikali hutenga fungu la dharura katika bajeti yake yaani "contigence" hilo ndio lilitumika.
Usipotoshe ukweli kuna dharura gani kwenye swala la Ngorongoro? Pesa ya dharura ni kwa ajili ya majanga kama mioto mikubwa, mafuriko, baa la njaa magonjwa ya mlipuko nk
 
Wewe unaishi mizizi yako ilipo? Kila yako ilipo? Tamaduni zako zilipo?

Hakuna nchi ambayo watu hawahamishwi

Tuache ushabiki mandazi

Hata kule kwetu ikoma… ya 1967 siyo ya leo
 
Kuna watu wapo maeneo sasa hivi wanagonga glass, "mission accomplished "!
 
Kaongea vizuri sana, na mimi sipendi utekaji wowote

Lakini katofautisha kuzuia wamasai kuchunga kwrnye hifadhi vs wamasai kuishi kwenye hifadhi

Secondly, our country population inakua exponentially, tusipokua na njia njema ya kuzuia watu kusambaa kila kona… hata hiyo ikolojia itakufa kabisa

Maybe tatizo kubwa ni tukishaondoa wamasai, nini kinafuata

I would preserve land Kwa ukubwa wowote ule unaowezekana ili kuwatengea future wajukuu wa wajukuu wangu

Developed countries wala hawana demokrasia kwenye kuhifadhi ardhi
 
Mongela:Serikali itawasaka wote wanaohujumu Zoezi la Uwekaji Mipaka Pori Tengefu Loliondo

Na Mwandishi wetu Loliondo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa Serikali itawasaka wote watakaohujumu zoezi la uwekaji mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo hasa aliyehusika katika mauaji ya askari wilayani Ngorongoro, katika zoezi la uwekaji mipaka katika eneo hilo.

Amewataka wote waliohusika na tukio la mauaji ya askari polisi kujisalimisha katika kituo cha Polisi vinginevyo ajue hayuko salama.

Amesema hayo leo Juni 12, 2022 wakati wa kuaga mwili wa marehemu Garlius Mwita eneo la Loliondo, wilaya ya Ngorongoro ambapo mwili umeagwa kuelekea nyumbani kwa Musoma Mkoa wa Mara.
IMG-20220612-WA0442.jpg
 
Eeh kumbe huku Ni Ngorongoro kule ni visiwa! Something, somewhere is wrong

 
Dawa ni kuwaondoa CCM, leo wamewafanya wamasai watumwa na wakimbizi ndani ya nchi yao kesho wewe, na kuna umbwa humu wanatetea eti wamasai wapigwe tuu maana wamepewa viwanja na nyumba handeni sijui wapi, wamekaa pale mamia ya miaka leo mnawaita wakimbizi/wavamizi na kuwaua? CCM will pay big time for this ni swala la muda tuu
 
Ieleweke kwamba huko hawaishi masai tu....tutumie neno wananchi, watanzania au wakazi
Ahsante sana
 
Inaumiza sana, nchi hii hakuna mzalendo na hamna mwenye hari ya kuipenda nchi yake ,kila mtu anavuta kwa urefu wa kamba ndomana jpm alisema historia ya tanzania lazima ifundishwe.ndomana kuna makundi ya waasi wanaibukaga. walaniwe wao na vizazi vyao washenzi waliofanya hili, na dhambi hii ya dhuruma isiache koo zao.
Tulisema mwanzo kuwa nani anaelewa mama anakotupeleka? Wakadai mama anaupiga mwingi.

Leo kodi juu, bei za bidhaa juu na nchi imeanza kumegwa.

Wamasai kwao kumekuwa ughaibuni.
 
Deal done..!
Mark my words!
Hizi za sasa ni purukushani za muda tu na kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji..!
Ngorongoro is no longer ours..and maybe be it will never be ours again ..! Nani anakumbuka ya Loliondo? Pamoja na kelele zote zile haikuwahi kurudi kwetu...!

Siku ile pm alipoenda Arusha na ile list ndefu ya Wamasai waliokubali kuhamia ugenini huko Handeni Tanga... Ndio ilikuwa hitimisho la kuiaga Ngorongoro..

Ule mkutano
Zile picha
Yale majina
Zile video
Vyote vimechukuliwa na kuhifadhiwa vizuri kwamba kila kitu kilifanyika kwa kuzingatia haki za binadamu, matakwa ya kisheria nknk..

Hawa waliopelekewa moto leo wanahesabika kama wavamizi na ndio maana jeshi la polisi lilienda kule.. Na trust me kile kilichifanyika asubuhi ya leo ni salam tuu.. Ile ni kifungua kinywa tuu.. Full menu ya bufee itawaendea usiku kukiwa kuna kiza kinene. Hapo ndio shetani atasimamia ukucha...

Kesho yaweza kuwa siku ya kuokota mizoga, majeruhi vituo vya afya, watuhumiwa kwenye selo za polisi, na matukio ya watu kupotea huko Ngorongoro national park.

Kwa wiki chache zijazo safisha safisha itaendelea kuondoa masalia yote ya kitu kinachoitwa Wamasai wa Ngorongoro wavamizi.. Tutawekwa busy na unit za umeme kupaa, kesi za sabaya na drama zingine zote..!

Itakapofika 30/6 ndio itakuwa mwisho wa kuiona Ngorongoro uliyozoea kuiona japo kwa picha tangu ukiwa mdogo.. Kama una picha zake ama ulibahatika kufika kule na kupata kumbukumbu kadhaa..ZIHIFADHI VEMA..Hiyo bahati haipo tena!

Hakuna picha zake zitapatikana tena huko kwa uhuru na kujiachia, hakuna selfies tena za mbuga yetu ile urithi wetu...picha zitapigwa na watu maalum..! Na kwa sababu maalum...!

Na wazawa watakaoruhusiwa kuingia kule ama ni mamluki ama ni wafanyakazi wasio huru,.. Itakuwa ni kama watumwa katika nchi yao wenyewe!

Tusitaharuki zaidi, tusilie, bali tuanue tanga.. Msiba ulishaisha kwasasa tusubiri kusomwa historia ya marehemu.. Tukipata wasaa tutawasimulia wana wetu picnic, na study tour za kishule wakati pale pakiwa kwetu..
sasa wewe Ngorongoro imekusaidia nini kwa miaka yote tangu uzaliwe? si bora iuzwe
 
Back
Top Bottom