Ng'o,mbe wa maziwa hukamuliwa mara ngapi kwa siku?

Ng'o,mbe wa maziwa hukamuliwa mara ngapi kwa siku?

Kayoka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
2,407
Reaction score
2,265
Habari wana MMU!!

Jamani mwenzenu nina ng'ombe nimemleta hapa nyumbani wiki iliyopita. Ng'ombe huyu nilimnunua huko Mkoani Ruvuma miezi tisa iliyopita ila niliamua kumuacha kwanza huko akue na anenepe kidogo ndipo nimlete mjini ili nimfuge mwenyewe kwani kwa kipindi chote hicho nilikuwa bado sina uwezo wa kumtafutia nyasi za kula na madawa ya kumchoma hasa ukizingatia nilikuwa bado pia sina banda la kumfugia.

Sasa naomba msaada wenu kwa wenye ng'ombe wa maziwa mabandani mwenu, ni mara ngapi kwa siku (mchana/usiku) inatakiwa ng'ombe akamuliwe maziwa..!!?

Naomba tuelekezane hapa wadau ili nipate somo mwenzenu nimkamue ng'ombe wangu bila kumkondesha wala kumfanya apauke katika kipindi kifupi tangu nimuweke zizini

Halafu ni vyakula gani ng'ombe wa maziwa ale ili kumpa nguvu na uwezo wa kuvumilia pale anapokamuliwa?

Je, ni muda gani haswa hawa ng'ombe wanatakiwa wakamuliwe haswa i.e asubuhi mchana, jioni, usiku au alfajiri?

Je, kama mkaenda machungani na huyu ng'ombe wa maziwa inafaa kukamuliwa huko huko au sharti umlete zizini kwako halafu ndo umkamue?

Je, mkamuaji naye mambo gani ayazingatie ili amkamue ng'ombe kwa umaridadi na umakini zaidi?
 
Utapata majibu hayo mpaka utajuta kuileta hii post huku...!! wengi wa wachangiaji watafikiri tofauti kabisa wakiiona tu heading na baadhi watachangia bila hata ya kusoma post yote
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Utapata majibu hayo mpaka utajuta kuileta hii post huku...!! wengi wa wachangiaji watafikiri tofauti kabisa wakiiona tu heading na baadhi watachangia bila hata ya kusoma post yote

Sawa mkuu!
Upi uzoefu wako katika kuwakamua hawa ng'ombe wa maziwa?
Au mwenzangu bado hujafuga mpaka sasa na hupendi kabisa kukamua?
 
Peleka jukwaa la biashara. Hapa ni mahusiano mapenzi na urafiki, labda kama una uhusiano wa kariiiibu na ng'ombe wako............samahani lakini!
 
Peleka jukwaa la biashara. Hapa ni mahusiano mapenzi na urafiki, labda kama una uhusiano wa kariiiibu na ng'ombe wako............samahani lakini!
Duh sasa we unadhani ataletaje post bila kuwa na uhusiano na ng'ombe wake?
 
Peleka jukwaa la biashara. Hapa ni mahusiano mapenzi na urafiki, labda kama una uhusiano wa kariiiibu na ng'ombe wako............samahani lakini!

usilolijua ni sawa na usiku wa giza totoro...!!
Kuna watu kama akina Excel wameshanisoma kitambo.

Nauliza hv "unamkamua mara ngapi kwa siku ng'ombe unayemfuga mwenyewe bandani kwako?
 
Sawa mkuu!
Upi uzoefu wako katika kuwakamua hawa ng'ombe wa maziwa?
Au mwenzangu bado hujafuga mpaka sasa na hupendi kabisa kukamua?
Kwakweli nilifuga zamani nimesahau kila kitu nikumbukacho ni lishe bora hasa pumba na kuna kitu kinaitwa jiwe la chumvi anapewa alambe na maji safi kwa wingi
 
we mkamue tu deile ili asipate maziwa yakakamuliwa na wezi mpe majani akisiba tu kamua
 
we mkamue tu deile ili asipate maziwa yakakamuliwa na wezi mpe majani akishiba tu kamua
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza totoro...!!
Kuna watu kama akina Excel wameshanisoma kitambo.

Nauliza hv "unamkamua mara ngapi kwa siku ng'ombe unayemfuga mwenyewe bandani kwako?
Kwakweli hata mimi sijakusoma ulilenga nini ndo maana honestly nimecoment kwenye ufugaji halisi
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza totoro...!!
Kuna watu kama akina Excel wameshanisoma kitambo.

Nauliza hv "unamkamua mara ngapi kwa siku ng'ombe unayemfuga mwenyewe bandani kwako?

Lol, kwa hiyo binadamu mwenzio ndo ukampa sifa ya ng'ombe? Hata kama tafsida na tashbiha basi yako imezidi.
Kama ndo ng'ombe huyo mkamue kila unapojisikia, iwe barabarani, kitandani, sebuleni, jikoni, malishoni, bafuni, kwenye gari hata mbele ya wageni ukijisikia we kamua tu. Akiona anateseka mwenyewe atarudi kwao.
 
Hahaaaa ng'ombe akamuliwa popote ati, hata machungani akiwa na maziwa kamua sio mpaka bandani, we mlishe akishiba funga kamba miguu ya nyuma kamua, hata usiku wa manane kama vipi amka umkamue la sivyo majirani watamkamua we usipokua mkamuaji mzuri. Tena ng'ombe wa ruvuma wana maziwa mengi kwerikweri
 
Habari wana MMU!!
Jamani mwenzenu nina ng'ombe nimemleta hapa nyumbani wiki iliyopita.
Ng'ombe huyu nilimnunua huko Mkoani Ruvuma miezi tisa iliyopita ila niliamua kumuacha kwanza huko akue na anenepe kidogo ndipo nimlete mjini ili nimfuge mwenyewe kwani kwa kipindi chote hicho nilikuwa bado sina uwezo wa kumtafutia nyasi za kula na madawa ya kumchoma hasa ukizingatia nilikuwa bado pia sina banda la kumfugia.
Sasa naomba msaada wenu kwa wenye ng'ombe wa maziwa mabandani mwenu eti ni mara ngapi kwa siku (mchana/usiku) inatakiwa ng'ombe akamuliwe maziwa..!!?

tena kamua kama hivi kwa ng'ombe wa vijijini
 
Uwe unamnywesha maji ya vuguvugu ili kiu kisikatike ambapo atakunywa maji kwa wingi sana, matokeo yake atatengeneza maziwa mengi na kukufanya upate lita za kutosha!!
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza totoro...!!
Kuna watu kama akina Excel wameshanisoma kitambo.

Nauliza hv "unamkamua mara ngapi kwa siku ng'ombe unayemfuga mwenyewe bandani kwako?

acha ufala wewe..
 
hapa kuna neno naona kama vile ni message behind the message kwa sisi wana fasihi tumeelewa kaka we mkamue kila anapojisikia hamu pia kutegemea na afya yake
 
Ng' ombe wako kamua kila anapokuwa na hamu....
hakikisha unampa pumba, shudu, maji ya vuguvugu na mpe jiwe la kulamba lenye calcium asije toka bambani na kujua wenziwe wapewa nni.
Ukitegemea wa kijiji mkame Mara kwa Mara cos bado ana nguvu.
Mtunze vizuri michepuko no jua ng' ombe wako ndo mzuri na mwenye maziwa matamu
Loooo fasihi heee kazi kwel kweli
 
Tafuta mkamuaji! Mi ntajitolea aisee, muhimu awe na nido za ukweli na amenona sana hasa kunapohusika!
 
Back
Top Bottom