Ngeleja atajwa kuchota fedha TPDC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja atajwa kuchota fedha TPDC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njowepo, Nov 19, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Saturday, 19 November 2011

  [​IMG]
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja Bungeni Dodoma jana

  KAMATI ya Nishati na Madini ya Bunge imeanika uozo katika uendeshaji wa sekta ya gesi nchini, huku ikiitaja Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd (PAT) kufanya udanganyifu mkubwa ulioikosesha Serikali mabilioni ya shilingi.

  Kamati hiyo ilifanya uchunguzi jinsi sekta hiyo inavyoendeshwa kupitia kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Diana Chilolo na kubaini kwamba PAT ilifanya udanganyifu unaofikia Dola za Marekani 64 milioni (Sh110 bilioni).

  Akisoma taarifa hiyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Mbunge wa Bukene (CCM), Selemani Zedi alisema ukaguzi uliofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ulibaini kuwa PAT walijirudishia fedha hizo kama gharama walizotumia kuzalisha gesi kati ya mwaka 2004 na 2009.

  "Kati ya hizo Pan African Energy Tanzania Ltd wamekiri kwamba wamejirudishia isivyo halali kiasi cha Dola za Marekani 28.1 milioni ambazo ni sawa na Sh46 bilioni na kwamba kiasi cha Dola 36 milioni zilizobaki (sawa na Sh64 bilioni) wanaandaa vielelezo vya kuthibitisha uhalali wa kujirudishia gharama hizo," alisema Zedi.

  Kutokana na kubaini ufisadi huo, kamati hiyo imependekeza kusitishwa kwa mkataba baina ya TPDC na PAT na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika na udanganyifu ambao umeikosesha Serikali gawio la Dola 20.1 milioni sawa na Sh35 bilioni.

  Alisema miongoni mwa njia zilizotumiwa kufanya ufisadi huo ni katika malipo ya kusafirisha gesi ambako PAT ilijipatia kiasi cha Dola za Marekani 20 milioni.

  Aliitaja njia nyingine kuwa ni kuweka gharama za uzalishaji wa gesi katika nchi za Nigeria, Gabon na Uganda inakofanya kazi hiyo katika gharama za hapa nchini, hivyo Tanzania ikawa inabeba gharama zote kutoka katika nchi hizo.

  Zedi alisema Kamati hiyo pia inataka fedha ambazo PAT ilijilipa kinyume cha sheria na taratibu, zirejeshwe mara moja serikalini na kwamba Wizara ya Nishati na Madini lazima isimame kidete kutetea maslahi ya taifa kwa kushirikiana na TPDC.

  "Mpaka Kamati inaandaa ripoti hii, Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd, imeshindwa kuwasilisha uthibitisho wa uhalali wa kujirudishia gharama nyingine zinazofikia jumla ya Dola za Marekani 36 milioni, hali hii inaonyesha shaka kubwa katika uendeshaji wa sekta ya gesi nchini," alisema Zedi na kuongeza:

  "Kitendo cha PAT kuchukua gharama ambazo haikustahili na hatimaye kuisababishia Serikali na TPDC hasara, ni uzembe wa hali ya juu na ni uvunjivu wa sheria za nchi."

  Kamati hiyo ilibainisha kuwa tatizo kubwa katika sekta ya gesi ni kutokuwepo kwa sheria inayosimamia sekta hiyo na badala yake kutumia sheria ya petroli ambayo ina mianya mingi inayoruhusu ufisadi.

  Fedha za mafunzo
  Taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya Nishati na Madini pia ilibaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa na TPDC kwa ajili ya kusomesha wataalamu wa shirika hilo na wale wa wizara katika sekta ya nishati hiyo.

  Zeli aliliambia Bunge kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilipokea kiasi zaidi ya Sh1.5 bilioni kutoka TPDC ambacho ni asilimia 50 ya fedha zilizokusanywa lakini fedha hizo zimekuwa zikitumika kinyume cha sheria.

  "Kwa mujibu wa vielelezo kutoka TPDC, inaonekana kuwa Sh 20 milioni zilitumika kama mchango wa maandalizi ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2010/2011 na fedha nyingine zimetumika kulipia tiketi za ndege."

  Imebainika kwamba Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alichukua kiasi cha Sh76.8 milioni kwa ajili ya safari, fedha zilizotolewa na TPDC Mei 6, 2010. Kwa mujibu wa kielelezo namba 19 cha taarifa hiyo, matumizi hayo ya Ngeleja yameandikwa kwa Kiingereza ‘Travel on Duty Minister for Energy and Minerals.'

  Kielelezo hicho kinaonyesha kuwepo kwa matumizi mengi ya fedha hasa za safari za kwenda nje ya nchi kwa watendaji kadhaa wa wizara hiyo, matumizi ambayo ni kinyume cha malengo ya fedha hizo.

  Baadhi ya matumizi yaliyoko kwenye kielelezo hicho ambacho pia ni sehemu ya taarifa iliyowasilishwa bungeni na kiasi cha fedha kwenye mabano ni fedha zilizolipwa kwa shughuli za wizara Julai 1, 2009 (Sh40 milioni) na marejesho ya gharama za tiketi ya ndege kwa aliyekuwa Kamishna wa Petroli wizarani hapo Bashir Mrindoko (Sh5.42 milioni), Septemba 9, 2009.

  Fedha nyingine zilikwenda kwa ofisa aitwaye P. Victus ambaye Oktoba 8, 2009 alilipwa posho ya safari (Perdiem) Sh3.97 milioni, Oktoba 28, 2009. Yalifanyika pia malipo kwa Victus na Shilla yab Sh5.3 milioni na fedha za kununua tiketi za ndege kwa maofisa wa wizara ya Nishati na Madini Sh14.3milioni.

  Desemba 3, 2009 kulikuwa na safari ya kikazi kwa maofisa wa wizara kwenda India ambayo iligharimu kiasi cha Sh10 milioni, wakati Desemba 7, mwaka huo kulikuwa na vikao vilivyoitwa ‘ACM' ambavyo viligharimu kiasi cha Sh17.1milioni na kingine Sh24.8milioni.

  Kadhalika, malipo ya Sh13.2 milioni yalifanyika kwa safari za maofisa ambao hawakutajwa, wakati Januari 21, 2010 kiasi cha Sh4.1 kilitumika kwa ajili ya malazi na mkutano ambao pia haukuelezwa kuwa ni wa nini.

  Januari 27, 2010 kulikuwa na malipo ya posho kwa Wizara ya Nishati na Madini kiasi cha Sh85.8 milioni, Februari 23, 2010 kiasi cha Sh5.5milioni kikatumika kulipa gharama za tiketi ya ndege na Septemba 22, 2010 kiasi cha Sh14.84 kilitumika kwa ukarimu katika mkutano wa masuala ya nishati uliofanyika nchini Mexico.

  Chimbuko la uchunguzi

  Kamati ya Nishati na Madini ilipewa kibali cha kufanya uchunguzi huo na Spika wa Bunge, Anne Makinda baada ya kueleza nia yake katika taarifa kuhusu maoni yake kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Julai 15, mwaka huu.

  Uchunguzi huo ulianza Septemba 5, mwaka huu ulifanywa na Kamati ya Wajumbe tisa, Christopher Ole Sendeka (Simanjiro - CCM), Chilolo (Viti Maalumu -CCM), Yusuph Abdallah Nassir (Korogwe Mjini - CCM), Mwanamrisho Abama (Viti Maalumu - Chadema), David Silinde (Mbozi Magharibi - Chadema), Mbarouk Salum Ali (Wete - CUF), Sarah Msafiri (Viti Maalumu - CCM) na Zedi.

  Uchunguzi wa Kamati hiyo ulijikita katika mkataba baina ya Serikali na Songas, pamoja na ule unaoipa Kampuni ya Pan African Energy mapato makubwa yanayotokana na uzalishaji wa petroli (Production Sharing Agreement), badala ya fedha hizo kwenda TPDC.

  CHANZO: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Safi kwa kuwagundua, kwanza watulipe pesa zetu, pili wafukuzwe mara moja. Sasa nimeanza kupata logic kwanini serikali iliamua kwenda China kukopa pesa za kujenga bomba lake la gesi.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa wanajua serikali yetu ni legelege
   
 4. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sio legelege bali ni corrupt kuanzia Naibu Waziri, Waziri mpaka Ikulu...haiingii akilini kuwa miaka yote hii hakuna hata siku moja waziri au hata naibu wake amewahi kuhoji pesa zinakwenda wapi?
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Pan ni ya rostam!na ofisi zipo jengo la ra mirambo 50
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,673
  Likes Received: 82,523
  Trophy Points: 280
  KAMATI ya Nishati na Madini ya Bunge imeanika uozo katika uendeshaji wa sekta ya gesi nchini, huku ikiitaja Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd (PAT) kufanya udanganyifu mkubwa ulioikosesha Serikali mabilioni ya shilingi.

  Kamati hiyo ilifanya uchunguzi jinsi sekta hiyo inavyoendeshwa kupitia kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Diana Chilolo na kubaini kwamba PAT ilifanya udanganyifu unaofikia Dola za Marekani 64 milioni (Sh110 bilioni).

  Akisoma taarifa hiyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Mbunge wa Bukene (CCM), Selemani Zedi alisema ukaguzi uliofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ulibaini kuwa PAT walijirudishia fedha hizo kama gharama walizotumia kuzalisha gesi kati ya mwaka 2004 na 2009.

  "Kati ya hizo Pan African Energy Tanzania Ltd wamekiri kwamba wamejirudishia isivyo halali kiasi cha Dola za Marekani 28.1 milioni ambazo ni sawa na Sh46 bilioni na kwamba kiasi cha Dola 36 milioni zilizobaki (sawa na Sh64 bilioni) wanaandaa vielelezo vya kuthibitisha uhalali wa kujirudishia gharama hizo," alisema Zedi.

  Kutokana na kubaini ufisadi huo, kamati hiyo imependekeza kusitishwa kwa mkataba baina ya TPDC na PAT na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika na udanganyifu ambao umeikosesha Serikali gawio la Dola 20.1 milioni sawa na Sh35 bilioni.

  Alisema miongoni mwa njia zilizotumiwa kufanya ufisadi huo ni katika malipo ya kusafirisha gesi ambako PAT ilijipatia kiasi cha Dola za Marekani 20 milioni.

  Aliitaja njia nyingine kuwa ni kuweka gharama za uzalishaji wa gesi katika nchi za Nigeria, Gabon na Uganda inakofanya kazi hiyo katika gharama za hapa nchini, hivyo Tanzania ikawa inabeba gharama zote kutoka katika nchi hizo.

  Zedi alisema Kamati hiyo pia inataka fedha ambazo PAT ilijilipa kinyume cha sheria na taratibu, zirejeshwe mara moja serikalini na kwamba Wizara ya Nishati na Madini lazima isimame kidete kutetea maslahi ya taifa kwa kushirikiana na TPDC.

  "Mpaka Kamati inaandaa ripoti hii, Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd, imeshindwa kuwasilisha uthibitisho wa uhalali wa kujirudishia gharama nyingine zinazofikia jumla ya Dola za Marekani 36 milioni, hali hii inaonyesha shaka kubwa katika uendeshaji wa sekta ya gesi nchini," alisema Zedi na kuongeza:

  "Kitendo cha PAT kuchukua gharama ambazo haikustahili na hatimaye kuisababishia Serikali na TPDC hasara, ni uzembe wa hali ya juu na ni uvunjivu wa sheria za nchi."

  Kamati hiyo ilibainisha kuwa tatizo kubwa katika sekta ya gesi ni kutokuwepo kwa sheria inayosimamia sekta hiyo na badala yake kutumia sheria ya petroli ambayo ina mianya mingi inayoruhusu ufisadi.

  Fedha za mafunzo
  Taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya Nishati na Madini pia ilibaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa na TPDC kwa ajili ya kusomesha wataalamu wa shirika hilo na wale wa wizara katika sekta ya nishati hiyo.

  Zeli aliliambia Bunge kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilipokea kiasi zaidi ya Sh1.5 bilioni kutoka TPDC ambacho ni asilimia 50 ya fedha zilizokusanywa lakini fedha hizo zimekuwa zikitumika kinyume cha sheria.

  "Kwa mujibu wa vielelezo kutoka TPDC, inaonekana kuwa Sh 20 milioni zilitumika kama mchango wa maandalizi ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2010/2011 na fedha nyingine zimetumika kulipia tiketi za ndege."

  Imebainika kwamba Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alichukua kiasi cha Sh76.8 milioni kwa ajili ya safari, fedha zilizotolewa na TPDC Mei 6, 2010. Kwa mujibu wa kielelezo namba 19 cha taarifa hiyo, matumizi hayo ya Ngeleja yameandikwa kwa Kiingereza ‘Travel on Duty Minister for Energy and Minerals.'

  Kielelezo hicho kinaonyesha kuwepo kwa matumizi mengi ya fedha hasa za safari za kwenda nje ya nchi kwa watendaji kadhaa wa wizara hiyo, matumizi ambayo ni kinyume cha malengo ya fedha hizo.

  Baadhi ya matumizi yaliyoko kwenye kielelezo hicho ambacho pia ni sehemu ya taarifa iliyowasilishwa bungeni na kiasi cha fedha kwenye mabano ni fedha zilizolipwa kwa shughuli za wizara Julai 1, 2009 (Sh40 milioni) na marejesho ya gharama za tiketi ya ndege kwa aliyekuwa Kamishna wa Petroli wizarani hapo Bashir Mrindoko (Sh5.42 milioni), Septemba 9, 2009.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Unfortunately, hiyo ndiyo hali halisi ya Tanzania; nchi ambayo kazi kubwa ya serikali ni kuwadhibiti wanasiasa wa upinzani badala ya kusimamia majukumu yake sahihi kama haya ya kutunza raslimali na mapato halali ya nchi.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,673
  Likes Received: 82,523
  Trophy Points: 280
  We acha Mkuu yaani hawa jamaa wanathubutu kuoverstate operational costs zao kwa kutubebesha/kutubambikia gharama zao za uendeshaji katika nchi nyingine (Nigeria, Gabon na Uganda) ili waendelee kutuibia mabilioni yetu lakini kule Nishati na Madini hakuna hata aliyeshtuka wote wamechapa usingizi.
   
 9. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  dah! Hii ni hatari sana,yaani tunaibiwa kweupeeee mbuzi anakula majani! Watz tupotupo tu. Nalog off
   
 10. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  .......Ngeleja ww ni kijana, tufisadi kwa hatua, utuache tujikune hata wa kujikuna tu pale utakapotufanya tuwashwe, usiwe kama wazee ambao wao kimsingi huona sisi wote ni maamuma na kutudanganya kizamani, haya bwana!
   
 11. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  NAAMINI KATIKA HILI KILA MTANZANIA (ANAYEITAKIA NCHI MEMA) ATAPENDA KUONA HAWA WEZI WANAFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUFILISIWA MALI ZAO.
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]

  [/TR]
  [TR]

  [/TR]
  [/TABLE]
  'Sack them'
  • Parliamentary probe committee's report fingers Luhanjo, Ngeleja, Malima, Jairo and Utouh

  Sunday, 20 November 2011
  By Florence Mugarula, The Citizen Reporter
  Dodoma.

  Parliament yesterday called for stern disciplinary measures, including dismissal, against five senior government officials, among them Energy and Minerals minister William Ngeleja and Chief Secretary Philemon Luhanjo.

  Also mentioned in the report of a parliamentary select probe committee tabled in Dodoma were Controller and Auditor General (CAG) Ludovick Utouh, suspended Energy and Minerals Permanent Secretary David Jairo and deputy minister Adam Malima.

  In a heated and sometimes emotional debate on the last day of the fifth sitting of Parliament, MPs bayed for the blood of the five after they were implicated in embezzlement, forgery and cover-up of corruption at the ministry.

  MPs who debated the report said they were shocked at its findings and urged the President crack the whip to rid the government of corrupt officials and show that it was committed to good governance.

  Committee chairman Ramo Makame tabled the report after investigations were instituted in August into allegations that Mr Jairo had dubiously collected over Sh400 million to influence the passage of his ministry's budget.

  Yesterday's debate was reminiscent of the 2008 report on the infamous Richmond emergency power scandal, popularly referred to as the ‘Mwakyembe Report', that prompted the resignation of the then Prime Minister, Mr Edward Lowassa, and Cabinet ministers Nazir Karamagi and Ibrahim Msabaha.

  Mr Makame (Tunduru North-CCM) said Mr Jairo abused the powers of his office and irregularly collected millions and misappropriated tens of millions of shillings. The PS was accused of abetting theft at the ministry, with findings showing that he approved fraudulent allowance claims by senior officials.

  The committee said in its 150-page report that Mr Ngeleja should either shoulder responsibility and resign or be sacked by the President for presiding over impropriety at the ministry and its agencies.

  Mr Luhanjo, who is based at State House, was accused of deliberately suppressing the truth to get Mr Jairo off the hook. Mr Luhanjo and Mr Utouh, who has in recent years won praise for his annual government audit reports, was accused of coming up with findings the committee felt were misleading and only aimed at exonerating Mr Jairo.

  The committee suggested that disciplinary measures be taken against Mr Luhanjo, who is a presidential appointee. Mr Utouh on the other hand, should be investigated as to why he gave misleading findings and advice after he was asked to investigate the Jairo saga by Mr Luhanjo.

  Mr Makame said the committee interviewed 146 people and collected 32 official documents during its investigation.

  He said the ministry planned to spend Sh207 million to facilitate the tabling of the budget, Sh171 million of which was collected from agencies on the orders of the PS.

  He said while 69 was the actual number of ministry officials assigned duties in Dodoma during the tabling of and debate on the Energy and Minerals budget, this was inflated to 243 individuals, who were supposedly paid Sh127 million in five days.

  "There were 182 ghost officials in attendance," Mr Makame said, adding allowances were inflated by up to 400 per cent.

  He said ministry officials brazenly used seminars to steal public funds. "Funds were set aside to pay for the Pius Msekwa Hall in Dodoma, but it is common knowledge that the venue is available free of charge to MPs. While only 150 MPs attended one of the seminars organised by the ministry, records showed that allowances were paid to 350 parliamentarians," Mr Makame said.

  Allowances paid to each participant ranged from Sh20,000 to Sh80,000, but figures were altered to show Sh120,000 and 180,000. Moreover, ministry records show that officials used 15 vehicles in Dodoma and that each car used 230 litres of fuel a day.

  "The committee could not find documents to account for Sh126 million of the Sh418 million collected by the ministry," Mr Makame said, adding that both the minister and his deputy were paid Sh4 million each as entertainment allowance.

  According to the report, Tanesco, Ewura, Rural Energy Agency (REA) and TPDC contributed the cash. Mr Makame said Tanesco contributed Sh40 million, TPDC Sh50 million, REA Sh50 million and Ewura paid Sh9.7 million for food and drinks.

  The committee chairman told Parliament that officials in the agencies said they feared losing their jobs if they did not release the money.

  MPs were unanimous that action must be taken to protect the integrity of the government and independence of Parliament.

  The Leader of the Official Opposition in Parliament, Mr Freeman Mbowe, said there was a need to investigate all ministries, adding that misappropriation and outright theft of public funds was widespread in the government.

  Mrs Beatrice Shellukindo (Kilindi-CCM), who in July read out in Parliament a damning letter that Mr Jairo sent to various agencies under the ministry, said MPs should demand concrete action.

  She said the government must undertake major changes to promote accountability.

  Mr Ezekiel Wenje (Nyamagana-Chadema), Mr James Lembeli (Kahama-CCM), and Mr Moses Machali (Kasulu Urban-NCCR-Mageuzi) said Mr Ngeleja and his subordinates must leave office immediately.

  Mr Machali went further, saying: "I think the President and Prime Minister must also think of resigning if they will fail to deal with this matter effectively."

  Ms Anne Kilango (Same East-CCM) said state officials were sinking the nation deeper into poverty through greed.

  "This is just one ministry…what if we look into others? It is time we acted to stop this theft by permanent secretaries if we are to serve the public diligently," she said, and warned against the State's tendency to ignore parliamentary resolutions.

  Mr Hamad Rashid (Wawi-CUF) said the CAG had tarnished his good name, while Mr Christopher ole Sendeka (Simanjiro-CCM) asked President Kikwete to suspend all those adversely mentioned in the report.

  Mr Tundu Lissu (Singida East-Chadema) said it was time to change the country's leadership, adding that it had continuously failed Tanzanians.

  Responding, the Minister in the President's Office responsible for good governance, Mr Mathias Chikawe, said the government would implement the recommendations made in the report
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ngoja tusubiri cinema hii itaishia wapi. Magamba siku zote huwa siyaamini kabisa.
   
 13. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Komredi Ngereja uwazri huo wasubiri hiii njooo mtaani ulitusahau watu wa sengerema
   
 14. n

  nyangasese Senior Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Laana ya kuitesa familia yatima ya Mwanza itakuandama maisha yako yote ngeleja.Hao yatima hujui wazazi wao wamehangaika vipi kuipata hiyo nyumba.Huo ufisadi serkalini umeamua kuhamishia sasa kwenye nyumba za watu.Ninaandaa makala na picha kuhusu manyanyaso na vitisho wanayopata hao vijana ktk kutetea nyumba yao kuporwa na waziri na diwani wa ccm
   
 15. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Wako macho sana na wanajua watendalo. corruption ndugu yangu. nchi iko mifukoni mwa wafanyabiashara.
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Interesting you're being paid 4 million for entertaiment and allowance.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yooooooooooote haya JK anayajua maana ana intelijensi nk ila kayabariki ni wenzake hao akisema tu nao wataanza kumwaga leak la nguvu kwa waandishi so nani wa kuwagusa ?
   
 18. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Tumefikia hapo si kwa bahati mbaya bali ni tamaaa za viongozi wetu, katika nchi za ulaya na marekani siasa si chanzo cha utajiri bali ni kazi ya heshima wakati afrika ni kinyume chake watu wamekabidhiwa madaraka mwaka mmoja tu nimesikia humuhumu tayari wana mayutong kama kumi hivi. Madhara yake ni kwamba mtu kama muwekezaji akishagundua udhaifu wako basi umekwisha maana atakuwa hakuheshim tena na ikibidi yeye ndio anakuwa juu kimaamuzi anakuwa bosi wako, how come sisi tukalipie gharama za Nigeria na kwingineko? Na haya ni asilimia 2% tu ya uozo uliopo kwa watendaji wetu hapo hujagusa mashirika ya umma na taasisi za serikali hukosasa unaweza kuwehuka!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zitto alisema kweli na sasa waziri kaumbuka!
   
 20. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mimi nina wasiwasi Rostam sio binadamu wa kawaida! Kumbe Ngeleja hana sababu ya kuwa na mawazo he is in safe hand.
   
Loading...