Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 731
- 658
Kituo cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) kinachopangwa Morogoro kinafungua fursa mpya katika sekta ya usafirishaji, kwa kuwezesha magari na vyombo vingine kutumia nishati mbadala yenye gharama nafuu na rafiki kwa mazingira. Serikali kupitia TPDC imepanga kuweka kituo cha CNG katika eneo la Chuo cha Ardhi Morogoro, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo na kupunguza gharama za uendeshaji wa magari.