Ngawaiya: CHADEMA wanapewa pesa na Marekani kuchochea fujo

Kila mti watakimbilia na kung'ang'ania.....! lakini kwa kuwa siku ya kufa nyani mti yote huteleza, basi na kila watakapokimbilia na kujaribu kung'ang'ania patateleza tu, na hivyo watadondoka tu.......! Walipekua kila kona ya nchi na dunia wakitafuta walau ukweli wowote wa kutungia wimbo, lakini wamekwama...... Na sasa wanaendelea kupekua kila kona ya dunia kutafuata walau uwongo wa kuwapumbaza Watanzania ili wapate kujinusuru na anguko lao siku za usoni...... Lakini kwa kuwa uwongo siku zote haujengi, basi watazidi kujimalizia wenyewe bila kujua....!
 
Mzee kumbe **** kiasi hicho, anashndwa kutofautsha vitu knachofanyika north ni uasi wa kuikataa govt. Naomba HIYO STATEMENT CDM WASII'UPUUZIE KWA KUSHIRIKIANA NA BALOZI YA MAREKANI WATOE TAMKO HATUA WANAZOCHUKUA
 
Na yeye Ngawaiya atueleza kapewa Pesa na nani leo aje kueleze haya.

Kwa sasa Ngawaiya ni mtumba wa kisiasa.
Hana cha kutueleza.
 
Hizi ni porojo kama porojo nyingine tu. Kwani hawezi kutaja mpaka sasa wamepokea kiasi gani? zimepitia benki gani? Tusikubali tugeuzwe taifa la tetesi na majungu. Yaani mtu anaamka tu na kuanza kuhisi vitu kama yuko ndotoni! Mara CCM wanalindwa na majini, mara CDM wamepewa hela waandamane! Upuuzi mtupu
 
CCM maji yamewafika shingoni....hawaachi kutapatapa....wanafanya kila wanaloweza kuhakikisha wanaipaka chadema matope..hamtudanganyi tena,tumechoka na siasa zenu za maji taka..siku zote mbinu za ccm ni kuchafuana.hii inatokea hata wao kwa wao dats why hata kwao kuna majungu majungu na makundi....acha wasali sala zao za mwisho
 
Hawa watu sijui wanamatatizo gani wakiambiwa wathibitishe kauli zao wanaingia mitini.wanaropokaropoka tu.
 
Amekaririwa na ITV kwenye taarifa ya saa tano na robo usiku huu

Jina lake kamili ni Thomas Ngawaiya, aliwahi kuwa mbunge wa Moshi vijijini kwa tiketi ya TLP, baada ya kukorofishana na Mrema akajisalimisha ccm

Ameongea kwa kutumia wadhifa wake wa Mkiti wa wazazi wa ccm mkoa wa Kilimanjaro

Amesema yeye na MREMA waliwahi kupewa pesa na serikali ya marekani ili wachochee vurugu tz watu wauane ili nchi ionekane ni ya machafuko kama kenya. Amesema alikuja pesa na kuanzisha maandamano sana Dar

Amesema baadaye Mrema alimwambia kwamba hizi pesa wanazopewa kuanzisha vurugu kwenye nchi Yao wakati wamarekani wamekaa kwao kwa amani hazifai. Wakawakatalia wamarekani halafu mrija wa pesa ukakatwa.

Amesema ni staili hiyo wamarekani wametumia kuleta uasi huko afrika kaskazini. Kwamba Hapa tz wamewapatia Chadema hizo pesa ili wachochee uasi Kama ule wa afrika kaskazini. Kwamba ndo maana Chadema "wanachochea vurugu" kwa sababu wameshalipwa pesa.

Alikuwa anaongea kwa kujiamini huku akieonekana kama yuko kwenye group activity fulani, sikuina vizuri, labda walikuwa wanapanda miti.

Huyu uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo sana, tena ni mroho wa madaraka kama Mrema. hana kipya. anyway napita tu.:smow:
 
Dah/// siamini haya kumbe uyu mzee ana zeeka vibaya.kama pesa kwa ajiri ya kun;goa mafisadi mbona poa sana ata 2na kuwekw kwenye risti ya watakao ngorewa upo
 
ngawaiya akumbuke tambwe alikuwa anaongea sana leo kama kafa vile kimya kabisa asitafute umaarufu kupitia cdm yetu
 
Huyu babasio njaa zinazomsumbua? Anahangaika sana na siasa halafu anaishia kuwa kichekesho.Inafika mahala ni muhimu kuanza kulea watoto maana siasa za kudandia kwenye ulaji ambazo ndio zinawasukuma walio wengi huwa zinafikia kikomo.
Familia inakuhitaji acha kutudanganya muheshimiwa
 
Nasema hongera chadema kwa kupokea hizo fedha maana katika fedha hizo tunaonja matunda ya kudai uhuru kwa mijitu mieusi uhuru wa pili baada ya ule wa wakoloni ,huyo ngwaiya ni malaya wa siasa ameolewa na bwanake sisiemu .tumempuuza hanamaana hizo habari alipaswa kumwambia mjukuu wake ama nyenya wake hata mwandishai wa Itv anapaswa kuchunguzwa kama ana akili nzuri kutuletea habari ambayo imekosa sifa alipaswa kumhoji vieelelezo vya ushahidi kuhusu upokeaji wa fedha hizo.uje mbele yetu ni lini fedha ziliingia ,kiasai gani cha fedha ,zilipitia account ipi na benki ipi ache kuropoka .
 
Iwe wanapewa na US, wanapewa na Babu wa Loliondo au Wanachukua mifukoni mwao, jambo la msingi hapa ni ukweli na uhalisia wa yale wanayoyapigania kwa niaba ya Watanzania waliochoka kudanganywa.

Mi nililidhani Ngawaiya angesema wameiba na angekuja na ushahidi. Lakini jambo jingine ni kwamba, wazee kama hawa tushawachoka na maneno yao ya kujikomba kwa CCM. CCM wameiba na ushahidi tumeletewa hadi humu JF mbona hakusema, wakatudanganya kujivua gamba, ni wizi unaendelea.

We need change and the change is to come now when we want it.

CDM mwendo mdundo, tupo pamoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom