Ngasa kwenda west ham!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngasa kwenda west ham!!

Discussion in 'Sports' started by Baisha, Mar 20, 2009.

 1. Baisha

  Baisha Member

  #1
  Mar 20, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  naona dogo bahati zinamdondokea tuu!wadau kama hayo ni ya kweli naomba dogo apewe ushauri na ajengwe kisaikolojia,vile vile ajifue vya kutosha kabla hajaenda.kila la kheri kijana!!
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa mkuu habari inaonekana nzuri, tatizo hujaweka background i.e facts za kutosha au ungetwambia umesoma kny gazeti fulani au mtandao etc tuelewe vizuri kinachoendelea! Anyway labda ni tetesi, pengine kuna members wanadetails zaidi!
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Atakalia benchi mpaka atoe malengelenge!!!!
   
 4. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  IN SHORT,tanzania bado haijawa na mchezaji wa ku cheza premier league
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Tawilee!!! Kiwango cha akili zao kinalingana na kiwango cha mpira wanaocheza bongo hapa....huwezi kuingiza mtu Ngasa kwenye premier...
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  source please!
   
 7. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Wadau hii ni tetesi tu nadhani. Sheria za uhamiaji zinaweka wazi kwamba kibali cha foreign professional footballer kitatolewa endapo mchezaji anatokea kwenye nchi ambayo ni ya at least 70 kwenye FIFA ranking, kwa maana hiyo kama wewe u mtanzania hata uwe unakipiga kama Pele- visa hupati. Most of PL clubs watakachofanya kama kuna mchezaji mzuri kwenye nchi ambayo hai qualify ni kumsajili mchezaji huyo na kum loan out kwenye ligi nyingine ndogo za Ulaya kama Belgium au Swiss then after 3 year ndani ya EU wanagain hiyo qualification na ndipo wanawachukua.
   
 8. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  mambo ya michezo tanzania inabidi tushabikie kama burudani,lakini in reality tanzania hakuna michezo.hivi tumewahi pata medali ya GOLD katika olympics.kenya na uganda nadhani wanazo gold nyingi tu.ukiondoa filbert bayi katika commonwealth games hatuna cha ziada.footballwise mimi naona its just a big ZERO
   
 9. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Habari ya Ngasa iko kwa gazeti la Mwananchi.

  Mrisho Ngassa aalikwa Uingereza kwa majaribio West Ham
  Na Mwandishi Wetu

  TIMU kongwe inayoshiriki Ligi Kuu ya England, West Ham United imempa mwaliko wa majaribio ya wiki mbili, winga wa Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngassa.

  Majaribio hayo yamepangwa kuanza Aprili 13 kwa mujibu wa Katibu wa West Ham United, P.R. Barnes.

  Barua ya klabu hiyo kwa Yanga kupitia wakala wa FIFA, Bakhressa, Ngassa atagharimiwa kila kitu na timu hiyo wakati wote wa majaribio hayo.

  Majaribio hayo yatakuwa chini ya idara ya ufundi ya West Ham inayoongozwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Italia, Giafranco Zola.

  Kwa mujibu wa nakala ya barua hiyo, Ngassa anatakiwa kufika England kabla ya tarehe hiyo na maandalizi ya mazoezi hayo yamekwisha kamilika.

  Uongozi wa Yanga ulithibitisha kupokea mwaliko na kusema wametoa ruhusa kwa Ngassa kwenda kujiunga na timu hiyo.

  Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema kuwa hawana tatizo na suala hilo kwani wakala wa FIFA aliyekuwepo hapa na klabu hiyo wamefuata utaratibu ambao unakubalika.

  “Kumbuka tulimzuia Ngassa kwenda klabu ya Ligi daraja la pili ya Lov Ham ya Norway kutokana na ukiukwaji wa sheria, wakala wa FIFA ametupa taarifa na tumepokea barua ya timu, hapa hakuna jinsi, na nasema tunampa ruhusa kwa ajili ya majaribio,” alisema Kisasa.

  “Tayari West Ham wanawasiliana na sisi na wakala wa FIFA, huu ni mwanzo wa uhusiano mpya katika masuala ya kimichezo, tunafarijika sana na tunamwombea Ngassa afanye vyema kama ilivyokuwa kwa Nonda Shaaban,” alisema.

  Hata hivyo, Ngassa huenda akakwamba kuchezea timu hiyo kwa kuwa Tanzania haiko kwenye 75 bora duniani kwa mujibu wa taratibu za usajili wa wachezaji England. Tanzania ni ya 105 kulingana na viwango vya ubora FIFA.

  Kocha wa Polisi, John Simkoko alisema kuwa amepoteza mchezo na ni sehemu ya mchezo wakati kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema kuwa wachezaji wake wamecheza vizuri ndiyo maana wameshinda.

  Source: Mwananchi Read News
   
 10. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ni west ham ya hapa hapa Africa ama ninayoijua mimi. Please, wekeni data kwa anayejua zaidi tuone uhalisia wa hili
   
 11. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  NIMESEARCH,kwenye various websites,nimedraw blank,naona hii ni juhudi ya gazeti la mwananchi to shift a few extra copies to the unsuspecting public who dont know they are being taken for a ride
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ana umri gani vile?

  ...matarajio ya Tanzania kutoa mchezaji mwenye uwezo wa kucheza EPL, Serie A, au La Liga, utatokana watoto waliokulia, waliozaliwa/wataozaliwa kwenye nchi hizo...full stop!

  Kuna watanzania wengi tu waliolowea katika nchi za ulaya, na marekani, ...hopefully baadhi yao watakuja kutuwakilisha hapo baadae, kama Senegalese, Nigerians, Morrocans, etc...

  Mpaka sasa ni Kalimangonga Ongala tu, anaehesabika kuwa ni mchezaji wa Tanzania anayecheza Nje, ....wekeni dual nationality, hata waliochukua uraia wa nchi za EU na America waje watusaidie, tena hata kwenye michezo mingine, mfano Swimming, Athletics, Archery, etc etc

  fact; List of African football players in Europe - Wikipedia, the free encyclopedia
   
 13. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  MBU,you are spot on,mtanzania kucheza england,will solery depend na hii generation ya kids ambao tayari wako hapa katika various football academies unfortunately by the time the blossom,they could well be no longer tanzanians!!!!!!!!!!!
   
 14. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #14
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cha msingi nafikiri ngasa aandaliwe kisaikolojia ili akafanye vema majaribio yake,kwani huu ndo unaweza ukawa mwanzo wa tanzania kupata wachezaji wengi zaidi wa kulipwa na hivyo kuifanya timu yetu ya taifa kuwa mwiba mkali kwa timu pinzani itakazoutana nazo kwenye mashindano mbalimbali. Big up,Ngasa!!!!!!!!!!!!!
   
 15. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Asante mfumwa kwa kuposti hiyo news hapa lakini najua kikwazo kitakuwa work permit.
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,137
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Akamuulize mohamed mwameja;na hussein masha
  ushauri

  kabla ya kuondoka ajifunze kuchuma machungwa ingawa kule atakutana na matunda itamsaidia kuona kama kazi ya kawaida na si utumwa
   
 17. A

  Audax JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni ile west hama unayoijua mkuu, ila ngasa naye mbona wantaka kumpaisha haraka?
   
 18. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Posted Date:: 2009-03-20 08:22:00 Ngassa set for trials with West Ham By Majuto Omary Young Africans ace Mrisho Ngassa has received an invitation to join English premiership club West Ham United for trials. Ngassa, who has been constantly hunted by European teams, will fly to England early next month for the two-week trials. A letter signed by West Ham United secretary P.R. Barnes says Ngassa is supposed to join the team from April 13. It said the club was ready to incur all expenses for the playerýs stay in England till the end of the trial. "We are ready to pay for his transport, meals and accommodation during his stay in the country. We wish him good luck," said Barnes in the letter. He said they have contacted Bakhressa, the agent recognised by FIFA, to organise the playerýs trip to London. Ngassa would be under the technical bench led by Coach Gianfranco Zola. The bench would assess his stamina, speed and attitude. Young Africans secretary general Lucas Kisasa confirmed the good news, saying they have accepted the request through Bakhressa. Kisasa urged Ngassa to train hard before departing for London in order to meet qualities required. The move would benefit his club, as it is responsible for his transfer, should he pass the trials. "We are happy with the invitation. It is a good opportunity for the player to show his prowess; it is also a golden opportunity for him, Young Africans and his country at large," said Kisasa. This is the second time Ngassa gets a request for trials from European teams. Lov-Ham of Norway was the first team to seek his services. However, the teenager's earlier move hit a snag after the Norwegian club messed up with transfer procedures for not involving his club in the process.
  SOURCE: The Citizen 20th March 2009.
   
 19. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Siku hizi hata hizo jobs za matunda kuzipata ni mbinde, wapolish wamezikamata zote! LOL
   
 20. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Habari hii pia ime-appear kwenye gazeti la Dailynews la leo 20th March 2009 (Refer to the attached document) na bwana Madenga pia kazugumzia habari hii kwenye TCB1 habari.
   

  Attached Files:

Loading...