Kama hii habari ni ya kweli, ninamuombea marehemu apumzike huko anapokwenda,japokuwa mapumziko yake hayatakuwa na amani. Huwezi kulitumbukiza taifa katika hujuma kubwa namna hii halafu ukapumzika kwa amani kuzimu. Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Si bora tu angeita waandishi wa habari akatoboa kila kitu hata kama na yeye alihusika pengine hii ingeweza kuwa fundisho kwa next governors and presidents. Jamani hizi pesa tutaziacha hapahapa duniani. Ni vyema tukawaachia mazingira mazuri walio hai hapa tanzania.
Waandishi wa habari hebu jaribuni kuongea na mke wake mama muganda, huenda anaweza kuwamegea kidogo.
Ndio maana mimi sina imani na benno hata kama ni mtaalamu aliyetukuka katika elimu ya uchumi. Kesho na kesho kutwa atarudia yaleyale ya balali, maana waliokuwa wanashirikiana na balali bado wapo hai na wamekamata sukani. Sasa benno achague kusuka ama kunyoa.