New York: Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Tanzania - Starring Samia Suluhu Hassan, President of The United Republic of Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Niko Standby kuwaletea link ya uzinduzi huu.

====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo ashiriki kwenye uzinduzi wa makala maalumu iitwayo ‘Royal Tour’ jijini New York nchini Marekani.

Makala hayo maalumu ambayo mchakato wake umefanyika kwa takribani mwaka mzima umemshirikisha moja kwa moja Rais Samia akiwa katika vivutio mbalimbali vya utalii nchini Tanzania kwa lengo la kuongeza watalii na kuvutia wawekezaji.

Uzinduzi huo wa aina yake unahudhuriwa na takribani watu 400 unafanyika kwenye Jumba Mashuhuri la Makumbusho liitwalo Guggenheim kuanzia saa moja na nusu za usiku za Marekani, sawa na saa nane na nusu usiku kwa Afrika Mashariki.

Miongoni mwa washiriki ni pamoja na wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, viongozi wa kisiasa, mashirika ya kimataifa, waandishi wa habari na Watanzania waishio Marekani.

Pia wafadhili na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za uhifadhi kama TANAPA, NCAA, TTB, TAWA, TFS na makundi ya wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania wakiwakilishwa na CTI, TBA, TPSF, TATO na CEOrt wahudhuria.

Shughuli hiyo inaoneshwa mubashara kupitia televisheni za Marekani kwenye mfumo wa utangazaji wa umma (PBS) kupitia kituo cha televisheni cha WTTS yenye watazamaji takribani milioni 3.5 na baadaye makala hayo itaoneshwa kwenye zaidi ya chaneli 300 zinazowafikia takribani asilimia 86 ya Wamarekani.

Makala hayo yatazinduliwa pia jijini Los Angeles, Aprili 21, mwaka huu na baada ya matukio hayo mawili, filamu hiyo pia itarushwa kwenye mtandao wa kidijitali wa Amazon na Apple TV.

Kwa Tanzania, filamu hiyo itazinduliwa kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili na baadaye visiwani Zanzibar tarehe 7 Mei.



Taarifa zaidi soma;

Uzinduzi wafanyika New York
Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour umefanyika usiku wa kuamkia leo Aprili 19, 2022 Jijini New York Nchini Marekani na kuhudhuriwa na watu wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Filamu hiyo maalumu ilitengenezwa kwa mwaka mzima ikimshirikisha Rais Samia kama mhusika mkuu akiwa katika vivutio mbalimbali vya utalii #Tanzania kwa lengo la kuongeza watalii na kuvutia wawekezaji.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na zaidi ya watu 400 katika Jumba la Makumbusho la Guggenheim, baadhi ya waliohudhuria ni wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, wanasiasa, mashirika ya kimataifa.

1FDF99D4-1240-4C90-8A5E-56A2329D5644.jpeg
545FED05-36C5-4E92-90F0-CBA0BA8A3472.jpeg
A4272472-38F1-4912-AF00-67941DC01706.jpeg


Paskali
DSM
Tanzania

PIA, SOMA: Ufafanuzi: The Royal Tour, filamu ya Rais Samia inayolenga kukuza utalii
 
Update.
Event hii ya uzinduzi wa filamu ya Royal Tour haiko live.
Kama kuna member wetu yoyote uko ukumbini, please share, na mimi will share the few clips that I have
P
Sijui hii if ya siku hizi imekuwaje?!. Ingekuwa ni ile JF ya enzi zile, saa hizi ungekuta tuna updates zaidi ya members 10!.
Yaani unamaanisha kati ya hao waalikwa zaidi ya 400, hakuna mwana JF yoyote kutu update!.
P
 
Sijui hii if ya siku hizi imekuwaje?!. Ingekuwa ni ile JF ya enzi zile, saa hizi ungekuta tuna updates zaidi ya members 10!.
Yaani unamaanisha kati ya hao waalikwa zaidi ya 400, hakuna mwana JF yoyote kutu update!.
P
Tupo tunasikilizia maumivu,jinsi pesa zetu zilivyoliwa na maza yupo kimya.
So tunaona hata wakiongezeka watalii zitaishia mifukoni mwao na hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya CAG kuja kutusomea tena ngonjera
 
Sijui hii if ya siku hizi imekuwaje?!. Ingekuwa ni ile JF ya enzi zile, saa hizi ungekuta tuna updates zaidi ya members 10!.
Yaani unamaanisha kati ya hao waalikwa zaidi ya 400, hakuna mwana JF yoyote kutu update!.
P
Walengwa wa hiyo filamu ni wazungu, sio sisi members wa jf ambao wengi ni watanzania. Labda kama lengo ni kuturungishia. Hivyo sitegemei sisi watanzania wengi kuvutika na hiyo filamu maana sio walengwa wa filamu hiyo. Naona umehamasika na hilo tukio mpaka unadhani na wengi wetu tumehamasika hivyo hivyo. Ila si vibaya maana ww umehamasika utuletee hizo clips kadhaa tuone huo uhondo unaokupagawisha.
 
Back
Top Bottom