Never underestimate the power of nyumba ndogo

Never underestimate the power of nyumba ndogo

Heeeeheeeee......Aisee Lunch yangu ya leo ni full maraha....wape wape!
hao wanaojiita nyumba ndogo wanajipa matumaini maana
ni mguu ndani mguu nje, kakosa hata
wa kumdanganya nitakuoa,wanajishaua tu,wataishia kutoka vitambi
kwa bia za ofa na chipsi kavu,watupishe sie khaaaa!!
 
mi hata hanisumbui na hizo nyumba ndogo zake bana, kwani mimi ndio sitongozwi?

huyu wa kwangu alinirusha roho sana na hizo nyumba ndogo..mwanaume anarudi usiku saa 8-9

kwa uchungu na upendo nilikuwa hata silali, namuwazia tuuuu mume wangu, nikipiga cm hapokei, hapo chakula nimemuandalia, mwenyewe nimeoga nimejiremba namsubiri arudi wapi..mwishoe unaishia kulala na njaa na hasira juu

nikaona ya nini, na mimi nikawa na kidumu changu, yeye hata arudi asubuhi mi sijali...yale mapresha ya kuhangaika kumtafuta nikawa sina, na chakula nakula mapema nalala wala habari sina..na akirudi wala sikasiriki mana najua na mimi si ninaye? ila mimi sichelewi nyumbani na for years hakujua ila alishangaa tu simjali tena, yaani yale maatention mume kachelewa sijui yuko wapi wala sina..yaani kwa kifupi wivu sina ye aende anakotaka arudi muda anaotaka, mi poa tu..

alivoona sina time naye sasa ndo akaanza kutafuta why? bado hajui ila ana wasi wasi na mawivu kibao simu yangu ikiita tu keshaishika..mara anakuja ofcn bila taarifa ilimradi tu aone km niko kweli ofcn, na huko kuchelewa usiku keshaacha long time anawahi home kuliko hata mimi, sijui ndio keshatemwa na uyo nyumba ndogo au vp! au ndo kajionea bora ya mama fulani!!!!! sijui, wala sijamuuliza... haya sasa nasema nyumba ndogo imeishia wapi siku hizi? kawa mpole kama kamwagiwa maji, na hiyo nyumba ndogo yenyewe inamtukana kama mtt mdg, yani ukiona hizo msg anazotumiwa utamuonea huruma..na ndio kamzalisha na mtoto basi ndio anakomaje? mie namwangalia tu, namwambia nenda mkalee mtoto unaitwa, hajibu kimyaaaaaaaa kama kamwagiwa maji vile..kuna siku kaniambia eti mi nataka kumtelekeza huyo mtt nifanye nini? nikamwambia usinihusishe kwenye zambi zako kwani wakat una..........huyo mama yake ulinambia? basi kimya anabaki kama kamwagiwa maji ya baridi vile...
na hio nyumba ndogo yake ikipiga simu nampa namwambia pokea, wakati mwingine hapokei itapigwa weeeeeeeee mpaka namlazimisha ndio anapokea basi utasikia wanavojibizana na mitusi kibao!!!! heheeee, najisemea moyoni..uliyataka mwenyewe sasa utajibeba!!! wewe si uliona nyumba ndogo ya maana ngoja ikuonyeshe kazi sasa...na hiyo nyumba ndogo inamuaibisha hadi kazini, anakomaje????... na sasa alivo hana akili akawa na nyumba ndogo isiyo na kazi halafu ikazaa, yaani ni vurugu kwa kwend ambele.........ndio sasa eti karudisha majeshi kwa mama naniii mpooooole mwenyewe, hata umseme vipi anajiinamia tu...anaona aibu tuu

na moyoni najisemea mi nilikuwa sijui kucheat, amenifundisha yeye..(in fact alinikuta virgin)..na nilikuwa sijui mwanaume zaidi yake...lakini hizo nyumba ndogo zake zimenitia akili, nami nikajua maaana halisi ya kidumu...

kwa iyo msifikir nyumba ndogo ni soulution...ingekuwa ni solution basi huyu wa kwangu angekuwa na furaha tele na amani kibao lkn kwa sasa ndio kazidiwa na mawazo lukuki na ananishitakia mimi nimsaidie jinsi ya kuhandle hilo li nyumba ndogo lake waliloshindwana....kila siku anajutaga tuuu, na mi nasema bado.......mfyuuuuuuuuu

Kwanini msikae mkaongea kama watu wazima? Mtakomoana mpaka lini?
 
Miss neddy nimekupenda ghafla..ulosema yote yana ukweli.Wanawake hawabweteki wana majukumu mengi ya kifamilia zaidi ya kupet hao wanaume.Nyumba ndogo anapewa kila hitaji lakini mke hujihangaikia mwenyewe kukamilisha mahitaji yake na wakati mwingine ya kifamilia.Hivo huwezi kuwafananisha machangudoa (nyumba ndogo) na mke.

like, like, like... wanawake siku hizi tunabeba majukuma ya wanaume pia, tunahangaika kutafuta shilingi kwa ajili ya kusaidia kulipa fees, ujenzi n.k. lakini wao, za kwao wanataka kupeleka nyumba ndogo
hao nyumba ndogo zao toka asbh hawana shughuli ya maana zaidi ya kukaa na kuwasubiri mabuzi.
mkiweza kuweni nazo hata 5 hizo small house ila nikifahamu, ujue na mimi ndio umenikosa
 
sio tu kupunguza stress inaleta heshima pia!!!! yani asifikiri yeye tu ndo anajua kutongoza, ajue kabisa na mimi huwa ninatongozwa vile vile!!!!!!!

unajua wanume wakishaona umezaa watoto 2-3 wanaona umezeeka, huna soko..basi atakurusha roho na hivo vihawara vyake weee, siku akijua kuwa wife anaweza kucheat/ kacheat ndio akili inamrudia kuwa naweza mpoteza wife hivi hivi


wanaume wakijua unatongozwa, au unaweza kucheat huwa wanachanganyikiwa. yani akiona unacheat au hata akihisi tu, anachanganyikiwaje!!! na ukiamua kucheat, unatakiwa kutoka na yule anayemzidi yeye kwa kila kitu
 
We jiachie achie uone kama hayatakutokea.

good girls ndo wanaokuwa cheated on,you do EVERYTHING FOR HIM he takes it for granted...ya kazi gani
If he cheats i cheat,or rather ntamuwahi,
 
like, like, like... wanawake siku hizi tunabeba majukuma ya wanaume pia, tunahangaika kutafuta shilingi kwa ajili ya kusaidia kulipa fees, ujenzi n.k. lakini wao, za kwao wanataka kupeleka nyumba ndogo
hao nyumba ndogo zao toka asbh hawana shughuli ya maana zaidi ya kukaa na kuwasubiri mabuzi.
mkiweza kuweni nazo hata 5 hizo small house ila nikifahamu, ujue na mimi ndio umenikosa

Laana yeyote impatayo mwanaume mwanamke no mshirika haikuachi kwa kuwa ulitoka kwa mwanamme direct hayo ni majumu yako na. mumeo wote pamoja nyosha kauli yako according to bible.
 
nitajituma mke wangu awe house wife nione kama na yeye atajituma kujipamba, kupamba familia na kuwajibika iasavyo uwanjani. ee Mungu nisaidie.simu yangu inagoma kutoa like, ila Nampongeza sana mtoa mada kwa kuweka hii kitu mezani. kwa kweli ndoa nyingi zipo hobela hobela kutokana na huu ukweli.hili la wanawake kufanya kazi na kuchoka limekuwa kisingizio kikubwa cha ma mazahouse. ndio maana naomba mungu abariki mahangaiko yangu, ili nitimize azma yangu hapo juu. wanawake jitumeni ili kujenga familia zenye furaha. hakuna utajiri mkubwa kama happy family.
 
nitajituma mke wangu awe house wife nione kama na yeye atajituma kujipamba, kupamba familia na kuwajibika iasavyo uwanjani. ee Mungu nisaidie.simu yangu inagoma kutoa like, ila Nampongeza sana mtoa mada kwa kuweka hii kitu mezani. kwa kweli ndoa nyingi zipo hobela hobela kutokana na huu ukweli.hili la wanawake kufanya kazi na kuchoka limekuwa kisingizio kikubwa cha ma mazahouse. ndio maana naomba mungu abariki mahangaiko yangu, ili nitimize azma yangu hapo juu. wanawake jitumeni ili kujenga familia zenye furaha. hakuna utajiri mkubwa kama happy family.

Siyo kisingizio ni ukweli usiopingika! Wanaume wazembe wameshindwa majukumu yao inabidi wanawake waingilie kati kuyafanya halafu warudi nyumbani wamechoka, then waanze na shughuli za mwanamke nyumbani na kumalizia za mume wake! Mnadhani hawa ni robot? Haiwezekani! Men you should take all your responsibilities! to make your wives do theirs as well! Wanafanya mara 2 ya wanaume, it's not fair!
 
Na wewe mwanaume kwenda kwa nyumba ndogo ndivyo unavyompa nafasi mke wako naye kufanywa nyumba ndogo na mwanaume mwingine,ngoma draw usije kulalamika,....mapenzi is two way traffic acheni kulalamika,play your part well......

Well said!
 
kwa hiyo na nyie mkishndwa kutimiza mahtaj yetu tutafute vdumu??? sometimes mume humtoshelez mkeo kwa bed lkn anavmilia.......... unaishiwa huna hela dada wawatu anashndia uj wa sembe lkn anavumilia..... bidada mshahara wake unaishia kulea familia hata kujifanyia shoping anashndwa na vitabu vya dn vimeandka mwanamke atazaa kwa shida na mwanaume atakula kwa jasho. bt stil bidada anazaa kwa shida na kula kwa tabu lkn anavumilia......... sasa nyie mnashindwa nini kutuvumilia???! co cr mwanamke akizaa majukumu yanaongezeka so tuvimiliane jaman coz hata nyumba ndogo unayoiona tamu ikizaa itakua chungu sasa utamaliza nyumba ndogo ngap??! RUBIS!!!!!!!!

Well said kula Like babe gal!
 
nikisema hizi ndoa stress tupu mtabisha...
 
cha muhimu
kwa wanandoa ni kwa kila mmoja kutambua na kutimiza majukumu yake...easier said than done? Yes! But marriage is a lot of work....not a walk in the park. Otherwise there is no excuse to cheat...kuna hasara nyingi za kujaribu kutatua tatizo kwa kuongeza matatizo mengine....nyumba ndogo na serengeti ni matatizo!
 
Laana yeyote impatayo mwanaume mwanamke no mshirika haikuachi kwa kuwa ulitoka kwa mwanamme direct hayo ni majumu yako na. mumeo wote pamoja nyosha kauli yako according to bible.

mmh! kuna watu wamejihalalishia hizo small house, ya nini kusubiri mpaka uletewe maradhi. kama kitu hukipendi na hukikubali inatakiwa mwenzio ajue kwamba hukikubali, ili ajiandae kwa yatakayojili baadae kama akiamua kuwa na hiyo small house
 
Back
Top Bottom