Netflix documentary ya The Backhams ina funzo kubwa sana ya ndoa za kisasa zinapaswa ziweje.. modern life ndoa inapaswa muendane sana

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau

Muda si mrefu nilikuwa natazama documentary ya familia ya beckham Netfilx inayokimbiza sana huko netflix nikajifunza vitu kuhusu ndoa za kisasa

1. Wanandoa mnapaswa mfanane.. yaani mwanamke awe female version ya huyo mwanaume and vice versa. Hii namaanisha mwenza anapaswa awe na purpose ambayo kama angezaliwa jinsia nyingine angefanya vitu kama mwenza wake.

Beckham na victoria life purpose zao zimewafanya wadumu na wawe na ndoa tamu sana.. ndio maana netflix wamewalipa mabilioni. Na kutengeneza documentary ya ndoa yao.

2. Ndoa nzuri ni ile inayofungwa wanandoa mkiwa na bado wadogoo. Safari ya ukuaji wenu iwakute kwenye ndoa. Ndoa inapaswa ifungwe ujanani sio kwenye utu uzima.. beckham na victoria walifunga ndoa wakiwa 23s... phase zote zilizofata za maisha wamepitia pamoja kama wanandoa.

3. Ndoa haipaswi kuwa na long distance relationship. Wanandoa mnapaswa muishi nyumba moja siku zote. Isipokuwa dharura za safari za muda mfupi

4. Ndoa ni watoto. Watoto wanaunganisha sana wanandoa.. na ni vizuri hao watoto wakazaliwa mapema.. ili wakuwe na nyinyi wazazi.. early 30s. Iwakute mmeshamaliza kuzaa watoto wote mbaki kupambana na malezi tu. Pia mwanamke akiwa 20s uzazi unakuwa mwepesi sana.. mimba anabeba kwa urahisi na kuzaa anazaa kwa wepesi. Kuchelewa kuzaa sio sahihi.

5. Pesa ifate pesa. Wanandoa pande zote wawe wanatoia familia zinazofanana maisha.. na pia kwenye harakati za utafutaji mfanane fanane.. beckham akiwa superstar mancherster utd late 90s.. alifunga ndoa na victoria beckham na yeye akiwa muimbaji aliyefanikiwa kwenye kundi la spice girls...kila mtu alikuwa na pesa zake na maisha yake yaliyonyooka hakuna kusema mtu mmoja anamnyonya mwenzake..

Kwa wenye account netflix na wanaopenda documentary ni vizuri tukaitazama hiyo documentary netflix.

Nimejifunza Ndoa inapaswa iwe furaha.. sio vita

Nimeweka na video ya kina beckham ya mwaka 2023 wakiwa wanacheza wimbo ule ule walioucheza siku ya harusi yao mwaka 1999.. miaka 25 iliyopita

 
Ulaya/America wanandoa wapi committed na ndoa zao wakati Africa ndoa n ndoano.
 
Waafrica mapenzi sio fani yetu, kwanza hautosikia kwenye ndoa nyingi za waafrica nimemuoa Rafiki yangu WA utotoni, mapenzi tunayavamia ukubwani na hatuanzii chini Kwa sababu ya umaskini na tofauti ya vipato,

hatufundishwi upendo tangu tukiwa watoto,uwa nawashangaa sana watalii aswa wazungu wakija Africa uwa baadhi ni couple zimeongozana tofauti na waafrica
 
Hiyo no 2 ni bonge moja la point.... binafsi ndo kitu imefanya na inaendelea kufanya nifurahie commitment yangu
 
Kwahiyo Kwa mujibu wa bandiko lako, vijana ambao hawajaoa na kuolewa wafate utaratibu huu wa Beckham na mkewe?
 
Back
Top Bottom