@malcomlumumba
tatizo maandiko yamekuwa overated mno,
"nitakufanya uwe taifa kubwa"
israel haipata kuwa taifa kubwa,
mataifa makubwa ya zama zile yanafahamika,egypt,asyria,aram,babel,alexandra the great,ottoman empire etc.
Hivi ni lini israel imewahi kuwa taifakubwa?
Inawezekana kabisa mkuu,
Lakini hebu tuangalie hili suala katika mapana kidogo.
Ukubwa wa taifa unaangalia mambo mengi sanaaaaa.
Ardhi,Rasilimali,Idadi ya watu, nguvu ya kijeshi, nguvu ya kiuchumi na ushawishi wake katika jamii inayowazunguka.
Leo hii tukizungumzia ukubwa wa kijeographia wa taifa na Idadi ya watu,
Basi nadhani nchi Kama Brazil, Uchina na India ndiyo yanaweza kuwa mataifa makubwa duniani.
Tukiangalia kwenye suala la rasilimali basi tunaweza kusema mataifa ya Afrika ndiyo makubwa sana duniani.
Lakini tukiangalia kwa mtazamo wa uhalisia,
Vitu kama rasilimali, idadi ya watu na eneo kubwa la ardhi havilifanyi taifa kuwa kubwa.
Bali hivi vinaweza kuwa viashiria kwamba taifa hili lina nguvu au linaweza kuwa na nguvu huko mbeleni.
Hii kwenye lugha ya Malkia tunasema "A nation has a potential to be great and powerful in the future"
Nikupe mifano mizuri tu:
Afrika tuna "Potential" ya kuwa Bara lenye nguvu sana kwasababu tuna kila kitu lakini sisi siyo Taifa kubwa.
Katika historia ya dunia hii, falme iliyowahi kuwa kubwa sana ni ile ya Mongolia chini ya Chengis Khan na Qublai Khan.
Ilikuwa inamiliki kama asilimia 16% ya ardhi ya dunia kama nakumbuka vizuri lakini ufalme ule haukuwahi kuwa na nguvu zaidi ya kutumia majeshi na kumwaga damu tu. Mfumo wa siasa ulikuwa mbovu, Uchumi mbovu na elimu mbovu, wakashindwa kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano baina yao wenyewe na hivyo taifa likaanguka lenyewe tu.
Halafu tuangalie upande wa pili wa shilingi,
Mataifa ya Ugiriki yalikuwa ni madogo sana kieneo.
Ukiangalia taifa kama Athene, Sparta, Thebes, Corinth yalikuwa madogo lakini yalikuwa ni mataifa yenye nguvu sana.
Ushawishi wa Athene uliweza kusambaa Ulaya yote hadi kutishia mustakabali wa taifa lenye nguvu kijeshi kama Sparta.
Tena ukiangalia katika historia,
Ufalme wa Umedi na Uajemi (Persian/ Achemenid Empire) wakati unatawala dunia ulikuwa na watu millioni 45,
Sawa na idadi ya Watanzania kwa Sensa ya miaka kama 4 au 5 hivi iliyopita, lakini walikuwa wanaogopa sana nguvu ya vitaifa hivyo vidogo vya Ugiriki. Hii ni kwasababu vilikuwa vina ushawishi mkubwa Kidini, Kisiasa, Kiuchumi na Kielimu.
Wakati Mfalme Dario na Mtoto wake Xerxes wamevamia Ugiriki kwenye The Battle of Marathon walipigwa sana na Athens,
Wakaja kurudia tena wakatwangwa kwenye The Battle of Salamis na hivyo wakaamua kuwaacha Wagiriki na maisha yao.
Kifupi hawakufanikiwa kabisa kuwatawala Wagiriki hadi wagiriki walivyounga chini ya Alexander na kuwasambaratisha waajemi na ufalme wao.
Sasa basi,
Hadi kama hadi leo hii tunawasoma Wagiriki wa miaka zaidi ya 4000 iliyopita utasemaje haya ni mataifa madogo ???
Mifumo yetu ya Kidemokrasia ndiyo ile ile ya Waathene wa Ugiriki ya zamani: Mawazo yutu ni yale yale ya Plato, Aristotle au Socrates. Warumi katika Jeuri yao yote walikuwa wanatumia falsafa za Wagiriki kutawala dola lao ambalo lilikuwa kubwa sana hapa duniani.
NB 1: Leo hii Falme za Uingereza ni ndogo sanaa,
Zinaweza zikaingia mara hata 50 kwenye nchi ya Tanzania (Kieneo)
Lakini lile ni taifa kubwa sana na lenye nguvu kubwa mno kiushawishi hapa duniani.
Kuanzia mifumo yao ya kielimu (Cambridge System), mifumo yao ya Kisheria (The Common Law) na Mifumo yao ya Kisiasa (Parliamentary Democracy): Dunia nzima tuna vitu vizuri vya KUJIFUNZA KUTOKA KWAO na huu ndiyo ukweli usiopingika.
Hata Marekani katika Jehuri yake yoteee,
Amechukua vitu vingi sana kutoka kwa Waingereza,
Pia ushawishi wa Muingereza ndiyo ulifanya taifa la Marekani liwepo tokea kwenye Mkataba wa Paris wa mwaka 1782.
NB 2: Upande mwingine wa hilii ni huu.
Mataifa makubwa huwa hayalingani kabisaa.
Kila taifa linakuwa na nguvu yake ye kipekee ambalo taifa jingine halina.
Na ukishindwa kuheshimu hili basi ndiyo utaishia kuamini kwamba mataifa ya Afrika ya zamani kama Ufalme wa Congo, Ufalme wa Mwenemutapa, Ufalme wa Meroe, Ufalme wa Zanzibar walikuwa hawana chochote hapa duniani.
Siyo kweli hata kidogo,
Kwasababu taifa linakuwa na nguvu sana pale tu linapowafanya watu wake waendelee,
Ukiangalia maisha ya watu wa Athens, Rumi, Uturuki, Uajemi, Qing, Mali au Uingereza utakubali ninachokisema hapa.
Nchi ikiweza kujenga mifumo imara ya kisiasa na watu wakafaidika nayo basi ni lazima nchi hiyo itakuwa na ushawishi tu.
Sasa kule Mongolia,
Kulikuwa na mauji makubwa, Ubakaji, Vurug kila siku.
Watu watapataje kuendelea wakati vimejaa vifo, vita na magonjwa kisa tamaa za mtu moja tu ??
Japo lilikuwa dola lenye uwezo "Potential" wa kutawala dunia kwa miaka zaidi ya 400 hivi.
Lakini walishindwa vibayaaaaa.
NB 3: Sasa ukubwa wa mataifa ya Mashariki ya kati yaangalie katika minajili ya ushawishi wao.
Leo hii hapa duniani dini kubwa na zenye ushawishi usio mithiriki na Ukristo na Uislamu.
Bahati mbaya sanaa hizi dini zilianzishwa na Wayahudi na Waarabu.
Historia za hizi dini ndizo zimeigawanya dunia kwa miaka mingi sana hata kabla ya kizazi hiki.
Dini hizi zimefanikiwa kuathiri hata uwezo wetu wa kufikiri na hata mitazamo ya kidunia (Huu ni ukweli mchungu)
Leo hii hata huu uzi wengi wetu tunaungalia kwa minajili ya kidini tu.
Hivyo utasemaje kwamba hawa watu hawakuwahi kuwa taifa kubwa ???
Israeli chini ya Suleimani, Uzziah na Ahabu liliwahi kuwa taifa lenye nguvu sana sema kwa muda mfupi.
NB 4: Kwenye Ukweli tukubali na kwenye Uongo tukaetae kabisa.