Neno " lol " lina maana gani?

Ndio maana mimi huwa silitumii.

ukijizoesha sana kufatilia mitizamo (opinions/veiws) za watu wa conspiracy theory au walokole,utaambiwa hata hiyo "boxer",bikini panty,tshirt,condom uliyovaa ni ya ki-iluminat.na mwishowe utaona bora kutembea uchi kuliko kuvaa nguo za mashetani.siku za awali nilikuwa na mtizamo hasi kama wewe,kila jambo nilihusisha na u-freemason/ushetani.matokeo yake akili ikawa dormant and unable to analyse things in a normal approach as they are..baada ya kujielewa nikaanza kupotezea baadhi ya mitazamo ya kijinga.vitu vingine ni trend na siyo vya kuhoji sana.
 
Wadau ... Tusaidiane hapa .. Neno "lol" 1. Lina maaana gani ? 2. Hutumika mazingira gani ? 3. Jinsia ipi hupaswa kutumia neno hilo.? Na akilitamka kwa jinsia ipi ? Asanteni .
Hili neno linatumiwa sana na jinsia ya kike. Ukikuta mwanaume analitumia lazima huyo atakuwa MLIBERALI.
 
Kama wadau wengine walivyotafsiri "Loughing out loud" lakini ni neon la kizunguzungu zaidi haliendani na mazingira na muktadha wetu waswahili sema watu wengi wameingia kwenye kitu naweza kuita "Mkumbo" yaani kama fasheni kulitumia. Binafsi naona limekaa ki-kikekike zaidi!!

Sana,liko kike kike zaidi. Mwanaume kuandika lol huwa nakua na mashaka nae,au mwanaume kuandka "haya wangu" au "sawa wangu" au "nambie wangu" huwa nakua na mashaka nao.
 
kwanini..???lakini sikatai kwa mawazo yako inaweza kuwa sahihi,nisawa navyoona mimi maneno ya kiswahili kama "majanga","utajiju","sielewi","aje aje"...nikati ya vimisemo ambavyo naona havifaikusemwa na mwanaume

Au nimekumisijee!! Nimeipendajee!! Zipo kike kike
 
Afadhali we umekuja kuuliza sasa kuna wale wenzangu na mie kina sipitwi. Kitu hakielewi ili aonekane wa kishua anacoment Looooooool yaani huwa nacheka ili mradi aonekane yumo. Ndo maana mnaagizaga Watsapp za baridi.LMAO
 
Nachukiaga ukute dume zima eti linasema "umependezaje" au "chezea mimi wewe" hii ni misemo ya kina dada haifai kuongelewa na wanaume.

minaona watu wengi wanakosea.wanadhani 'lol' inawakilisha mshangao. anajibu 'lol' akishangazwa na sio kufurahshwa.
utakuta dume anasema 'pendeza sana' .!!
inaboa!
lakn dominick nyalifa anasema 'chezeiyaaar....' inakua naswaga ya kivyake kdg.mi ile nimeikubali.
 
Sana,liko kike kike zaidi. Mwanaume kuandika lol huwa nakua na mashaka nae,au mwanaume kuandka "haya wangu" au "sawa wangu" au "nambie wangu" huwa nakua na mashaka nao.

Hata mimi lazima niwe na mashaka nae. Kuna vimaneno fulani yaani ukishaona wakina dada kama wametawala kuvitumia inakuwa sio poa mwanaume kuvitumia.
 
Afadhali we umekuja kuuliza sasa kuna wale wenzangu na mie kina sipitwi. Kitu hakielewi ili aonekane wa kishua anacoment Looooooool yaani huwa nacheka ili mradi aonekane yumo. Ndo maana mnaagizaga Watsapp za baridi.LMAO

Hata mimi huwa nashangaa wana maana gani! ingekuwa looo! ya mshangao ningeelewa lakini hiyo nyingine ni balaa!
 
Afadhali we umekuja kuuliza sasa kuna wale wenzangu na mie kina sipitwi. Kitu hakielewi ili aonekane wa kishua anacoment Looooooool yaani huwa nacheka ili mradi aonekane yumo. Ndo maana mnaagizaga Watsapp za baridi.LMAO

Hata mimi huwa nashangaa wana maana gani! ingekuwa looo! ya mshangao ningeelewa lakini hiyo nyingine ni kituko!
 
Mie nisaidieni LMAO

LMAO... Lough My Ass Off
SMH... Shake My Head (Inasikitisha)
OMG... Oh My God (Mungu wangu!)
LOL!... Lough Out Loud (Inafurahisha, unachekesha...)
TGIF... Thank God It's Friday (Yaani ni siku ambayo utalala muda mrefu kwakuwa siku inayofuata unapumzika)
PYA...Protect Your Ass (Yaani kuwa makini na ufanyalo)
 
Kinachonishangaza ni kwamba hapa JF tumejaa watu ambao tunajivunia lugha ya kiswahili kama lugha yetu ya taifa, lakini mata eti 'lol' ina maana sijui nini mara btw ina maana sijui baa ya tukunyema ina watoto mara sijui nini na nini.
Kwa nini tusiunde vifupi vyetu vya kiswahili? Kwa mfano: tuna neno 'kama kawa' = kama kawaida. Tuendeleze vifupi vingine vya kiswahili.
1.kuw = kwa ufahamu wako
2.nnt = nilikuwa natania tu
3.akk = asante kwa kunijulisha
4.us = umenichekesha sana
5. nk nk. Unda kifupi kizuri kitamu cha kiswahili tutakipenda tu.
Hayo ma btw, lmfao, lol, tuwaachie wenyewe!

..............acha siasa LMAO !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom