Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

falsafa yenye walakini... yeye kachagua mti mmoja, aliotaka kuuona na akaamua kwingine kuna msitu, aliotaka yeye uwe!!!

in history we all have shrubs, bushes, forests and trees... no tall nor short trees...

The question here is what defines a tree?
 
Makubwa haya mimi ningemuomba Maggid atuletee kipande cha hotuba ya Mandela aliposema hivyo!.. maanake haiingii akilini kabisa. I can bet Mandela hakuwahi kusema hivyo....

FMES, Hata kama mtu mmoja hawezi kuongoza kwani mti mrefu ndio huongoza msitu? Au maana yake nzuri ingekuwa kwamba Dr.Slaa pekee si msitu ni miongozi mwa wananchi (msitu) hivyo kumwonda yeye haina maana umeuvunja msitu...
 
Thanks mkuu...

Tatizo letu kubwa ni kudhani tunafanya uchambuzi, kumbe tunajaribu kutohoa tu!!
 

Kitu kimoja unasahau,

Kutokana na nguvu zilizokuwa zimemzunguka John Garang matokeo yake ni kuwa mara baada ya kufariki kwake na vision yake ya Sudan moja yenye usawa ikatupwa. Wakaibuka kina Salva Kiir na wenzake with ile hidden intention ambayo ni succession by any means...Nadhani kilichoendelea wakati na baada ya uchaguzi wao mwezi July unakijua....Kinachofuatia baada ya referendum dalili hazifichi......

This tells a lot about political organisations zenye kujinasibu na ajenda ya UKOMBOZI. Always with hidden agenda ambayo wenye nayo huwa tayari kujificha nyuma ya kinara wa "UKOMBOZI", huwa zinaibuka wazi mara baada ya kinara kuondoka ama kuondolewa na mara nyingi huwa na remifications zake ambazo huathiri wale ambao walipaswa kukombolewa. No wonder u see people like Museveni hawako tayari kuondoka ama kuondolewa kwani wanajua hayo ya hidden ajenda.

Inapokuja na "ukombozi" wa Tanzania, na kwa kuangalia propaganda zinazoendeshwa kumzunguka KINARA Slaa pekee ni kuwa wenye kuendesha UKOMBOZI huo wanajua kuwa ukifunua zaidi ya Dr Slaa na ajenda ya ukombozi utakuta mengi yasiyo na sura za kuvuti kwa wale wanaopaswa kukombolewa....

Here is the scenario: "UKOMBOZI" unafanikiwa, Chochote kinatokea kwa Rais Slaa, Makamo wake hakuna anayetakiwa kumjua hadi sasa zaidi ya jina lake na kuwa anatoka Zanzibar (we all know kuwa kama sio hitaji la katiba wala asingekuwepo)........So the real power will remain with who..........FREEMAN MBOWE, Chairman and Prime Minister (The guy learned a lot from Lowassa)....utamalizia mwenyewe kitakachofuata.......

Just like in Zanzibar with Maalim as Pragmatic and bridge builder...but u know who will fill his position if anything happen???? Will the reconciliation agenda have chance to survive or IT WILL BE OUR TURN TO SUPPRESS and EAT ENOUGH?? Well, atleast CUF have more developed institutions and party discipline.
 

Omarilyas,

..sasa hiyo ni worst case scenario, tueleze basi na best case ikoje.

..ikiwezekana tueleze na 50-50 case scenario ikoje.

NB:

..second in charge wa Chadema anaweza kuwa rafiki yako Zitto Kabwe. why not??
 
Post kama hizi na hii ya Mjengwa huhitaji hata kupoteza muda wako kuwaelewesha .... inatakiwa tu tuandike rubbish...
 

Hata Maggid alitaka kwenda huko huko sema anazunguka mbuyu na kwasababu wengi hawapendi kuziangalia hoja zake kiundani kutokana na ile dhana kuwa ni mnafiki.

Kimsingi hata yeye ametoa mifano ya viongozi kufa....Akitaka tujiulize what ifs'...Kwamba eti Slaa atakufa na Mbowe kuwa Rais?Ama unamaanisha kuwa huyo atakayerithi kiti cha urais ndiye atakayekuwa kibaraka wa Mbowe?Ofcourse hapo mwananchi mwenye akili atakuwa ametambua kuwa kumbe ni kweli Slaa si mtu wa kuburuzwa,na kwasababu mwananchi hachagui rais "eti kwasababu hatauwawa ama atauwawa"then mfano na hisia zenu zimekula kwenu!

Hivi kweli Omarilyas mnamaanisha kwamba ni kweli Dr Slaa atakufa hadi hilo liwe msingi wa kumchagua rais ajaye?Kwahiyo ndugu Omarilyas AKA Tanzania Njema utamweleza mwananchi kuwa asimpigie Dr Slaa kura kwasababu atakufa halafu Mbowe atakuwa rais?
Ama kweli mkiishiwa na hoja mwaanza viroja!
Kwangu mimi this is nothing but uchuro at its best.
 
maggid, ahsante kwa mchango wako...ni kama kwenye mpira, huwezi kushinda ukitegemea mchezaji mmoja/wachache hodari..kushinda you need team work !
 
maggid, ahsante kwa mchango wako...ni kama kwenye mpira, huwezi kushinda ukitegemea mchezaji mmoja/wachache hodari..kushinda you need team work !
Maggid hazungumzii scenario ya "kupata ushindi",anazungumzia "baada ya ushindi" (soma kwa makini)...Kwamba Slaa atakufa halafu Mbowe ndiyo atakuwa kiongozi/mwenye nguvu/maamuzi.
 

- Bob Heshima yako kaka, mimi nimejaribu kuielewa hoja ya Majjid kuhusu mti mrefu, hayo mengine siyajui sijaenda that far maana ninaamini bila kuungana Wapinzani na kuwa kitu kimoja kwa sababu nia yao ni moja kama sikosei, basi itakwua ni kupoteza muda na pesa nyingi za kuimarisha vyama, kwa maoni yangu!

Es!
 
ina maana wakina maprof woote ndani ya Chadema hawawezi kuunda serikali wakina Lissu, Baregu, Mdee, two Nyerere's Leticia+Vicent, Marando, Arfi, Komu, Mogendi, Zitto, Mwikabe Mwita Waitara na wengineo weengii? acha utani wewe hizo njaa zako Majid zitakufikisha pabaya! we kijana mkuu! ustaarabu muhimu hebu niambie Nyerere alipochukua nchi hii alikuwa na wasomi wangapi? Heshima mbele Mkuu
 

FMES,

..uliyoyasema ni kweli.

..watu kama Majjid hawakupaswa kuwajenga hofu wananchi.

..hapa Tanzania we have a chance to do what has been done in Kenya and Zimbabwe without shedding blood. we have an opportunity to form a government of national unity.

..hali inaelekea kwamba CCM watakuwa na majority bungeni, lakini CUF au Chadema have a shot at the Presidency.

..kwa misingi hiyo Raisi atakayetoka CUF au Chadema atalazimika kufanya kazi na wana CCM wasafi ktk serikali atakayounda.

..hiyo pia itakuwa fursa nzuri sana ya vyama vya siasa, haswa CCM, kujisaili na kujisahihisha.
 

Mh Joka Kuu,unamaanisha Lipumba ana nafasi sawa na Dr Slaa when it comes to chances of winning presidential elections?Unaweza kutuwekea vigezo ulivyovitumia?Tafadhali mtuwekee data hapa kuhusiana na kampeni za urais coz sijaona wala sisikii lolote kuhusu Lipumba ambaye unadai both him and Slaa have a shot at the presidency?Ni vyema basi kama Lipumba na yeye anafanya vyema kwenye kampeni,basi mtuwekee taarifa ili tuweze kujadili fairly badala ya kuwa bias....Ili tuweze kusema wana nafasi sawa,ni vyema tukawa na vigezo madhubuti.
 

- Thanks bro!, point noted!


Es
 
FMES,
Hata mimi nimeelewa hivyo toka mwanzo lakini hainingii akili mtu mzima kufikiria kwamba Chadema (msitu) ni Dr.Slaa ambaye tumekuja mchagua hivi majuzi tu kwa riidhaa ya wanaChadema. Dr.Slaa ni mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya Chadema hivyo sielewi huo msitu unaozungumziwa ni Chadema au Tanzania.

Pili, Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema, kweli yawezekana ana matatizo yake lakini la muhimu ni kutazama katiba ya nchi inasema nini sio katiba au mpangilio wa Chadema. Sasa kama Katiba inasema kwamba rais akifa kesho basi anayeshika madaraka ni Mwenyekiti wa Chadema hapo tunaweza kujadili hata kama Mbowe atakuwa Waziri mkuu.
Ifahamike tu kwamba Chadema kama chama kitafuata katiba ya nchi hadi hapo watakapo badilisha Katiba hiyo na kutenganisha Mawaziri na Wabunge na bado Mbowe ni mbunge, hivyo wasiwasi iko wapi.

Na pengine fikra hizi zinakuja kutokana na wengi kufikiria kwamba CCM umeweza kusimamisha miti mingi kina Dr.Shein ambao hatukuwafahamu before wameshika madaraka, iweje leo tufikirie Chadema na Dr.Slaa lakini wazito sana kufikiria CCM na JK. Mathlan JK akiondoka leo nani atakuwa rais?..Kwa fikra na jicho hilo hilo tunamkuta ni Lowassa..Haya CUF je akiondoka Lipumba nani atakuwa rais? Seif Sharrif Hamad maanake ndio wanaoviendesha vyama.

Sasa iweje tu watu mnaitazama Chadema hali kila chama kina mtu anayewapeleka watu puta? Ndiyo yawezekana Mbowe hana maamuzi yanayopendwa na wengi lakini chama chochote kinatakiwa kiongozi mwenye msimamo na pengine jeuri ili kuweka displine kwani kila mtu anayekuja ndani ya chama huwa na mawazo yake. Na rahisi sana kukivuruga chama hasa ikiwa wapo baadhi wenye ambition..

Halafu jamani huyu Mbowe na ukorofi wake kaweza kuachia kugombea kiti cha Urais, jambo ambalo nina hakika hakuna kiongozi yeyote Tanzania angeweza kufanya hivyo.. hakuna, hata JK mwenyewe asingeweza. tatizo kubwa ni wapambe wa Mbowe hili nina hakika nalo sana hawa jamaa wanatafuta sana sifa na kukibomoa chama kwa maslahi ya vitu fulani fulani... sina haja ya kuendelea huko.

Hivyo haiwezekani kabisa mti mmoja kuwa msitu wala msitu sii idadi ya miti inayofanana unless miti hiyo ni pandikizi...Na hata siku moja binadamu hawawezi kufananishwa na mti au msitu ndio maana nikasema mandela hawezi kusema ujinga huo..
 

maggid umejisahau ama kuna ujumbe unawapa ccm
juu ya uhusika wa salma na riz1?
 
Wengi hatutaki kuujadili ukweli. Kiuhalisia si CHADEMA pekee hata vyama vingine vya upinzani pia havina organization ya kueleweka. Kuanzia uendeshaji wake ni wenye kutia mashaka ya hali ya juu. Ipo mifani kadhaa ambayo inaongeza wasiwasi.
1. Wkt wa harakati za kutafuta mgombea wa Urais, CHADEMA walimpitisha mgombea wao na kuwakilisha jina NEC hata kabla ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu. (Hii ndio dhana ya rubber stamp).
2. Mgombea wa Urais alimtaja M/Kiti wa CHADEMA wa Iringa kuwa alijitoa baada ya kupewa rushwa. Hapa pamoja na kumtaja tulitarajia kuona CHAMA kinachukua hatua na kumfikisha mahakamani maana yaelekea ushahidi wanao.
3. Mkutano Mkuu uliofanyika hivi karibuni ulionyesha ni namna gani CHADEMA inataka nani aendelee kuongoza.
Haya na mengineyo hayana tofauti na CUF.
Kiuhalisia CHAMA kinahitaji muundo imara na DEMOKRASIA inayoonekana na si kusemakana. CHAMA kinahitaji muundo ambao ni imara na uliona uwakilishi wa sehem kubwa ya nchi. CHAMA kinachoweza kutambuliwa km CHAMA na si km mtu na ambacho kwa namna yoyote ile kinaweza kujitofautisha na kutofautishwa na kabila au dini fulani. CHAMA ambacho wanachama wanaweza wakatoka mbele na kujisifia (hapa namaanisha wasomi maana wao ndio waoga kuliko wasiosoma).
Mjengwa yupo sahihi kiasi fulani ingawa si lazima uwe mti mrefu km watu wanavyotarajia wapime height la hasha anamaanisha mti unaoonekana. Ingawa CONCEPT yake is prune to critism kwamba extent ya urefu wa mti (kwangu mie naona bora ustawi wa mti) inatakiwa isizidi miti mingine.
 
Huu ujumbe ni Wa JK na CCM hususani pale ambapo Makamba alidiriki kusema ya kuwa CCM haina mtaji mwingine unaozidi JK. Hata itikadi ya CCM iko chini ya miguu ya JK.

Kauli yako hii rafiki yangu Maggid yathibitisha ukweli huu:-

Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma.
 

jmushi1,

..nimesoma kwamba kampeni za CUF na Prof.Lipumba zimepokelewa vizuri sana ukanda wote wa kusini mwa Tanzania.

..kwa upande mwingine, Prof makes a lot of sense katika mambo mengi anayoyazungumzia. he would have helped himself kama angeamua kujijenga kwanza kama mbunge kabla ya 2010.

..sasa, ukiweka mapenzi ya chama pembeni, ukasikiliza hoja kwa hoja, baina ya JK,Prof.Lipumba,na Dr.Slaa, naamini kabisa you will end up with a toss up btn Lipumba and Slaa.

..kwa upande wangu nadhani kura za Uraisi hazitatofautiana sana baina ya vyama vitatu CCM,CUF,na Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…