Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
CCM kujivua gamba ni ngumu sana.
Binafsi nadhani CCM kinahitaji Katibu Mkuu aliyekuwepo kwenye ama TANU au ASP pia ili kukidhi mahitaji ya sifa ya uzalendo na uadilifu.
Umma umeishaaminishwa kuwa ufisadi ni zao la CCM na siyo zao la TANU na ASP. Kama wapo mafisadi wa CCM ambao walikuwa wafuasi wa TANU na ASP basi hao wameambukizwa ufisadi na CCM.
TANU na ASP havikuwa na rekodi ya ufisadi bali uadilifu na uzalendo vilivyojulikana duniani.
Hakuna wafuasi, Makada na Makamisaa waliopata ukwasi ndani ya TANU na ASP bali wamepata ndani ya CCM ambacho falsafa yake ni kujitegemea na kwamba ni chama cha wakulima na wafanyakazi kada ambazo haziwezi kutengeneza matajiri wa haki kutokana na kuwa hazina mazingira ya kutajirika hapa Tanzania.
TANU na ASP iliamini hao ni wanyonyaji na makupe kutokana na kuwa kazi ndani ya vyama hivi na taasisi zao zilikuwa ni za kujitolea 100%.
TANU na ASP vilitegemea rasilimali za wafuasi kujiendesha SIYO wafusi walitegemea rasilimali za vyama hivi kutajirika. Mfumo huu ulikuwa mzuri sana kwa sababu ulikuwa unachuja mchele na chuya.
CCM kimekuja kurithi tunu hiyo tangu 1977 lakini kimeelemewa na uchu mkali, tamaa kali, kiburi kikali, udikteta mkali na kujikuta kikipoteza tunu hiyo.
CCM madaraka yanagombaniwa kwa utakatifu na ulozi pia wakati dhamana za madaraka ndani ya TANU na ASP ziliogopwa kama ukoma.
Katibu Mkuu anayekifaa CCM ni aliyekitumikia TANU pia kwa wadhifa andamizi.
Naomba kutoa hoja.