NEMC inawakumbusha Wawekezaji kupata cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linapenda kuwakumbusha wawekezaji wa miradi juu ya takwa la sheria ya mazingira linaloelekeza miradi kupata cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi. Wito huo umetolewa na Afisa Elimu ya Jamii wa NEMC, Suzan Chawe leo 31 Julai 2023 Jijini Mbeya wakati akiongea kwenye Maonesho ya nane nane Kimataifa Jijini Mbeya.

Baraza limerahisisha mchakato wa TAM kwa kuanzisha usajili wa miradi
kwa mfumo wa kielektroniki (online) na kusogeza huduma katika ofisi zetu za Kanda zinazopatikana Tanzania nzima. Amesema Suzan Chawe

Aidha, tunawakaribisha wenye sifa za kuwa washauri elekezi wa Mazingira kujisajili na kupata cheti cha utendaji kwa ajili ya kufanya TAM na ukaguzi wa mazingira

Pia Suzan Chawe ameongeza kwamba, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linawakaribisha Watu wote kwenye Banda lake mkabala na Banda la Ofisi ya Makamu wa Rais kwenye maonesho ya 8 8 katika viwanja vya John Mwakangale

Huduma mbalimbali zinatolewa ikiwemo:
1. Usajili wa wataalamu elekezi wa Mazingira.
2. Usajili wa miradi kwa ajili ya cheti Cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira.
3. Elimu ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira
4.Pamoja na Kupokea malalamiko na maoni yanayohusu mazingira na kuyashughulikia.

Mazingira yetu, Uhai wetu, Tuyatunze yatutunze

 
Back
Top Bottom