Habari zenu?
Naomba mnisaidie mawazo, mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 4, nimeolewa kwa ndoa ya kanisani kabisa mwaka 2004.
Mume wangu alikuwa mtu mzuri sana kwangu yaani sijawahi kupata mwanaume kama yeye sema sasa familia yake ni watu wabaya sana, kabla sijaolewa watu walinishika masikio ooh huo sio ukoo unaouingia mie nikaona wazushi maana nilikuwa na mimba ya mume wangu ambaye ndio huyu mtoto wetu. Mama mkwe wangu ni nesi na wakati nina mimba nilikuwa napima kwake Tumbi Hospital miguu ilikuwa inavimba mama mkwe ananiambia ndio vizuri yeye anapenda miguu ivimbe mie mimba ya kwanza sijui hili wala lile. Mzazi ni mzazi mama yangu akili ilikuwa haimpi akachukua kadi langu mpaka muhimbili kufika huko wakamtaka mgonjwa ambaye ndio mie namam yangu akanipigia simu nikafika pale. Kufika nesi wa kwanza kaniambia panda kwenye mzani kupima duh akaanza kuita wenzie nilikuwa na kilo 108 kwa kweli mume wangu alikuwa ananitimizia kila ninachokitaka, baada ya hapo nikaenda kupima pressure duh hapo ndio ukaanza mtafutano yaani pressure iko juu mpaka aisomi kuangalia miguu wakaanza kumsemamama yangu kwanini yuko na mie katika hali ile? nikachukuliwa juu kwa dr. duh! kuona vile dr pale pale akaniandikia siza maana mtoto alikuwa anachungulia ila kila dr akija akipima pressure anakimbia anasema ahataki kesi. Nilipata kisu saa mbili usiku tangu saa saba mchana na madaktari walikuwa wanasema either afe mtoto or mie au tufe wote na sio kubaki wote ila namshukuru mungu kwamba tulibaki wote na wanafunzi muhimbili wasoma hilo somo nikapewa offer sikulipa hata shilling.
Tangu nimejifungua sikumuona mama mkwe wangu kwa miezi 2.
Baada ya hapo vikaanza visa kwa mkwe wangu ooh anamwambia mume wangu aache kazi dar aende kwao kibaha akafanye kazi, na visa tele kuwa ananiendekeza mie mwanamke. Siku moja mume wangu tuligombana sana mwishoe akaanza kutoa siri za kwao kuwa kabla sijaolewa ndugu zake waliniendea sehemu ili nikubali kuolewa na yeye ingawaje yeye alikuwa ananipenda ukweli sema ndugu zake walikuwa wana hofu nitakataa, pia kabla sijaolewa nilikuwa naona mambo ya ajabu ajabu kwa wifi zangu kila leo majumbani kwao hakweshi kuwa na waganga. Mume wangu na nduguze ni wazigua na mam mkwe ni mbondei.
Baada ya miaka 2 ya ndoa yetu mama mkwe alimtafutia mwanae kazi Kibaha ikabidi aache kazi dar aende kibaha na yeye mama mkwe anaishi huko kibaha. siku moja mume wangu alikuja akanieleza kuwa natakiwa kuhamia kibaha yaani mimi na yeye, nikamuuliza mume wangu the way ndugu z\ako walivyo hivyo itawezekana kwelikukaa karibu nao? Yeye mume wangu alikuwa ananipa moyo sana ila mie machale yalikuwa yananicheza sana maana mama mkwe wangu ni mswahili sana. NIkamueleza kuwa mie siwezi kwenda huko basi ndugu zake wakamtia maneno akahama nyumbani aliniacha sina kazi walamtaji na nina mtoto wa miaka 2 kipindi hicho kwa kweli maisha yalikuwa magumu sana ila nilikomaa nayo. mungu si athumani ndani ya miezi 4 nikapata kazi na kuanza maisha yangu, sasa ni miaka 2 tangu tuwe mbali mbali yeye mwanaume alishavua pete hana na siku moja alitaka kuchukua zangu nikamuomba kumwambia hii ni kinga ili nilee mwanangu.
Sema sasa tangu kipindi hicho yaani nikipata bwana nimekaa nae siku nyingi mwezi lazima tuachane kwa kisa au bila ya kisa, nikipata mwanaume hata nimtie ndani ya mboni ya jicho hakai hii miaka miwili nimebabaisha wee sasa mpaka naona umri unakwenda na mwanangu anataka mdogo wake.
Naombeni ushauri wenu sijaona baba wa kuzaa nae baada ya mume wangu maana wote hatukai nao siku nyingi, na pia sipendi kuzaa kila mtoto na babake je mwanishauri nirudi kwa yule mume wangu? Ingawaje mume wangu alinionyesha kuwa yeye sio strong kwa kumsikiliza mama na nduguze? Na pia najua ni ukoo usionifaa sasa nakuwa namnyima haki mtoto wangu yaani huyo tu ndio ananiumiza mimi. ushauri wenu ndio utaniweka pahali pazuri nateseka sana na mawazo mume wangu nampenda na najua yeye ananipenda sema tatizo ni ndugu zake na mama yake na nguvu za giza alizokuwa nazo.
Mkiwa!