Mama Mkwe wangu ananivunjia heshima

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,098
4,246
"Akina mama wa Kidamba yaani Wandamba wa Malinyi Morogoro hii ni asili yenu au huyu mama mkwe wangu ana lake jambo.

Iko hivi nimeoa kwa ndoa sasa mwaka wa pili ndani mke wangu tunaheshimiana sana changamoto ni mama mkwe akija nyumbani kusalimia hakuna kazi atafanya ikitokea Binti yake anaumwa basi nitafanya Mimi kazi za ndani mama anaangalia tu lakini pia sisi tukitoka nyumbani kwetu nilishatoa maelekezo Kwa mke wangu haijalishi nyumbani amebaki nani lazima chumba tunacholala na mke wangu kifungwe na funguo tuwe nazo sisi wenyewe

lakini ajabu siku moja mama mkwe alihoji kwa Nini mnafunga chumba chenu wakati Mimi nipo? Hatukumjibu Siku za hivi karibuni nilienda Malinyi kwani shughuli zangu za kilimo ni huko tulishajenga kibanda cha kufikia lakini kwa vile sisi tunaishi mkoa mwingine pale tulimwacha mama mkwe akae.

Akiwa anafahamu kabisa kwamba nipo safarini naenda Malinyi huyu mama katika chumba chetu alileta mwanaume maana yeye hajaolewa nilifika usiku kwa changamoto za usafiri pale nakuta anajivinjari nililazimika kulala Lodge asubuhi mapema niliamkia pale nyumbani nikabadili nguo nivae za kwendea shamba bado nikamkuta hawara yake yupo.

Kwa tamaduni za kwetu sikuingia ndani alitumwa mtoto akaniletea nguo nikabadilishia bafuni nikaenda shamba.Hilo likapita wakati naandaa shamba yeye alisema kijana wake ambae ni shemeji yangu ana ng'ombe hivyo nisitafute ng'ombe wa kulimia kwingine basi nikalipa pesa kabisa kuwahi nafasi ili msimu ukianza waanze kunilimia Mimi

lakini tarehe za kulima zilipofika wakagoma kulima shamba langu nikamuuliza shemeji kwa nini wakati nilishalipa pesa mapema nikajibiwa mama mkwe amezuia kulimiwa Mimi hadi wamalize mashamba yao.

Naunganisha dot naona kama huyu mama mkwe heshima ninayompa hailingani na anayonilipa nasisitiza binti yake hana tabia hizi naomba kujua nifanye nini au huyu mama kusudio lake nini kwenye ndoa yetu na zaidi ni mbinafsi hata tumpe msaada kiasi gani haonyeshi kurizika ni lawama tu amefikia hatua ya kusema mwanaume anaemuoa Binti yake ikiwa hatoelewana na yeye mama mkwe basi hatodumu na Binti yake.

Mimi nilikuwa nikisikia huyu mama ana uhitaji wowote nitapambana kumtimizia lakini kwa hizi tabia na matendo na kauli zake nafika hatua natamani kuamua niishi kwa kutoelewana nae ili niweke mipaka ya kutozoeana kwa Afya ya ndoa yangu. Naomba maoni na ushauri wa wadau tafadhali"
 
Wewe ni Mjinga na unaonekana hujakamilika kama Mwanaume kamili yaani Mama Mkwe analeta mwanaume wake kwenye kitanda unacholala na Mkeo unahisi kwa nini kafanya hivi?sababu kubwa jitathmini kama ni mwanaume kamili au lah Asante
Inawezekana mkewe kavujisha siri kuwa mshkaji wanadinyana mara moja kwa mwezi, tena kwa mbinde sana hadi astuliwe na betri ya gari
 
Screenshot_2024-02-10-14-33-14-596_com.twitter.android.jpg
 
Watoto wa firauni wangekwambia mpe kamba mama mkwe heshima irudi.. Haiwezekani ajue unakuja na alete mwanaume. Kwanza kwa familia zenye maadil hutakiwi kushea hata bafu na mama mkwe yaani kitendo cha kuona mama mkwe anaenda kuoga au toilet hiyo ni aibu kwa mkwe sasa nyie mnaoshea had vitanda 🤔
 
Huyo mama mume wake alifariki au aliachwa??
Kama ni singo maza wa kuachwa wengi wao wanakuaga na wivu kwa watoto wao.

Kama mwanamke kalelewa na singo maza basi katatizo kanaweza kua kwa mke kwa kuiga tabia za mama au mama kwa kua na wivu kwa mwanae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom