Ndugu za mume wangu na mama Mkwe wananichanganya

Mkiwa

Member
Feb 25, 2008
12
1
Habari zenu?

Naomba mnisaidie mawazo, mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 4, nimeolewa kwa ndoa ya kanisani kabisa mwaka 2004.
Mume wangu alikuwa mtu mzuri sana kwangu yaani sijawahi kupata mwanaume kama yeye sema sasa familia yake ni watu wabaya sana, kabla sijaolewa watu walinishika masikio ooh huo sio ukoo unaouingia mie nikaona wazushi maana nilikuwa na mimba ya mume wangu ambaye ndio huyu mtoto wetu. Mama mkwe wangu ni nesi na wakati nina mimba nilikuwa napima kwake Tumbi Hospital miguu ilikuwa inavimba mama mkwe ananiambia ndio vizuri yeye anapenda miguu ivimbe mie mimba ya kwanza sijui hili wala lile. Mzazi ni mzazi mama yangu akili ilikuwa haimpi akachukua kadi langu mpaka muhimbili kufika huko wakamtaka mgonjwa ambaye ndio mie namam yangu akanipigia simu nikafika pale. Kufika nesi wa kwanza kaniambia panda kwenye mzani kupima duh akaanza kuita wenzie nilikuwa na kilo 108 kwa kweli mume wangu alikuwa ananitimizia kila ninachokitaka, baada ya hapo nikaenda kupima pressure duh hapo ndio ukaanza mtafutano yaani pressure iko juu mpaka aisomi kuangalia miguu wakaanza kumsemamama yangu kwanini yuko na mie katika hali ile? nikachukuliwa juu kwa dr. duh! kuona vile dr pale pale akaniandikia siza maana mtoto alikuwa anachungulia ila kila dr akija akipima pressure anakimbia anasema ahataki kesi. Nilipata kisu saa mbili usiku tangu saa saba mchana na madaktari walikuwa wanasema either afe mtoto or mie au tufe wote na sio kubaki wote ila namshukuru mungu kwamba tulibaki wote na wanafunzi muhimbili wasoma hilo somo nikapewa offer sikulipa hata shilling.
Tangu nimejifungua sikumuona mama mkwe wangu kwa miezi 2.

Baada ya hapo vikaanza visa kwa mkwe wangu ooh anamwambia mume wangu aache kazi dar aende kwao kibaha akafanye kazi, na visa tele kuwa ananiendekeza mie mwanamke. Siku moja mume wangu tuligombana sana mwishoe akaanza kutoa siri za kwao kuwa kabla sijaolewa ndugu zake waliniendea sehemu ili nikubali kuolewa na yeye ingawaje yeye alikuwa ananipenda ukweli sema ndugu zake walikuwa wana hofu nitakataa, pia kabla sijaolewa nilikuwa naona mambo ya ajabu ajabu kwa wifi zangu kila leo majumbani kwao hakweshi kuwa na waganga. Mume wangu na nduguze ni wazigua na mam mkwe ni mbondei.

Baada ya miaka 2 ya ndoa yetu mama mkwe alimtafutia mwanae kazi Kibaha ikabidi aache kazi dar aende kibaha na yeye mama mkwe anaishi huko kibaha. siku moja mume wangu alikuja akanieleza kuwa natakiwa kuhamia kibaha yaani mimi na yeye, nikamuuliza mume wangu the way ndugu z\ako walivyo hivyo itawezekana kwelikukaa karibu nao? Yeye mume wangu alikuwa ananipa moyo sana ila mie machale yalikuwa yananicheza sana maana mama mkwe wangu ni mswahili sana. NIkamueleza kuwa mie siwezi kwenda huko basi ndugu zake wakamtia maneno akahama nyumbani aliniacha sina kazi walamtaji na nina mtoto wa miaka 2 kipindi hicho kwa kweli maisha yalikuwa magumu sana ila nilikomaa nayo. mungu si athumani ndani ya miezi 4 nikapata kazi na kuanza maisha yangu, sasa ni miaka 2 tangu tuwe mbali mbali yeye mwanaume alishavua pete hana na siku moja alitaka kuchukua zangu nikamuomba kumwambia hii ni kinga ili nilee mwanangu.

Sema sasa tangu kipindi hicho yaani nikipata bwana nimekaa nae siku nyingi mwezi lazima tuachane kwa kisa au bila ya kisa, nikipata mwanaume hata nimtie ndani ya mboni ya jicho hakai hii miaka miwili nimebabaisha wee sasa mpaka naona umri unakwenda na mwanangu anataka mdogo wake.

Naombeni ushauri wenu sijaona baba wa kuzaa nae baada ya mume wangu maana wote hatukai nao siku nyingi, na pia sipendi kuzaa kila mtoto na babake je mwanishauri nirudi kwa yule mume wangu? Ingawaje mume wangu alinionyesha kuwa yeye sio strong kwa kumsikiliza mama na nduguze? Na pia najua ni ukoo usionifaa sasa nakuwa namnyima haki mtoto wangu yaani huyo tu ndio ananiumiza mimi. ushauri wenu ndio utaniweka pahali pazuri nateseka sana na mawazo mume wangu nampenda na najua yeye ananipenda sema tatizo ni ndugu zake na mama yake na nguvu za giza alizokuwa nazo.

Mkiwa!
 
Pole sana mama,

Ukiona watu hatujibu si kwa sababu hatujali ila ni kutokana na uzito wa masuala yenyewe.Mimi si mtaalamu wa mambo ya familia na hivyo siwezi kusema mengi zaidi ya kwamba ndoa ni ya watu wawili na ingawa ndugu wana ushawishi mkubwa, kama mnapendana sana wenyewe mtakuja kushinda matatizo yenu.Wanasema hakuna kizuri kiso vikwazo.Kitu kikubwa ni kupendana na kujua kujitegemea kwani kama hamna kupendana na kujitegemea hata nia na uhuru wa kuendelea pamoja unakosekana.

Mtu mbaya unammaliza ubaya wake kwa uzuri tu, mpaka siku moja (kama si shetani mwenyewe) atakuja kuelewa ubaya wa choyo chake na inda zisoyumkinika.
 
duh kweli pundit uliyoyasema....matatizo mengine kuyajibu waweza chochea moto bureee ila jus know tuko pamoja mama yetu sana sana mie napendaga kuwashauri watu wakiwa katika hard times ehh wakae karibu na Mungu maana he is the only one wa kutujali kwa kila kitu tumwombe yeyey na ye atatutimizia...ndi ahadi aliyotupa!!!!
 
Cha muhimu katika ndoa ni UPENDO baina wa wanandoa, it must be a mutual relationship. Sasa je unampenda bado unampenda mumeo? au unampenda mwanao kuliko mumeo? na Je ni lazima uwe na watoto zaidi ya mmoja? Kama unajisikia unampenda basi rudi kwa mumeo, unamuachia mwanya ataibiwa bure na manyang'au ya mjini, take care usijeachiwa suruali ukabaki unahesabu paa.

Nina wasiwasi na mapenzi yako kwa mumeo, upendo umeshuka na ndio maana unayatilia mambo mabaya ambayo yatajustfy kumpiga kibuti. Vinginevyo ulionja vya nje kabla na ndio maana ulithubutu kuwa na wanaume kadhaa wakati ukijua fika ndoa yenu haijavunjika rasmi. Hukua kwa kiu ya mwanaume kiasi hicho kwani mumeo alikuwa bado ana open doors kwako-hakukupiga marufuku kwenda kwake ila wewe ndio hutaki kwa kisingizio cha ndugu zake. Ilikuwa ni kumfungia safari na kwenda hapo Kibaha tu kuliko kuwa na wanaume wengine.

Dada kaa chonjo na wanaume wa siku hizi especially wakitanzania. Kumuoa mtu ambaye ana mtoto tayari ni wachache sana wanaweza kufanya hivyo. Pia kumbuka ndoa yako ni ya kikristo, sio rahisi kuivunja na ukaweza kuolewa tena mbele za Mungu isipokuwa kifo kiwatenganishe, inawezekana ndio maana wanaume wanakuja kukutumia na kisha kutimua zao.

Huwezi kumfanya mumeo akupende wewe kuliko anavyowapenda ndugu zake, lazima kuna kitu kutoka upande wa pili wa shilingi ambao hujauweka hapa (ninahisi tu). Kama unampenda utayaweka kando mabaya na kusikilizia mazuri tu. Acha na hayo mambo ya kupendwa na ndugu zake, kwani wewe umeolewa na ukoo?

Fanya unavyoona inakusuit wewe, mapenzi ni ya watu wawili na wewe ndio unajua what you get and what you are missing. Usikilize moyo wako zaidi.
 
...mume wangu alinionyesha kuwa yeye sio strong kwa kumsikiliza mama na nduguze

Na pia najua ni ukoo usionifaa

sasa nakuwa namnyima haki mtoto wangu yaani huyo tu ndio ananiumiza mimi.

mume wangu nampenda na najua yeye ananipenda sema tatizo ni ndugu zake na mama yake na nguvu za giza alizokuwa nazo.

Mkiwa!

Mkiwa, kwanza pole kwa yaliyokusibu,

ushauri wangu ni huu;

* ndoa ni baina ya nyie wawili, kipimo cha ndoa imara ni msimamo wa kila mmoja wenu katika kuilinda, kuiheshimu na kuthamini ndoa yenu, hilo ni jukumu lenu wote, sio lako peke yako, au lake pekee. Iwapo mmoja wenu anayumba yumba, matatizo hayataisha ndani ya nyumba yenu

* bahati mbaya ya jamii zetu za kiafrika, ukioa au ukiolewa jua kwa namna moja au nyingine familia zote mbili zitahusika, hasa panapotokea ugonjwa, kifo nk... Hiyo dalili ya ukoo kutokukufaa, ni dalili tosha kukuonyesha iwapo patatokea ugonjwa au kifo utawekwa kwenye kundi gani!, Haipendezi, na huwa inaniksikitisha sana kuona kina mama wengi ndio wanaoathirika kwenye kutengwa, kusimangwa, na hata kudhulumiwa mali na haki anazostahili mfiwa, mjane, hasa kama mumeo tokea mwanzo hakuwa na msimamo wa kukulinda pindi lolote linapotokea. Liangalie hilo kwa makini.

* Unamnyima vipi mwanao haki yake? sidhani kama imeandikwa popote ni haki ya mtoto kupata mdogo wake. Kuzaa ni majaaliwa, vile vile haipendezi kwa mazingira uliyokuwa nayo kuongeza mtoto eti tu kwa sababu ya kuiokoa ndoa yako. Usitumie mtoto kama kinga! Mlee mwanao, na hakikisha unampatia mapenzi na mahitaji yote anayostahiki kupata, kama ndoa yako haikujaaliwa kuwa, huyo mtoto ni faraja pekee itayokusaidia kuendelea na maisha, badala ya kulazimisha mapenzi kwa kuzaa tena.

* Katika ndoa, uliwaacha wazazi na ndugu zako ili kuolewa na kuishi na huyo bwana, naye anastahiki kuwaacha ndugu zake ili aweze kuishi nawewe. Iwapo hayupo tayari kuukubali ukweli huo, hiyo ndoa yenu itaendelea kuwa ya mashaka na migogoro isokwisha.

iwapo unaamini ukweli kabisa anakupenda, na yupo tayari kurudiana nawe, basi mshauri mkae mbali na hao ndugu zake, na wewe pia hivyo hivyo. Some men are 'Mummy's Boys', wao kila kitu mpaka kwa ushauri wa mama zao! Taabu kweli kweli...

Jihadhari pia na hayo mahusiano ya muda mfupi na wanaume wengine, huenda unajitumbukiza zaidi shimoni badala ya kujinasua. Jipe muda wa kutafakari na kujua nini roho yako inataka badala ya hayo mawazo yako yanataka. Maombi na sala yatakusaidia, pia kuondokana na hizo imani potofu.

Ni mtizamo wangu tu,

Pole sana.
 
Dada yangu,

Pole sana kwa matatizo. Ila nakuomba kama ukijisikia nenda Kibaha ukapate sacrament yako kisha rudi dar, haya mambo ya kuhangaika na wanaume si mazuri utambulia HIV bureeee.
 
Habari zenu?

Naomba mnisaidie mawazo, mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 4, nimeolewa kwa ndoa ya kanisani kabisa mwaka 2004.
Mume wangu alikuwa mtu mzuri sana kwangu yaani sijawahi kupata mwanaume kama yeye sema sasa familia yake ni watu wabaya sana, kabla sijaolewa watu walinishika masikio ooh huo sio ukoo unaouingia mie nikaona wazushi maana nilikuwa na mimba ya mume wangu ambaye ndio huyu mtoto wetu. Mama mkwe wangu ni nesi na wakati nina mimba nilikuwa napima kwake Tumbi Hospital miguu ilikuwa inavimba mama mkwe ananiambia ndio vizuri yeye anapenda miguu ivimbe mie mimba ya kwanza sijui hili wala lile. Mzazi ni mzazi mama yangu akili ilikuwa haimpi akachukua kadi langu mpaka muhimbili kufika huko wakamtaka mgonjwa ambaye ndio mie namam yangu akanipigia simu nikafika pale. Kufika nesi wa kwanza kaniambia panda kwenye mzani kupima duh akaanza kuita wenzie nilikuwa na kilo 108 kwa kweli mume wangu alikuwa ananitimizia kila ninachokitaka, baada ya hapo nikaenda kupima pressure duh hapo ndio ukaanza mtafutano yaani pressure iko juu mpaka aisomi kuangalia miguu wakaanza kumsemamama yangu kwanini yuko na mie katika hali ile? nikachukuliwa juu kwa dr. duh! kuona vile dr pale pale akaniandikia siza maana mtoto alikuwa anachungulia ila kila dr akija akipima pressure anakimbia anasema ahataki kesi. Nilipata kisu saa mbili usiku tangu saa saba mchana na madaktari walikuwa wanasema either afe mtoto or mie au tufe wote na sio kubaki wote ila namshukuru mungu kwamba tulibaki wote na wanafunzi muhimbili wasoma hilo somo nikapewa offer sikulipa hata shilling.
Tangu nimejifungua sikumuona mama mkwe wangu kwa miezi 2.

Baada ya hapo vikaanza visa kwa mkwe wangu ooh anamwambia mume wangu aache kazi dar aende kwao kibaha akafanye kazi, na visa tele kuwa ananiendekeza mie mwanamke. Siku moja mume wangu tuligombana sana mwishoe akaanza kutoa siri za kwao kuwa kabla sijaolewa ndugu zake waliniendea sehemu ili nikubali kuolewa na yeye ingawaje yeye alikuwa ananipenda ukweli sema ndugu zake walikuwa wana hofu nitakataa, pia kabla sijaolewa nilikuwa naona mambo ya ajabu ajabu kwa wifi zangu kila leo majumbani kwao hakweshi kuwa na waganga. Mume wangu na nduguze ni wazigua na mam mkwe ni mbondei.

Baada ya miaka 2 ya ndoa yetu mama mkwe alimtafutia mwanae kazi Kibaha ikabidi aache kazi dar aende kibaha na yeye mama mkwe anaishi huko kibaha. siku moja mume wangu alikuja akanieleza kuwa natakiwa kuhamia kibaha yaani mimi na yeye, nikamuuliza mume wangu the way ndugu z\ako walivyo hivyo itawezekana kwelikukaa karibu nao? Yeye mume wangu alikuwa ananipa moyo sana ila mie machale yalikuwa yananicheza sana maana mama mkwe wangu ni mswahili sana. NIkamueleza kuwa mie siwezi kwenda huko basi ndugu zake wakamtia maneno akahama nyumbani aliniacha sina kazi walamtaji na nina mtoto wa miaka 2 kipindi hicho kwa kweli maisha yalikuwa magumu sana ila nilikomaa nayo. mungu si athumani ndani ya miezi 4 nikapata kazi na kuanza maisha yangu, sasa ni miaka 2 tangu tuwe mbali mbali yeye mwanaume alishavua pete hana na siku moja alitaka kuchukua zangu nikamuomba kumwambia hii ni kinga ili nilee mwanangu.

Sema sasa tangu kipindi hicho yaani nikipata bwana nimekaa nae siku nyingi mwezi lazima tuachane kwa kisa au bila ya kisa, nikipata mwanaume hata nimtie ndani ya mboni ya jicho hakai hii miaka miwili nimebabaisha wee sasa mpaka naona umri unakwenda na mwanangu anataka mdogo wake.

Naombeni ushauri wenu sijaona baba wa kuzaa nae baada ya mume wangu maana wote hatukai nao siku nyingi, na pia sipendi kuzaa kila mtoto na babake je mwanishauri nirudi kwa yule mume wangu? Ingawaje mume wangu alinionyesha kuwa yeye sio strong kwa kumsikiliza mama na nduguze? Na pia najua ni ukoo usionifaa sasa nakuwa namnyima haki mtoto wangu yaani huyo tu ndio ananiumiza mimi. ushauri wenu ndio utaniweka pahali pazuri nateseka sana na mawazo mume wangu nampenda na najua yeye ananipenda sema tatizo ni ndugu zake na mama yake na nguvu za giza alizokuwa nazo.

Mkiwa!

Pole sana na matatizo. Je, wewe mwenyewe upo tayari kuishi na ndugu za mume wako na mama yake pamoja na kuwa unawajua tabia yao ya kishirikina? Baba mtoto anakusaidia matumizi ya kulea mtoto mliyejaliwa? Kama hakusaidii je, una kipato cha kukutosha katika gharama za kila siku na mtoto mliyejaliwa? Kama jibu la mengi ya maswali hayo ni hapana, basi mimi ushauri wangu ni kwamba huna haja ya kwenda Kibaha. Piga konde moyo na uendelee na maisha yako na huna haja ya kuwa na mtoto mwingine kama kipato ulichokuwa nacho hakiwatoshi wewe na huyo mtoto wako wa kwanza. Hakuna ukweli wowote kwamba kila mtoto anakuja na riziki yake. Maisha ya leo ni magumu, hivyo sasa hivi kipaumbele chako kiwe ni kuhakikisha mna maisha mazuri wewe na mwanao na siyo kupata mtoto wa pili.
 
Huo ushirikina unaosema siyo hisia tu kama za akina Sitta na Chenge! Kama kweli ungekuwa unampenda mme wako ungemshawishi mkae pamoja Dar au hata Kibaha lakini si kwa ndugu zake. Tatizo lingine walilonalo dada zetu ni kuwa mkishaolewa mnataka kuwatenganisha ndugu. Hivi bila hao ndugu, ungempata wapi huyo mme! Mimi I strongly disagree with this kind of attitude. Mimi nakuoa nikiwa na umri wa zaidi ya miaka 25. miaka yote hiyo nimekaa na dada na mama yangu, wewe kufika unaanza mara ndugu ni washirikina na blaa blaa zingine! Excuse me, why didnt you do a thorough search/due diligence kabla ya kuolewa. Unajua ndoa ni kama mkataba ambao unatakiwa kujua motto ya "buyer be aware"!
 
nenda tu kanisani ukaombewe ... kama there is any spell on you .... Mungu ataiondoa ... huwezi kupata raha na huyo mume wako as long as the mother is still alive ... maana wamekukataa ... na huyo mama anamwendesha mwanawe na remote ... huwezi kupigana vita kama hivi

Mtoto wako ni mmoja .. kulea mtoto mmoja si kazi ... jipange tu na ujidhatiti maana huenda hata ukanyanganywa kama watachukulia kwamba ndicho kitakacho kurudisha kwao ... jitulize ... usijaribu kureplace your husband immediately maana its too soon and hujaweza kufuta machungu ya nyuma ... wait till you are ready utapata tu atakaekupenda ... tena mtoto bado ni mdogo anahitaji utulivu katika ulezi ... just do the kid that sacrifice .. usimletee mijitu kila kukicha baba huyu mara yule ... utakosa heshima kwa manao maana watoto wa sikuhizi wanapata uelewa mapema
 
Pole sana Mkiwa,
nakubaliana na yote yaliyosema na hata uliyosema yanakusibu. ndoa na swala la mahusiano ni watu wawili yaani mume na mke. mahusiano yoyote ili yawe mazuri ni ya wawili hasa haya ya kimapenzi. akiingia mtu wa tatu basi hali huanza kuwa mbaya.
maswali yangu ya msingi kwako ni haya:
1: Je ulipoona mambo yanabadilika ulishirikisha rafiki zako wa karibu?
2: tatizo lilianzia wapi hadi ndugu wa mume wako wakaanza kutokukupenda?
3: Kwa nini hukuambata na mumeo kwenda huko alikoenda kufanya kazi?

-kama Jibu la swali la kwanza ni ndio basi hao marafiki ndio wabaya kwako. fikiria tena kwa makini ushauri waliokupa na ujaribu kurekebisha panapo makosa.
-kama unajua tatizo lilipoanzia basi uko ktk position nzuri ya kumaliza mzozo wako na mpenzi wako huyo na hata nduguze,
-kama hukuwa na sababu ya maana ya kutokuambatana na mumeo basi ujue unavuna ulichokipanda,
-
Ila hakijaharibika kitu kama mumeo anakuamini na hukuwahi kumsaliti. kama ulimsaliti ujue amejua ndio maana anakukwepa na wala si ndugu zake.

ukihitaji ushauri zaidi nitafute privately

ni mimi bingwa wa maswala ya mahusiano ya Kimapenzi
Mtumwa-Utuwani
 
pole sana mama,haya ni mapito katika maisha.
kitu kikubwa hapa ni kuangalia mapenzi yako kwa ex husband wako na pia mapenzi yake kwako, naamini hapo utakua na jibu zuri kwa maana penzi la kweli huvunja vikwazo vyote vilivyo mbele ya watu wawili,
pili, kama unaona huwezi kurudi kwa mmeo,hilo wazo la kuwa na mtoto mwingine,inabidi uliweke kando kwanza,ni hatari sana kuwa na watoto wenye baba tofauti halafu ukiwa hujaolewa,jamii huchukulia kama ni mwanamke muhuni tu,haiangalii njia ulizopitia.
Tafakari vizuri,usiwe na papara angalia na hali ya maisha ya sasa, na muombe mungu akupe nguvu katika hili na utapata majibu,mungu ni muweza wa kila kitu.
 
Asanteni sana kwa maoni yenu. Kama nilivyosema mie ni mama wa miaka 32 sasa mawazo yeu nimeyasoma na kuyaelewa ila sasa napenda kuwaelezea zaidi kuwa juzi niliomba kuonana na mume wangu kanisani mimi na yeye na mchungaji lakini kuonyesha kuwa matatizo yako kwao yeye alikuja na mkwe wangu wa kike na wifi yangu. Nilimwita chemba na kumueleza kuwa mchungaji alikuwa anatuhitaji sisi wawili lakini mama yake alisema kama yeye hataingia basi na waondoke na kweli waliondoka.

Mume wangu hana msimamo mke anamtaka na ndugu anawataka. Na nilipokuwa naongea nae mimi aliniambia kuwa mke wangu siwezi kupata mke kama wewe ila kama unaweza nipatie mtoto kweli jana ndio nimeachana nae rasmi bila ya talaka maana nilimjibu kama nimekukosa wewe basi naomba niachie mtoto.

Maana ndugu zake walisema kama mtoto atakuwa kwangu nijue mimi kwa lolote na kama akiwa kwao wao ndio watajua juu ya mtoto. Kwa kweli siwezi kusema sina maisha ya kumlea mwanangu ila mtoto anamjua babake kuna wakati huwa ananisumbua kidogo, sema nimeamua kupiga moyo konde na kutoka moyoni nilimpenda sana mume wangu ila amenitumbukia nyongo na sidhani kama nitakuja kumsamehe kwa hili ingawaje najua sio mwisho wa maisha.

Sihitaji mwanaume wa aina yeyote sasa nini naangalia ni mwangu ale alale na avae ili baadae asije kuona mie kumleta duniani nimesababishia matatizo. mume wangu si Strong man, yeye jana ananiambia ooh mie sijielewi nakumiss sana na ukiona naenda tofauti wewe ndio wa kuniokoa lakini jinsi nilivyoona mamake anavyomremote kwa kweli nitakuwa kwenye mtihani.

NI story ya kweli sijaongopa hata kidogo na ndio maana niliamua pia kusema ukweli wangu kuwa nilirukaruka kidogo ingawaje nilikuwa naruka salama sema nimeona kuwa mwanangu bado mdogo na anahitaji malezi yangu kama nimeshindwa kuwa na babake. Nawaahidi nimetulia nachoangalia ni mbele tu. Asanteni sana kwa mawazo yaani niliposema mawazo yenu jumatatu jioni nilienda kanisani nikaomba mchungaji ampigie tukutane pale na kweli alifika na hakuonyesha ubaya juu yangu ila naona kuna jinsi anavyopandikizwa sasa Hawezi kuwa baba bora atakuwa ni bora baba na hilo bora niliepuke mapema.

Mkiwa
 
Mungu mkubwa siku zote .... hauko pekeyako tuko nawewe na tunakupenda ... tunashukuru kwamba imejitambua na umekubaliana na hali ... Mungu akujaalie wepesi ... na akusogezee mengi mema ... Ameen
 
...simamia huo uamuzi wako, mw'mungu naye atakusaidia na kukupa kilicho na heri nawe. Kila la heri.
 
pole sana mama,
kwa haraka tu na kama mpita njia tunaweza kumlaumu sana mama mkwe.
mimi kama mama, pia, na mtoto wa pekee, wa kike najua jinsi wazazi wanavyoweza kujikuta wanahitaji msaada kuwaacha watoto wao wajitegemee.
ni ngumu sana hasa kama mama hakujenga ndoa nzuri na mumewe, anajikuta anakumbatia watoto hadi uzeeni. Ingemuhitaji mumeo awe na nguvu za ziada, na diplomacy ya ajabu kuwahandle wewe na mama yake.
si rahisi.
kama inawezekana ingieni pamoja kwa huyo mshauri, (wote watatu) kila mmoja afundishwe jinsi ya kuishi katika hio hali mliopo.
mimi namuonea sana huruma huyo bibi kwani anaogopa upweke.
itabidi wewe ujifanye karibu sana nae.
Ndio ukubwa huo.
Sasikia kuwa hata saa ingine huwa wanawake wanaomba kisiriri watoto wao wasipate mke mzuri kama yeye.
ila kutafuta replacement si vizuri,
ikishindikana kumuacomodate mama mkwe, then jitahidi usijeukawa kama yeye hapo baadae kwa kumkumbatia mno mtoto akashindwa kuishi na mkewe/mumewe kwa raha.
Always ni vigumu kuishi na mkwe anaempenda mwanae (from experience) you just lower your self, more than you do your parent,
we married women are stealing their last energetic men in the house. Lazima utumie akili.
 
Pole sana Mkiwa soma ushauri wa NaimaOmari ni mchango mzuri sana. Kuna watu kama mimi nimepitia the same situation uliyopitia. Ila namshukuru mungu naendelea vizuri na mwanangu. Sali Mungu atakuonyesha njia hakuna suluhisho zuri kama kumlilia Mungu na kumweleza shida zako though sometimes ni ngumu mpk unakata tamaa but you have to be strong ninafeelings zinaniambia you are very strong woman and you will make it. Mlee mtoto mama sasa hv uanze kutafuta damu zinginge za nini. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo wa ujasiri
 
Dada yangu pole sana,
kwa jinsi ulivyo eleza kuhusu ndoa yako inaonyesha ni ya kikristo hivyo basi nakuomba iweke hiyo hali katika mpango wa kumshirikisha MUNGU zaidi nikiwa na maana kuwa mcha MUNGU kweli kweli piga magoti ikiwezekana funga kwa ajili ya kumuombea huyo mume wako kwani inaonyesha bado unampenda. kwani ni shetani tu yupo hapo na hao wakwe zako hawamuogopi MUNGU.
hisijaribu tena kuhangaika na wanaume kwani lazima uwe mtu wa kusona na kujua nyakati hali ya dunia sasa ni mbaya (Ukimwi), na kwajinsi ulivyo na shida utampata mwanaume atakaye kupa mapenzi kweli kweli lakini ujuwe utapewa na vingine. nakuomba sali sana muite MUNGU wakati wote. MUNGu ni mwema wakati wote kwani ameweza kukupa hata mtoto huyo 1 ni jambo la kumshukuru pia.

bella
 
Pole Mkiwa,
Achana na kurukaruka. Concentrate kwenye kujiendeleza na kuangalia maisha yako na ya mwanao. Yaliyokupata yanapaswa kukupa fundisho kwa siku za mbeleni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom