Ndugu za mume wangu na mama Mkwe wananichanganya

Kwa faida ya mwanao mfuate mmeo Kibaha au mshawishi arudi Dar. Tumia njia ya maombi tu na si vinginevyo. Ikishindikana sana kaa utulie ulee mwanao na muombe Mwenyezi Mungu pekee atakusaidia, hakuna haja ya kuhangaika na wanaume utakufa uache mwanao mdogo Mungu atakujalia mme uliye ubavu wake. KWANI NI LAZIMA UWE NA MWANAUME?

Danga
 
POle sana Mkiwa.ndio ukubwa huo.lakini kama unaweza sali sana na kuomba mungu kwa yote.tUNAAMBIWA ADUI MPENDE sasa wewe hata kama hawakupendi we wapende sana .na zaidi mpende huyo mumewako dada.Mi nakushauri kama unampenda mumeo endelea kuwasiliana nae na ujenge utaratibu wa kumpeleka huyo mtoto huko ,ibaha angalau kwa masaa machache awe anaonana na baba ake.Mungu atakusimami mpendwa achana na wanaume kwa sas hawatakusaidia kitu dada.
 
mh pole san a dada yangu. Kwanza namlaumu huyo mama mkwe kwa kuamua kuingilia maisha ya mwanae ambaye keshaoa. Wewe huna haja ya kujilaumu kwa kuingia katika ukoo huo ni penzi ndilo llimekufanya ukaamua kuishi na bwana huyo.

Ila nakulaumu kwa kuamua kuwa na wanaume wengine wakati ndoa yenu haijavunjwa rasmi. Ungejaribu kuchunguza lengo hasa la huyo mama mkwe na kisa hasa cha mumeo kuamua kukuacha na kuhamia Kibaha. Hata hivyo fuata nafsi yako itakavyo kama unaweza kurudi tena kwa mumeo muombe sana MUNGU ili awe amebadilika na si kutegemea madawa.
kila la kheri
 
madaktari wa muhimbili useless hivi.. Yani wanakuambia kabisa kuwa either ufe wewe ama usife .lol ni akili hii kweli
 
madaktari wa muhimbili useless hivi.. Yani wanakuambia kabisa kuwa either ufe wewe ama usife .lol ni akili hii kweli

labda walikuwa wanamwandaa atubu kabisa dhambi zake..... Halafu kama umesoma vizuri wakamgeuza yeye ndo majaribio ya wanafunzi....

Ila mama mkwe mbaya sana alitaka binti afe ili iweje?
 
labda walikuwa wanamwandaa atubu kabisa dhambi zake..... Halafu kama umesoma vizuri wakamgeuza yeye ndo majaribio ya wanafunzi....

Ila mama mkwe mbaya sana alitaka binti afe ili iweje?

wanawake bana!.adui wa mwanamke ni mwanamke na adui wa mwanaume ni mwanamke na nyoka<shetani>
 
mie sikwambii pole, ila nakwambia kaza buti safari bado ndefu.

unajua nini kilitokea kati yako na wakwe zako?
wao hawakukupenda na mumeo alijua hilo na aliforce ili muoane akijua kwamba ataweza kuresist external forces ila kaproove kufeli. mumeo ni yule ambaye bado yuko nyumban yaani hajatoka kwao bado ni influenced na familia so ni ngumu sana kumbadilisha.

kosa ulilofanya wewe ni hili hapa ulipanic ukaanza kutafuta faraja badala ya the way out.
ushauri wangu.................kaa kwako lea mwanao achana na mawazo ya huyo bwana sikufichi ukirudi lazima wakutoe ndondocha tena watu wa kibaha ambao ndo ninaowajua mie hukawii kuzikwa gogo pangani kama si air msae.
 
If things go wrong, don't go with them. Kama ndoa imeshindikana fuata taratibu za kidini na kisheria ili uwe huru na maisha yaendelee. Usianze kuhangaika na wanaume wengine, utajitesa na kumtesa mwanao pia maana changamoto haziishi. Muda ukiwadia utafanya maamuzi mengine. Endelea kumuomba Mungu atakusaidia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom