Ndugu yenu nafilisika very soon

Ndugu yenu nafilisika very soon

Kijana nimejichanga hela kidogo nikaagiza mzigo wa simu na bidhaa zingine kutoka china kupitia shirika la usafirishaji wa DHL,sasa biashara yangu hii naona karibia nafilisika kabisa kutokana na kodi ninazolipa TRA.

Sasa wadau naomba njia yoyote itakayoniwezesha mimi kukwepa kodi au kuniwezesha nipunguze kiasi cha kodi nacholipa.

Nalipa kodi halali ila kiasi ni kikubwa sana kinaniumiza kwa kuzingatia Biashara hii yangu bado ndogo.

Nakaribisha maoni yenu na hata watakaonipa ushauri PM kunisaidia mimi mdogo wenu njia za kuweza kukwepa kodi.

Ahsante na karibuni.

Note: mambo ya #escrow pia yananipa machungu. :confused2:

cc: you

Je unakadiliwa kodi au unaandika mahesabu,yaani unaandaa hesabu zinaenda kukaguliwa TRA na wanakwambia kodi ya kulipa?
 
kwanini documents zangu za manunuzi wanazikataa? kwanini watumie market value zao?
Maskini kweli ntabaki kuwa masikini tu ila matajiri kina African Barrick na Tigo wao wanabadilisha majina tu...

Mkuu wataziaminije document zako kama hazioneshi chembe ya uhalisia?? yani uwaambie umenunua Range Rover Sport kwa Million 20 unafikiri watakwamini??? Alafu pia kabla hajasafirisha mizigo mtembelee ofisi za mapato mkaweke records clear ili hata kama una vipingamizi vya kodi wanayotaka uwalipe unamalizana nao mapema kabla ya huo usumbufu wote.. Pole mkuu ndo nchi yetu ilivyo hivyo, usishangae kijana amekaa custom miaka miwili ana ghorofa Mbezi Beach
 
Mkuu Price si ziko online, Ukinunua Toyota Rav 4 model fulani si wao wanaangalia kwenye websites za Toyota tu wanapata actual cost?? Au ulitaka wao wafanyaje labda??

Google "Toyota RAV4 MRSP" halafu ilinganishe na database ya TRA. Kisha rudi ufanye google tena what is MSRP (Imnajumuisha nini) labda utaelewa nina maanisha nini! MSRP ni Manufacturere "Suggested" Retail Price
 
kama una roho ngumu ya kupanda jahazi ni pm nikupe mchongo
 
Mkuu wataziaminije document zako kama hazioneshi chembe ya uhalisia?? yani uwaambie umenunua Range Rover Sport kwa Million 20 unafikiri watakwamini??? Alafu pia kabla hajasafirisha mizigo mtembelee ofisi za mapato mkaweke records clear ili hata kama una vipingamizi vya kodi wanayotaka uwalipe unamalizana nao mapema kabla ya huo usumbufu wote.. Pole mkuu ndo nchi yetu ilivyo hivyo, usishangae kijana amekaa custom miaka miwili ana ghorofa Mbezi Beach

Msaidie kijana apate njia ya kumfanya kuweza kupunguza hicho kiasi cha kodi, hadi kujenga ghorofa mbezi ni dalili za rushwa, mweleze vipi rushwa atatoaje na panya road inapitika vipi?

Nchi hii kodi vifaa vya electronics vipo juu sana kulinganisha na nchi zote za Africa Mashariki..
 
Simu zinalipiwa kodi? Hazipo katika ule exemption ya computer?
 
Msaidie kijana apate njia ya kumfanya kuweza kupunguza hicho kiasi cha kodi, hadi kujenga ghorofa mbezi ni dalili za rushwa, mweleze vipi rushwa atatoaje na panya road inapitika vipi?

Nchi hii kodi vifaa vya electronics vipo juu sana kulinganisha na nchi zote za Africa Mashariki..

Mwambie kesho anione ofisini kwangu pale TRA Tegeta... aje na bahasha ya kaki asiingie nayo bali amwachie mlinzi pale nje anaitwa Kapangawazi..
 
Labda wewe ni wa TRA au huwajui hao TRA. Yaani wanavyofanya assessment ya kodi unaweza ukabwaga mizigo airport. Just unrealistic kabisa. Mali uliyonunua $3,000 watakwambia ina thamani ya $8,000

Huwa wanafanya kusudi na wenyewe wanasema.Wanafanya hivyo ili kufikia malengo ya makusanyo waliowekewa.Wakiambiwa kwa mwezi wakusanye bilioni watakusanya hata kwa kubambikia
 
Ni PM nikupe mbinu au ubadilishe biashara,nitakuonyesha.
 
Kijana nimejichanga hela kidogo nikaagiza mzigo wa simu na bidhaa zingine kutoka china kupitia shirika la usafirishaji wa DHL,sasa biashara yangu hii naona karibia nafilisika kabisa kutokana na kodi ninazolipa TRA.

Sasa wadau naomba njia yoyote itakayoniwezesha mimi kukwepa kodi au kuniwezesha nipunguze kiasi cha kodi nacholipa.

Nalipa kodi halali ila kiasi ni kikubwa sana kinaniumiza kwa kuzingatia Biashara hii yangu bado ndogo.

Nakaribisha maoni yenu na hata watakaonipa ushauri PM kunisaidia mimi mdogo wenu njia za kuweza kukwepa kodi.

Ahsante na karibuni.

View attachment 205505
Note: mambo ya #escrow pia yananipa machungu. :confused2:

cc: you

tumekusikia tutakufikia!!
 
ukitaka kukwepa kulipa kodi muulize Reginald mengi
 
Back
Top Bottom