Ninasikitishwa sana na vyombo vya habari vya Tanzania. Kwangu mimi nilipongeza hatua ya serikali ya hivi karibuni ya kuyafungua magazeti mawili ( sio mwana halisi) kwa matarajio kwamba wana habari wetu watafika sehemu waache "ukasuku"
kwa namna habari ya Ufoo inavyotangazwa, tunakubaliana kwamba ni mtu "maarufu". ndio sababu vyombvopvyote vya habari kwa muda wa zaidi ya wiki moja vimekuwa vikishindana "kutafuta" habari yake. Jambo la kushangaza vyombo vyote( naamaanisha vyote) vimeshindwa kwenda hatua zaidi na kubaki kuimba kama kasuku yale yanayosemwa na watu fulani. Mara polisi, msimaji wa Moi, ndugu wa ufoo au shemeji wa ufoo! tena kwa yale ambayo hao wasemaji wanataka yaandikwe!
kwanini vyombo vyetu vya habari vinavyoitwa huru (hata hizi Blog) vuimeshindwa kufika sehemu na kutueleza zaidi ya ngonjera ambazo zimekuwa zikielezwa nma hao wanaokaririwa navyo.
1. inaelezwa kuwa huyo anayedaiwa kuwa muuaji alitoka Sudan ya kusini na kwenda moja kwa moja kilimanjaro kuzungumza na mama yake kabla ya kurejea dar es salaam: waandishi wetu kwanini wamehsindwa kufanya jitihada za kumwuliza huyo mama ni kitu gani hasa kilichokuwa kinamtatiza mtoto wake? na alikwenda kwake kufanya nini?
2. inaelezwa kuwa baada ya kufika dar es salaaam, wawili hao walikuwa katika gari moja wakielekea nyumbani kwao ufoo na kuwa ufoo alimpigia simu mama yake kuwa aondoke nyumbani kwani huyo mzazi mwenzie angeweza kumfanyia kitu kibaya: waandishi wetu kwanini hatuwezi kuhoji ilikuwaje huyu aliyekuwa akiendesha gari apige simu kumwleza mama yake kuwa kuna hatari na huku akiendelea kuendesha gari kuelekea katika hatari yenyewe?
3. ndugu mmoja ndani ya nyumba ya akina ufoo amekaririwa akisema kuwa alimwleza mwenzake kwenda kuangalia huko sebuleni kuna nini wakati yeye akiendelea kubaki chumbani: waandishi, ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na watu watatu, kulingana na taarifa za huyu jamaa ambaye pia alisema mzazi mwenzake na ufoo alijipiga risasi na kufa na ninyi mkadandia hivyo je inawezekanaje mtu ajipige risasi begani halafu aji[pige kidebvuni, au ndio habari za utawala wa MOI ulotoa ttaarifa za uchunguzi wa kifo cha Dr Robert Auoko kuwa alijipiga risasi akafa halafu akachoma moto mwil wake?
4. kwa nini mmeammua kufanya ubaguzi wa waziwazi kwa mzazi mwenzake na ufoo kuonekan mkosaji ( kwa kuua) ilihali hamtaki kutwambia CHANZO HASA cha mzozo huo ni kitu gani? tunaelezwa kuwa huyo mzazi mweziwe na ufoo alikuwa pia mwana habari akiwa pia amepitia ITV kwanini kumbagua, au kwa sababu ufoo hushika mafungu ya mshiko kwa wanahabari wanaokwenda kwenye ziara za vyama vya siasa. Igunga!.
5. Nilikuwa najiuliza siku nyingi malengo ya wahariri wa ITV kupenda kumtumia zaidi Ufoo saro katika safari za wanasiasa hasa chadema, ingawa siku hizi kumekuwa na mabadiliko kuwa ni kutokana na weledi wake mkubwa zaidi katika siasa au kuna sababu nyingine, na katikakufanya hivyo walikuwa wakiangalia ambacho kingeweza kujitokeza?
6 waandishi wetu habari ikitoka kwenye gazeti la mwananchi ukurasa wa mbele itakuwa hivyo hivyo katika magezeti mengine bila kufanya kazi ya ziada, hata kwenda kwa watalaamu wa saikolojia kutoa ushauri wao wa nini kinaweza kufanyika kwa mtu ambaye anajikuta katika hali kama ya huyo mzazi mwenzake na ufoo.
vinginevyo niwape pole waliokutwa na janga hilo nikiwatakia wapumzike kwa amani( waliofariki) na kupona kwa haraka wale wanouguza majeraha pamoja na waliopatwa msongo wa mawazo. lakini waanndishi wetu mmeshindwa katika hili na mengine mengi kiasi imefika wakati hata humu ndani watu wana fahamu kitu wanaishia kueleza ile mimba au ile nyumba.
Ndio sababu ni rahisi zaidi kupata habari ya tanzania kutokea marekani kuliko kutokea Tanzania.