Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

mbona inawezekana kabisa kuwa aliwapiga halafu akajipiga na yeye hizo mbili ili kuaminisha kuwa kulikuwa na mapambano fulani.
au alipigwa kwanza yeye akachukua risasi akawapiga wao za kutosha alipoona hali itakuwa mbaya kwake akajimaliza.


ahaa wasituchoshe tusubiri ufoo saro atoke aeleze na ukweli utajulikana.
 
si kuna waliokimbilia darini?wataeleza aliyeanza kupiga risasi ni nani
 
Au Mushi kweli alimshoot mama yake na katika purukashani akampiga Ufoo lakini hazikumpata vizuri na akanyangwa siraha na kumaliziwa yeye ya kiduvuni na begani. Ila mimi nadhani mama Ufoo alipigwa wa kwanza na wapili alikuwa Ufoo ila bahati nzuri hazikumpata vizuri, either mtu mwingine ndani ya nyumba au Ufoo mwenyewe alimnyanganya siraha hiyo na kumamlizia. Imani yangu ni kwamba Mushi hakujiua
Mbona linaelezeka kirahisi tu. Katika hali ya tukio hilo kuna uwezekano mkubwa kuwa kulikuwapo purukushani ya kujaribu kuzuia au kunyang'anyana hiyo silaha baada ya kumpiga mama mkwe. Purukushani hiyo inaweza kuelezea hiyo risasi ya begani. Baada ya huyo mwananume kupata tena udhibiti wa silaha yake, ndio akapata nafasi ya kumshambulia Ufoo na kudhani ameshawauwa wote wawili. Baada ya hapo, akajipiga risasi chini ya kidevu ili kujimaliza. Kama polisi wapo makini, sio kazi ngumu sana kubaini ni silaha ngapi/gani zilitumika katika tukio hilo. Hata hivyo, Ufoo anabaki kuwa shahidi muhimu sana katika tukio hili. Na ni kweli pia kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa mambo mengi tu yaliyojificha kuhusiana na kadhia hii.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Marehemu kajipiga risasi mbili? Eti moja begani na nyingine kidevuni. Kama Polisi wetu wangekuwa sio wavivu wa kuchunguza,hapo kulikuwa na neno jipya na la kustua.
 
Halafu mwandishi kaandika eti Mushi mpaka mauti inamkuta alikuwa mwajiliwa wa STR (badala ya ICTR) na uku anasema alikuwa Sudan. ni kwamba aliwahi kufanya kazi ICTR na sasa alikuwa UN Mission ya Sudan. Kwa hiyo tuseme alikuwa mwajiliwa wa UN upande wa Mawasiliano

Nukuu "... wakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa..."

Uandishi katika Vyombo vyetu vya "Bongo", iwe katika Kishahili au katika "ng'eng'e" ni janga!

Isitoshe, Marehemu Mushi bado ni MTUHUMIWA wa kujeruhi, kuua na kujiua kwa risasi kwa sababu uchunguzi wa Tukio bado kukamilika.

Hivyo angalau ingesomeka "... wakati mwili wa Marehemu Mushi, anayetuhumiwa kumjeruhi kwa risasi Mzazi mwenzie, Ufoo Saro, kumuua kwa risasi Mama wa Ufoo na kisha kujiua mwenyewe kwa risasi, ukiagwa..."
 
Uko sahihi mkuu, ila tatizo waandishi wa habari na washabiki wa Ufoo wanaandika na kuongea ili ionekane kwa asilimia mia Ufoo hana hatia wala hastahili kuhojiwa ushabiki umetujaa,
Nukuu "... wakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa..."

Uandishi katika Vyombo vyetu vya "Bongo", iwe katika Kishahili au katika "ng'eng'e" ni janga!

Isitoshe, Marehemu Mushi bado ni MTUHUMIWA wa kujeruhi, kuua na kujiua kwa risasi kwa sababu uchunguzi wa Tukio bado kukamilika.

Hivyo angalau ingesomeka "... wakati mwili wa Marehemu Mushi, anayetuhumiwa kumjeruhi kwa risasi Mzazi mwenzie, Ufoo Saro, kumuua kwa risasi Mama wa Ufoo na kisha kujiua mwenyewe kwa risasi, ukiagwa..."
 
...ETHICAL case....anayejua tatizo ni Ufoo mwenyewe, sie tutabaki kupiga TARARIRAAAA ili mradi genge lichangamkeee....hata atakapokuja kuueleza uma yaliyojiri hatasema yote...Kila mtu ana yake moyoni (hata ninavyoandika nina yangu moyoni na hakuna hata mahali nimeshawahi vujisha even kwa rafiki zangu wa karibu (intimate/close friend(s))...

FIKIRI yako na Si ya mwenzio

View attachment 117219

Hivi inatakiwa UFOO aueleze Umma au polisi wafanye uchunguzi wa kifo. Ninashangaa sana nchi hii inavyoendesha mambo kienyeji, Ufoo alitakiwa awe chini ya ulinzi pale Muhimbili kama mtuhumiwa namba moja hadi itakapoonekana hana hatia. Kila mtu anarukia CONCLUSION kuwa Mushi aliua, alijiua, lakini hakuna mtu anayesema ana uthibitisho wa haya. Media ime manipulate hii issue in favor of mwandishi mwenzao Ufoo saro na kum victimize Mushi, very unfair
 
Waandishi wa siku hizi. Wameshatoa hukumu kabisa. Eti "alimuua mama yake Ufoo kwa risasi" . Mlikuwepo? Inasemekana, marehemu anakuwa accused to, ukweli bado.
 
aiodaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mwili wa marehemu Anthery Mushi aliyejiua kwa kujipiga risasi mwishoni mwa
wiki iliyopita, umekutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine
kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.

Risasi hizo zimebainika kufuatia
uchunguzi uliofanywa na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa
kushirikiana na maofisa wa Jeshi la Polisi.

Isaya Mushi, msemaji wa familia ya Mushi alisema mwili wa ndugu yao ulikutwa
na risasi hizo baada ya uchunguzi uliofanywa juzi.

Alisema hayo wakati wa
kuuaga mwili wa Mushi tayari kuusafirisha kwenda Kijiji cha Ongoma, Uru, mkoani
Kilimanjaro.

Wakati huo huo, mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
walijitokeza kwa wingi hospitalini hapo kuuaga mwili wa Anthery.

Mushi
aliendelea kufafanua kuwa hakuna mtu anayejua hasa kuhusu nini siri ya ugomvi
wao mpaka sasa, zaidi ya kufahamu kuwa ndugu yao alirudi kimya kimya, na kwenda
Uru mkoani Kilimanjaro kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam siku ya
Jumamosi.

Mushi alisema kuwa ulitokea ugomvi kati yake na mzazi mwenzie
na wakaamua kwenda kwa mama yake, Ufoo ili kuusuluhisha.

Alisema
kulitokea kutokuelewana kulikosababisha Anthery achukue maamuzi magumu ya
kumpiga risasi mkwe wake, Anastazia Saro na kumuua hapo hapo na kumpiga risasi
mbili mzazi mwenzie, Ufoo Saro na kisha kuchukua maamuzi magumu ya kujiua yeye
mwenyewe kwa kujipiga risasi.

Alisema tukio hilo limeleta mshtuko mkubwa
na simanzi katika familia yao, kwani Anthery alikuwa ni mtu mpole na mkimya
sana.

Ndugu wa mume waja na mapya

09:49

NA JESSICA KILEO
FAMILIA ya aliyekuwa mzazi mwenzake, Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, Anthery Mushi (40), imevunja ukimya na kudai inapata wakati mgumu kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe.

Imesema suala hilo inaliachia Jeshi la Polisi lishughulikie ili kubaini undani wake.

Kaka wa marehemu, Isaya Mushi alidai hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wawakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa.

Mushi alidai wapo katika wakati mgumu wa kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe, kwani haiwezekani mtu akajipiga risasi sehemu mbili ambazo ni kidevuni na upande wa bega la kushoto.

Alidai sio kazi yao kutoa hukumu, kwani wanasubiri upelelezi wa polisi kutoa jibu lililo sahihi kuhusiana na tukio hilo.

Baada ya kifo cha ndugu yetu, wanafamilia tulifanya uchunguzi wa awali na bado linatuwia vigumu kutambua upi ni ukweli kuhusu jambo hilo kuhusiana na kifo hiki,î alidai.

Kaka huyo alidai katika uchunguzi wa madaktari, walibaini kuwa marehemu alijipiga risasi mbili sehemu tofauti.

Akisoma risala kwa waombelezaji, Mushi alidai marehemu alizaliwa Januari 3, 1973 katika kijiji Uru Ongoma Timbirini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mushi alisema alisoma Shule ya Msingi Ongoma Timbirini kutoka mwaka 1981 hadi 1987 na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Zanzibar na baadaye alisoma kozi mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari.

Alisema mwaka 1994 alijunga na Kituo cha Televisheni cha ITV na mwaka 2002 alikwenda STR na hadi mauti inamkuta alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa, Sudan, akiwa mtaalamu wa habari.

Kwa upande wake, dada wa marehemu, Eviolatha Mushi alisema alipokea kwa masikitiko msiba wa mdogo wake kwa sababu alikuwa mtu mwelewa na msikivu katika jamii ambayo wamekulia.

Eviolatha alitoa wito kwa wanandoa kumshirikisha Mungu katika maisha yao na sio mwanadamu, hali itakayosaidia kutatua matatizo wanayopitia kwa kuwa neno la Mungu linasema kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke lazima atalamba mauti, hivyo hawana budi kukubaliana na neno hilo.

Naye, mdogo wa marehemu, Happy Mushi, alisema hadi sasa hawezi kuamini chochote hadi polisi itakapotoa majibu ya upelelezi .

Alisema Oktoba 9, mwaka huu, marehemu alimpigia simu na kumwambia anamshukuru Mungu, kwani ametoka kufanya kazi katika mazingira magumu, hivyo muda si mrefu anaweza kuhamia Tanzania, na kwamba yupo nchini kwa ajili ya kumalizia nyumba yake ambaye ipo Mbezi, Dar es Salaam.

Lakini cha kushangaza kabla ya wiki alisikia katika vyombo vya habari vikitangaza kaka yake amejiua mwenyewe pamoja na familia ya mke wake,î alisema.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda kijijini kwao Ongoma Timbirini na unatarajiwa kuzikwa leo.

Wakati huo huo, Ufoo aliyelazwa Muhimbili hali yake imetengemaa na ameanza kutembea pamoja na kwamba daktari anayemhudumia anakataza watu kuingia kumtazama.

Ofisa wa Habari wa MNH, Aminiel Eliegaisha, alisema jana kuwa, Ufoo anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya kutembea, ingawa bado hawajaanza kuwaruhusu watu kwenda kumtaza kwa sababu ameshonwa sehemu nyingi na kwamba wanahofia kidonda kutokupona haraka.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Oktoba 13, mwaka huu, eneo la Kimbamba nyumbani kwa wazazi wa Ufoo, ambapo alikwenda akiwa na mzazi mwenzake Anthery Mushi.

Mushi alimuua mama wa Ufoo kwa kumpiga risasi zinazosadikika tano na kumjeruhi kabla ya kujiua mwenyewe.


source: Uhuru Online
 
Hiyo mimba aliyonayo Ufo ni ya nani! Ndio beneficiary wa kadhia hii!

Eheeeeee lete habari. Kumbe ana mimba tena!!!!! Una unakika mkuu au ni maneno ya kusikia mitaani?
 
Jamani tuache lawama kwani ufoo siyupo yeye ndo mwenye ukweli tusubiri siku ya kuhojiwa atakalo sema ndo utakuwa ukweli
 
Bullet to the brain through the chin will never let any part of your muscle twist except the relaxation of iris, diaphragm and sphincters!!!!!! Correct me if m wrong!!!!!!

Unless he shot the shoulder first and then the chin!!!!!!

inachukua sekunde zisizopungua 3 paka 10 kama risasi imeingia sensitive area kama brain to make it cease functioning so majibu unayo mkuu.
Pili from the chin to the brain hapo kuikuta risasi kwenye ubongo tena kwa risasi ya bastola ni ngum kidogo mkuu sanasana iwe imepoison tu.nafikiri majibu unayo hapa mkuu
 
Tutasikia mengi sana kuhusu marehemu na the so called mchumba wake Ufoo for ten years.
 
Hivi inatakiwa UFOO aueleze Umma au polisi wafanye uchunguzi wa kifo. Ninashangaa sana nchi hii inavyoendesha mambo kienyeji, Ufoo alitakiwa awe chini ya ulinzi pale Muhimbili kama mtuhumiwa namba moja hadi itakapoonekana hana hatia. Kila mtu anarukia CONCLUSION kuwa Mushi aliua, alijiua, lakini hakuna mtu anayesema ana uthibitisho wa haya. Media ime manipulate hii issue in favor of mwandishi mwenzao Ufoo saro na kum victimize Mushi, very unfair



Hapo Kiukweli Umetazama Kwa Jicho La Tatu.
 
sijui kama tuna forensic examination, kama wanavyoonyesha kwenye investigation discovery kujua tukio lilikuwaje...angle of shooting, shooting range, impact of bullet n.k ingeweza kutoa clues za nani mkweli....lakini pia morive na mmiliki wa silaha iliyotumika pamoja na kuuwawa kwa mama ufoo kutasaidia kuondoa utata.
 
Nasikitika sana

Yule mtoto wa marehemu ataishi kwa namna ya simanzi kubwa sana na sijui atawachukuliaje wanawake

sad part ni shina la ugomvi kuwa mali za kupita tu... tulizaliwa uchi, tunazikwa na nguo ambazo si ajabu hatujachagua... na makaburi tunapangiwa pia

bad stuff Ufoo..... bad stuff,

DAMU YA MTU HAIENDI BURE

Sure thing, yetu yawe macho
 
Back
Top Bottom