Ndugu wa Ahmed Msangi: Maisha yetu Hatarini; Hemedi Katumiwa!

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Ndugu mmoja (jina kapuni kwa usalama wake), wa karibu wa bwana Ahmed Msangi , askari anayechukiwa kuliko kila askari hapa nchini kwa tuhuma za utekaji na mateso ya Dr. Stephen Ulimboka, amenukuliwa akilalamika kwamba ndugu yao ametolewa kafara na kuyaweka maisha yake hatarini wakati yeye alifanya kazi aliyotumwa na wakubwa.

"Ndugu yetu amechafuka sana jina kiasi kwamba anatembea kwa wasiwasi kila anakokwenda. hamedi hana amani na tunaona kama vile yeye alitumiwa wakati waliomtumia wamenyamaza na muda mwingine wanamfokea kwa kufanya uzembe. Sisi wenyewe tunafatwa na makachero wanaotuhoji maswali mengi wakati hata huko mabwepande hatukujui.

Hatujawahi kumiliki bunduki wala gari. Hatujui chochote na hatuna uhusiano na usalama wala polisi. Wasicdhanie watabakia milele kwenye madaraka. wataumbuliwa tu siku moja......chanzo, ndugu wa karibu wa bwana msangi

NB
Hatuwezi kuweka jinsia au anakoishi huyu mtu kwa usalama wake. Ila familia ya msangi inaishi kwa wasiwasi. Watu wanaosadikiwa kuwa usalama wanajaribu kutafuta ni habari gani wanazozijua (majina ya wakubwa) kuhusiana na utekaji wa Dr. Ulimboka.


 
Hapo ndo naiona habari ka ya kupikwa hii

tiss wanatafuta ni wakubwa gani wako nyuma ya sakata????...very interesting...kwa nini wasimuulize msangi??

Anachomaanisha mleta thread ni kuwa kama kuna mwanafamilia anajua jina la mkubwa kwenye hili tukio basi "Hemed" atakuwa amevujisha siri kwa kujua ama bahati mbaya........Kinachofuata ni "silence" ili habari "mpya" zisitapakae.
 
Kwani unadhani hao tiss wameshindwa kwenda kwa ulimboka alikolazwa wakamuhoji mpaka wawaulize wajombazake?
 
Duh kumbe ndo huyu,alikuwa boss Moro kipindi wadogo zetu wanagoma goma pale SUA akawa anawahoji,duh umeharibu mkuu nilikuona wa maana sana ulipowaachia kina Davi,Peter na Bertha ila kwa hili sikusamehi.Let u harvest from what you planted.
 
"ndugu yetu amechafuka sana jina kiasi kwamba anatembea kwa wasiwasi kila anakokwenda. hamedi hana amani na tunaona kama vile yeye alitumiwa wakati waliomtumia wamenyamaza na muda mwingine wanamfokea kwa kufanya uzembe.

Na yeye anabeba responsibility yakukubali kutumika. Alijua what he is getting himself into alipoamua kulamba viatu vya wakubwa. Roho alizozitesa na kudhulumu zitamfuata popote anapojificha. This is a joint responsibility. Lazima abebe huu mzigo hamna jinsi. Nawapa pole sana hao ndugu zake. Afterall nafurahi kusikia hata ndugu zake wanajua Hemedi ndio mtuhumiwa na sio Mkenya.
 
Back
Top Bottom