Ndoto niliyoota ni reflection ya utumbuaji wa Bosi wa Bandari na Mkurugenzi wa Jiji

kidole cha simba

JF-Expert Member
Jun 3, 2022
1,290
1,658
Habari za mchana wadau,

Basi bhana, jana nikiwa ndani ya treni kama kawaida nikielekea home. Basi bhana ghafla nikaskia taarifa ya habari kutoka Idhaa ya Kiswahili sauti ya Japan, nikaskia mtangazaji akisema "Dar-es Salaam, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametengua nafasi ya bosi wa bandari ya Dar-es-Salaam kwa ufisadi, tena mara, waziri mkuu wa tanzania ndugu Kassim Majaliwa amfukuza mkurugenzi wa jiji la Dar-es Salaam kwa tuhuma za upotevu wa shilingi za tz billion 10.

Du! Nilisikia kiu ya Konyagi ghafla wakati nilikuwa sina kiu kabisa ya hiyo ki2 jamaa, basi niliposhuka nikaenda sehemu wanachoma asua za mbuzi, nikashushia na ile Konyagi, then nikaelekea home huku nikiwaza mambo mengi kama kachumbari. Aaaah! Nilivofika sikuoga kwani baridi ilikuwa kali sana, nikaingia kwenye neti nikauchapa.

Mara nikaanza kuota ndoto jamaa yangu aisee, ndoto ya kwanza nikaota jamaa kama 8 ivi wana vichwa vikubwa na vitambi wakidiscuss namna ya kumrudishia mzee Mbowe eneo lake lilikuwa na Bilikanas kasino pamoja na lile shamba lake la Hai. He! Ghafla wale jamaa waliokuwa wakiitwa "papaa" na wengine walikuwa wakiitwa watoto wa mbuzi wakitoka walipokua wapo na kuanza kula bata maeneo ya Sinza, Kinondoni na Tabata huku wakimwaga minoti kila mahali.

Nikiwa naendelea kupata, ghafla akatokea jamaa mmoko amevaa suti ya bluu ya mikono mifupi akinisogelea kwa speed ya ajabu na kunifokea "Unanijua mimi nani?" Nikaamka ghafla usingizini kwa uoga mkuu, nikamshukuru Mungu kumbe ilikuwa ndoto!

Bye mazee
 
Back
Top Bottom