Ndoa za siku hizi: Kuzimu kumesimamia ukucha

Ndoa za siku hizi: Kuzimu kumesimamia ukucha

hicho kipindi hichi yani ni hatari na wengi ndoa zao hufia hapo ,.. walinzi wa ndoa wanawake wameamua kuwa ni kujiweka vizuri kimwonekano likitokea la kutokea basi ajisepee akiwa na hali nzuri anaweza pata mwingine ... tukasahahu kuweka vizuri nyumba zetu tutafute amani na watu wote na amani haiji kirahisi rahisi ni mapamabano.. upendo furaha vyote hivi vinahitaji kujitoa na kusimama hasa .... ila sasa tumegeuka wakaguzi kutafuta ubaya kila dakika ipitayo kuviziana viziana kutafuta ubaya tu na unajua ubaya ukiuona jua amani hiyo inapotea ikifuatiwa na upendo na furaha mnabakiwa na chuki na vurugu .... tujitahidi kwa kweli ni ngumu na ndiyo maaana lazima kupambana simama kijeshi jeshi lazima uwe mshindi na usikubali kushindwa..... yani pamabana kiasi kwamaba hata kama anamichepuko anaona kabisa hakuna nafasi hiyo ndania anarudisha majeshi ndani ...
kuwa mlinzi wa nyumba yako acha kuwa mchungaji binadamu hachungwi analindwa ..

Kuwa Mlinzi wa ndoa yako,asante sana Miss Chagga kwa ujumbe mzuri kwa wake zetu.

Ukweli mimi kama mume na kama Baba najitahidi niwezavyo kuipenda familia yangu,kuwa karibu sana na mke wangu kipenzi,bila kumsahahu Mungu katika yote tufanyayo.Na nguzo kubwa kuliko zote ni kuomba pamoja na mwenza wako mkiwa mmeshikana mikono mkiomba Mungu kamwe awaweke pamoja na asitokee wa kuwatenganisha.Ndo kitu cha kwanza nafanya kila asubuhi kabla ya kwenda kazini na kila nirudipo.
 
asante mkuu na me ngoja nianze uutaratibu wa kufanya maombi
 
Hicho kipindi cha miaka 3,5,nilikoma ubishi,kwani nilikuwa na mtoto nje na nilificha ilipokuja kufahamika amani ilipotea kabisa,tuliishi kama mabondia mpaka nilihisi ndio fomla yenyewe,nilikuwa kutoka kwenye hizi changamoto baada ya miaka 6 hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika kufuatilia mambo ambayo kaka mshana jr umekuwa unatufahamisha hapa jf nimejikuta kutamani kuonana nawe maana una upeo mkubwa katika mambo mengi. shetani ndio baba wa zinaa na uzinzi hawezi kukukabali kuona ndoa takatifu zinakuwepo maana ndoa takatifu ndio dawa ya uasherati na uzinzi na pasipokuwa na ndoa takatifu basi uzinzi na uasherati unatamalaki.
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wake zetu hatuwapigi mashine vizuri that's why migogoro inaongezeka na tamaa za michepuko zinakuja...kama wewe ni mwanandoa hakikisha huamki kwenda kazini hali ukiwa na nyege ...ladies and gentlemen lets make effective use of our spouses kama tunataka kushinda vishawishi ndoa hoiyee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ndoa tu hata haya mahusiano ya kawaida ie uchumba, uchepuko sijui urafiki n.k shetani yu spidi hatari.
Ee mungu epushia mbali [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]

Mahondaw wa Smart911
 
Bado tuko kwenye majonzi ya kumpoteza mwanajf mwenzetu aliyefariki Riverside kwa ajali ya pikipiki siku chache kabla ya ndoa yake
Matukio ya namna hii ni mengi na si haba kila mmoja wetu hapa anaweza kuwa na story yake
Hata huku mitandaoni andika kitu cha kijinga kinaweza pata wachangiaji wazuri mpaka ukashangaa lakini weka tangazo la kutafuta mwenza uone!
Mungu akikusaidia ukavuka salama hiki kizingiti cha harusi, bado hauko salama! Miaka 3-5 ya kwanza bado utatafutwa tuu, michepuko, ishu za kukosa mtoto au kuzaa watoto wa jinsia moja tu... Ama la maisha kuanguka ghafla.... Kugundua tabia zilizofichika za mwenza wako, visa vya mawifi mama mkwe, ndugu wa mwenza wako nk nk! Vyote hivi ni vita mwanzoni mwa ndoa
Ukifanikiwa kuvuka miaka hiyo salama basi ndoa yako huanza kutengemaa baada ya miaka hiyo LAKINI usijisahau wala kubweteka!!! Ndoa ni jambo la kheri na ni utume wa Mwenyezi Mungu shetani hapendi, hivyo huwa na vita ya kudumu... Kumbuka hili pia, sometimes huja kinyume.... Miaka ya mwanzo huwa ya furaha maelewano na mafanikio sana halafu baada ya hapo changamoto huanza
Yote juu ya yote kuna kipindi cha kujaribiwa katika ndoa kuwa makini sana katika kipindi hicho na usimame imara hasa!
NB: mnapofunga mlango wa chumbani mkalala kwa amani juweni mko wawili, Mungu akiwa katikati yenu... Lakini ikitokea kutoelewana juweni shetani ndio kasimamia ukucha
.
Hebu kesho tuendeleee kukipambazuka

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuuuuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya mwanzo huwa ya furaha maelewano na mafanikio sana halafu baada ya hapo changamoto huanza. Yote juu ya yote kuna kipindi cha kujaribiwa katika ndoa kuwa makini sana katika kipindi hicho na usimame imara hasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka ujue nakuelewa zaidi ya kukuelewa
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom