Ndoa za siku hizi: Kuzimu kumesimamia ukucha

Ndoa za siku hizi: Kuzimu kumesimamia ukucha

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,207
Reaction score
866,466
Bado tuko kwenye majonzi ya kumpoteza mwana JF mwenzetu aliyefariki Riverside kwa ajali ya pikipiki siku chache kabla ya ndoa yake.

Matukio ya namna hii ni mengi na si haba kila mmoja wetu hapa anaweza kuwa na story yake, hata huku mitandaoni andika kitu cha kijinga kinaweza pata wachangiaji wazuri mpaka ukashangaa lakini weka tangazo la kutafuta mwenza uone!

Mungu akikusaidia ukavuka salama hiki kizingiti cha harusi, bado hauko salama. Miaka 3-5 ya kwanza bado utatafutwa tuu, michepuko, ishu za kukosa mtoto au kuzaa watoto wa jinsia moja tu, ama la maisha kuanguka ghafla.

Kugundua tabia zilizofichika za mwenza wako, visa vya mawifi mama mkwe, ndugu wa mwenza wako nk nk! Vyote hivi ni vita mwanzoni mwa ndoa,
ukifanikiwa kuvuka miaka hiyo salama basi ndoa yako huanza kutengemaa baada ya miaka hiyo lakini usijisahau wala kubweteka.

Ndoa ni jambo la kheri na ni utume wa Mwenyezi Mungu shetani hapendi, hivyo huwa na vita ya kudumu. Kumbuka hili pia, sometimes huja kinyume.

Miaka ya mwanzo huwa ya furaha maelewano na mafanikio sana halafu baada ya hapo changamoto huanza. Yote juu ya yote kuna kipindi cha kujaribiwa katika ndoa kuwa makini sana katika kipindi hicho na usimame imara hasa.

NB: Mnapofunga mlango wa chumbani mkalala kwa amani juweni mko wawili, Mungu akiwa katikati yenu lakini ikitokea kutoelewana juweni shetani ndio kasimamia ukucha.

Hebu kesho tuendeleee kukipambazuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kaka mshana wanaokuchukia na kukutishia wanakuchukia bure ndugu. huwa unaongea ukweli sema ukweli wako ndo unachukiwa sana. umesema vyema, kuna teja mmoja alisema ukiona unagombana na mkeo sana ujue jini lipo ndani.
 
[emoji115] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa sikuhizi zimekua mwiba na chanzo kikubwa niwatu kutomjua mungu,kwahiyo dhoruba kidogo hutosha kudondosha ndoa husika,sasa Ndugu waisakame,michepuko waisakame na bado shetani aisakame na mbaya zaidi Uwe uliolewa au kuoa kwa kuogopa maneno au watu hapawezi ndoa kudumu,nakua chana tayari nikuleteana DOA kwenye maisha
Tusiingie ndoani mpaka tuonapo niwakati sahihi
Mwenza sahihi
Na moyoni kuna amani ya kimungu juu ya ndoa hiyo
Katika yoote ukiingia ndoani jua umetangaza vita na maadui,mshike sana mungu ili safari iwe salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli umeongewa. Tena nimekuelewa zaidi.
Ila Mshana, unatutisha sisi ambao hatujaingia Ndoani.
Siku nyingine uje na Uzi wa kututia Moyo maana wengine ndo tunajiandaa kuingia.
Ubarikiwe kwa mada nzuri ya asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
Asante Mshana.Ni zaidi ya miaka kumi sasa Niko kwenye ndoa.I love my wife.Lakini tulipitia kipindi kigumu kidogo hapo nyuma. Majaribu yamepita na maisha ni mazuri.Wale wenye wito wa ndoa waoe, wasiogope.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro acha nitakutafuta inbox. Maana imebid nicheke tu,

Hapo kuna vita mnoo
Shetani hapend watu waoe vzr au waolewe vzr

Sababu Mungu aliumba mke na mume hakuumba dada na kaka

Shetan akiweza kuvuruga ndoa au kukufanya usioe vzr au usiolewe vzr
Inakuwa ni ushindi kwake

Lakin ukiweza oa vzr na kuolewa vzr utaishi paradiso dunian haa sababu mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa

Huyo mdada kufiwa na mchumba Mungu ampe nguvu tu

Ulimwengu wa roho una vitu vingi mno

Watu waombe mapema
Kuna mdada alipata wanaume wa 5 kila mtu anataka kumuoa, ikabid aombe kumuuliza Mungu ni yupi
Na akashirikisha na watumishi
jibu linakuja hata mmoja hakuna aliyeletwa na Mungu.

In ua Presence Jesus is where I belong
 
Asante dada, unajua kuna mapigo saba ya ndoa, ukiweza kuyashinda yote Utakuwa na mahusiano yenye furaha sana, na haya mapigo yanaweza kuja kwa kutangulizana, kufuatana ama kinyume nyume
Baadhi ni haya
Marafiki/mitandao ya kijamii
Ufukara
Mafanikio ya ghafla
Starehe
Uongo/tabia zilizojificha
Uaminifu na
Imani za kishirikina
Bro acha nitakutafuta inbox. Maana imebid nicheke tu,

Hapo kuna vita mnoo
Shetani hapend watu waoe vzr au waolewe vzr

Sababu Mungu aliumba mke na mume hakuumba dada na kaka

Shetan akiweza kuvuruga ndoa au kukufanya usioe vzr au usiolewe vzr
Inakuwa ni ushindi kwake

Lakin ukiweza oa vzr na kuolewa vzr utaishi paradiso dunian haa sababu mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa

Huyo mdada kufiwa na mchumba Mungu ampe nguvu tu

Ulimwengu wa roho una vitu vingi mno

Watu waombe mapema
Kuna mdada alipata wanaume wa 5 kila mtu anataka kumuoa, ikabid aombe kumuuliza Mungu ni yupi
Na akashirikisha na watumishi
jibu linakuja hata mmoja hakuna aliyeletwa na Mungu.

In ua Presence Jesus is where I belong

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hicho kipindi hichi yani ni hatari na wengi ndoa zao hufia hapo ,.. walinzi wa ndoa wanawake wameamua kuwa ni kujiweka vizuri kimwonekano likitokea la kutokea basi ajisepee akiwa na hali nzuri anaweza pata mwingine ... tukasahahu kuweka vizuri nyumba zetu tutafute amani na watu wote na amani haiji kirahisi rahisi ni mapamabano.. upendo furaha vyote hivi vinahitaji kujitoa na kusimama hasa .... ila sasa tumegeuka wakaguzi kutafuta ubaya kila dakika ipitayo kuviziana viziana kutafuta ubaya tu na unajua ubaya ukiuona jua amani hiyo inapotea ikifuatiwa na upendo na furaha mnabakiwa na chuki na vurugu .... tujitahidi kwa kweli ni ngumu na ndiyo maaana lazima kupambana simama kijeshi jeshi lazima uwe mshindi na usikubali kushindwa..... yani pamabana kiasi kwamaba hata kama anamichepuko anaona kabisa hakuna nafasi hiyo ndania anarudisha majeshi ndani ...
kuwa mlinzi wa nyumba yako acha kuwa mchungaji binadamu hachungwi analindwa ..
 
Ndo ni taasisi tena kubwa na ina idara nyingi hivyo huwezi kuimudu kwa kutumia kichwa chako tu.
MUNGU asipohusishwa taasisi hii inapata uongozi usio imara na usio wa maono unaojali mambo ya mwili tu.
Tunahitaji upendo wa dhati pamoja na msaada wa MUNGU ili tufurahie ndoa zetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom