Ndoa Yangu

Ndoa Yangu

SEHEMU YA 18

Siku hiyo ndiyo niligundua kwa mara ya kwanza kuwa kumbe mke wangu naye ni fundi kwenye uwanja wa seremala. Alinikatikia viuno kama mwali wa kimakonde huku akinililia kwa sauti za kumtoa nyoka pembeni. Hakika alinifanya nifurahie mapenzi kwa mara ya kwanza. Alinionesha utamu wa ndani kabisa wa mapenzi. Alinikwangulia nyama ya kifuu Atu na kujikwangua kimkuno nazi.
Siku hiyo nilipanda na kushuka vilima vinne pasipo kulala kuanzia hiyo saa sita hadi saa kumi alfajiri. Mchoko na uchovu ulinifanya nilale hoi. Uso ukiwa umetabasamu, akili ikiwa imefuta tukio la udhia na kujengeka mahaba niue ya Atu huku nafsi ikitakata kwa furaha ya utamu wa Atu ambao siku hiyo ndio niliujua vizuri.
Kitu ambacho sikukijua muda huo kumbe vichwa vitu vilikuwa na mawazo tofauti kabisa. Kipindi mimi nikiwaza kumfanyia mazuri mke wangu huku nikijihimiza kumtengenezea kila aina ya faraja ikiwa kama kuna sehemu nakosea nijirekebishe, kumbe mwenzangu alikuwa anafikiria kunikimbia kabisa.
Tulilala wote huku tukikumbatiana na nikajiachia nikiuacha usingizi uliobebwa na mchoko kunipitia. Atuganile hakulala wala hakusinzia zaidi alikuwa makini kunitaza na kuchunguza pumzi zangu. Aliporidhika kuwa sasa nimelala tena nipo katikati ya usingizi fofofo ikiwa kulikuwa kunakaribia kucha. Alijiengua kwangu taratibu na sijui kama alienda kuoga ama laah! zaidi alijiandaa na kuvaa nguo nzuri zaidi za mitoko sambamba na viatu nilivyowahi mnunulia vya gharama kuliko hata kiatu alichokivaa siku ya harusi. Alinyata na kutoka nikiwa sina lile wala hili. Usingizi ulionichukua kichovuchovu ulikuja kuniachia saa mbili asubuhi. Niligeuka kitandani kumtazama mke wangu sijamuona. Nilijigeuza bila hofu wala mashaka nikaendelea kuvuta shuka nikiamini atakuwa kaenda msalani. Lakini kilichokuja nistua baadae ukimya kutawala muda mwingi. Nilinyanyuka kitandani na kukuta kabati la nguo likiwa wazi. Nilinyanyuka na kupiga hatua kulielekea ndipo niligundua kuwa nguo zimetimka tofauti na mpangilio wake. Nilitazama nyuma ya mlango niliiona ndoo yetu ya kuogea hata mataulo yote yalikuwepo. Mh! niliguna na kutazama mlango ulikuwa umerudishiwa kidogo tu. Nilitoka nje hakukuwa na mke wangu, si jikoni si chooni. Nikarudi tena ndani huku wasiwasi ukinibishia hodi kwa mara nyengine kichwani mwangu na mapigo ya moyo kuanza badili kasi.
Nilikaa sofani nikifikiria na kumsubiri mke wangu pasi dalili ya urejeo wake. Hapo ndipo nikakata shauri na kujua kama hajaenda dukani kwa mpemba basi atakuwa kwa yule mama powa.
Nilitoka nikiwa na ghadhabu iliyokataa kufichika hadi kwa mama Powa lakini nilikuta geti lake dogo la mlangoni limefungwa. Ilionesha kila dalili hakukuwa na mtu ndani hata nilipoita ukimya tu ulitanda.
Nikasonga mbele hadi dukani kwa Mangi sikumuona pia nilishindwa kumuuliza yeyote. Nikajipa tumaini huenda tumepishana karudi nyumbani. Huyooo! nikarudi tena nyumbani hayupo.
"Hamjambo watoto wazuri eeh! eti mlimuona shemeji yenu kapita hapa? yule mke wangu mzurizuri?" Ilibidi sasa niwaulize watoto waliokuwa wanacheza kwenye kibalaza cha nyumba ya jirani kabisa na uchchoro wa nyumba yetu.
Watoto wale wa makamo walimtambua mke wangu na kila nilivyopita naye siku za nyuma tukiwakuta wanacheza pale waliacha hata kucheza wakitushangaa.
"Mimi sijamuona." Mmoja alijibu.
"Mimi nilimuona amepita kaelekea huku amependeza sana leo."
Jibu la mtoto wa pili lilinifanya nimuulize mara mbilimbili lakini hakuwa na jibu la ziada zaidi ya vile alivyonambia.
Haraka niliingia ndani na hapo ndipo macho yalinitoka nilipogundua sehemu tunayoweka viatu hakuna vile viatu ghali vya mke wangu.
"Shiit!" Nilichukua simu yangu na kumpigia mama haraka.
"Mama..mamaa mke wangu amefika huko?" Niliuliza huku nikiwa nazunguka zunguka ndani baada ya kumpigia simu mama.
"Mkeo? mbona tokea uje naye hakuja tena. Vipi kwani?!!" Aliniuliza mama kwa sauti iliyojaa mshtuko na mshangao.
"Mama Atu hayupo nahisi ametoroka."
"Ametoroka? kwani mligombana? Hee!!"
Nilishindwa kumjibu kitu mama na haraka nilichomoka nyumbani nikikumbuka kufunga mlango na kuchukua waleti yangu huku nikisahau hata kupiga mswaki achilia mbali kuoga. Kwenye waleti nilikuwa na shilingi elfu kumi na saba tu. Trakisuti niliyovaa usiku ndiyo niliyotoka nayo huku juu nikiwa nimevaa shati, miguuni kandambili.
Mawazo yalinituma Atu atakuwa amekimbilia Ubungo kituo kikuu cha mabasi ya mikoani. Nilikodi pikipiki ili nimuwahi huku nikimsihi dereva aendeeshe kwa kasi. Tulinusurika ajali si chini ya mara mbili katika safari hiyo. Tulipofika tu Ubungo baada ya kumpa pesa yake dereva bodaboda nilijikuta navuka pasipo umakini na kutokea chupuchupu kugongwa na magari achilia mbali pikipiki zilizokuwa zikinikwepa.
"Kum***aako utakufa mseeeeng**wee" Nilishushiwa matusi na vijana wa stendi.
Machoni nilionekana kama chizi. Ama nusu mwizi. Yaani leo mimi natazamwa vibaya na kutukanwa kwa sababu ya mtu niliyempenda na Hawakujua mwenzao nipo katikati ya kiza cha mapenzi. Nimependae anatumia udhaifu wangu kuniadhibu. Nilitazama lakini nilihisi kutooona vizuri ingawa sijapotea njia.
"ATUGANILE...ATUGANILE...MKE WANGU..!"
Sauti hii iliita kwa maumivu moyoni mwangu kadili nilivyopiga hatua na kumkodolea kila binti niliyepishana naye kituoni. Niliingia kwenye mabasi tofauti tofauti nikipita siti baada ya siti kumtafuta mke wangu. Kila basi nililoona limeandikwa Mbeya ama Kyela ambalo lilikuwa kituoni muda huo, niliingia ndani yake pasipo kusema kitu na yoyote nikimtafuta mke wangu.
Nilijua yeye ndiye nuru yangu. Tulizo la moyo wangu. Ndio maana nikafunga naye pingu. Aaaah! Atu kwanini anikimbie? Mimi ndie mumewe si bwana wala hawala. Mume hakimbiwi Atuganile aaaah... Niliumia na kujikuta machozi yakivuja pasipo kujitambua. Watu walinishangaa hususani abiria na makonda wakashindwa nielewa ni mzima ama zimeniruka.
"Mmh! huyu kaka atakuwa mwizi tu kama sio chizi!" sauti ya binti mmoja niliisikia pindi nilipokuwa nashuka kwenye basi moja wapo a Mbeya ambalo lilikuwa ndio linaondoka. Muda tayari uliyoyoma. Mabasi mengi yalitoka asubuhi sana na yale niliyoyakuta yalikuwa machache tu!
"Ina maana Atu wangu ndio ameenda?" Nilijiuliza na kusogea pembeni ambapo nilijikaza na kupiga simu namba ya mamaake.
"Hallow mama shikamoo." Nilisalimia baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
Sauti ya mamamkwe ilionesha hali ya uchangamfu tu.
"Samahani mama jana ulichati na mke wangu amekwambia nini mama?"
Nilimuuliza na kumshangaza. Kwa mara ya kwanza namuuliza mama mkwe habari zangu na mke wangu ihali sikuwa na mazoea hayo.
"Mh! mbona unanitisha baba! vipi kwema huko?"
Nilipata kigugumizi kumjibu haraka mama Atu swali lake na kujikuta namuuliza tena.
"Kwani mama mke wangu hajakupigia simu?"
"Hajanipigia ndio One mwanangu hebu nambie mmegombana ama nini kimetokea?"
"Hapana mama! mke wangu ametoka asubuhi hii na sijui alipoelekea na ndio nipo katika jitihada za kumtafuta."
"Mungu wangu." Sauti ya mama mkwe ilihamanika simuni na ndipo nilipokata simu huku nikichoka zaidi.
Nilihisi dunia nimeibeba kichwani kwa maswali juu ya sababu kuu ya mke wangu kunitoroka ihali kilichotokea jana yake kiliisha na wala sijampiga hata tulilala kwa amani na kunipa mapenzi motomoto.! Ina maana ilikuwa danganyia toto kumbe moyoni mwake alikuwa na mpango tofauti? au ndio ametimiza ahadi ya ule ujumbe kuwa asikose? Ooooooooh! jamani hata miezi mitatu ya Ndoa Yangu bado? chozi la maumivu na mateso kwenye ndoa yangu kama lilikuwa kusudio langu basi niko radhi kuadhibiwa kwa mateso makali zaidi....Lakini endapo sivyo! basi chozi hili utalilipa Atuganile.
 
SEHEMU YA 19

Nilitoka kituo cha mabasi ubungo huku nikiwa sijui nielekee wapi mara simu yangu iliita. Mama alinipigia akinisisitiza pamoja na dada zangu kuwa niende. Sikuwa na jinsi nilienda kwa mama huku nikiwa mwingi wa huzuni. Muonekano wangu hakika uliwahuzunisha sana ndugu zangu. Mama alishindwa kujizuia na kudondosha chozi pindi aliponikumbatia kwa kunifariji na kunipa maneno ya kuleta matumaini.
"Usichanganyikiwe baba, wewe ni mwanaume hebu kaa kwanza." Alinipa maneno ya ujasiri mama wakati huo dadaangu mmoja aliniandalia chai. Hata wajomba zangu watoto wa dada zangu waliponiona walihuzunika na kupooza kuniona nikiwa katika hali ile ya huzuni. Ingawa walikuwa watoto lakini walipata hisia kwa kile wakionacho. Kawaida yangu nilikuwa nakuja nimependeza tena wakinoiona walinikimbilia na kuwakumbatia huku nikiwabebea zawadi kama pipi na biskuti. Lakini haikuwa siku hii. Siku niliyokuja kama mkimbizi aliyenusurika vitani.
"Mama! nini kimemkuta mke wangu jamani?" niliuliza huku nikishindwa kizuia kilio kwa kumbukumbu nyingi zilizotawala kichwa changu. Si rahisi kwa binti kama Atuganile aliyeonesha kila aina ya tabia nzuri eti aje amtende mumewe kwa namna hii kwa makusudi kabisa? Hapana hii haikuniingia akilini. Kichwa changu kiliham,ia kwenye imani za kishirikina tu. Nilihisi huenda Atuganile amefanyiwa kipayupayu.
"Kwani ilikuwaje mwanangu hebu tuhadithie mbona hatukuwa kusikia kama mna matatizo eeh! mmeoana juzi tu hata kama mtu ana tabia zake mbaya lakini kwanza angeficha makucha walau mwaka upite." Alisema mama huku dadan zangu wakiunga mkono kauli ile. Nilitamani ningekuwa na kaka mkubwa ningemwambia kila kitu. Lakini ilibidi niongee hali halisi iliyotokea hususani tukio la jana yake tu huku nikiongopa kwa kuficha matukio mengine ya nyuma.
"Mh! ina maana alivyoondoka amejiandaa?"
"Ndio mama, tena amevaa nguo za mtoko kabisa kuna watoto wamemuona amependeza sana na hata nilivyocheki ndani amechagua vile viatu vizuri zaidi ingawa hakubeba begi lolote la nguo."
"Mh! kama kipayupayu nijuavyo mtu hakumbuki chochote hata kuvaa nguo nzuri zaidi mtu anaondoka tu na kutokomea." Alisema mama huku kauli yake ikiungwa mkono na dadaangu mmoja na kudakia.
"Kweli kabisa mama! yaani ulivyokuja kaka One ndiye kama umepigwa kipayupayu. Huyo atakuwa ameondoka akiwa na akili zake timamu kakaangu hata usichanganyikiwe na kuumiza kichwa. Kwanza namba ya huyo mwanaume si unayo?" Aliniuliza dada nami nikamjibu kwa kichwa kumkubalia huku nikiitoa simu yangu mfukoni.
"Sasa nipe mimi hiyo namba kama huyo Atu amekimbilia huko tutajua hapahapa lool!"
Nikampa dada namba ya jamaa niliyoichukua jana usiku ambaye ndiye alikuwa anachati na mke wangu. Alichokifanya dada ni kunivutia ndani na kuipiga ile namba huku akibadili sauti kuilegeza na kujifafanya yeye ni rafiki wa Atuganile.
"Hallow shemeji mambo." Alianza kwa kusalimu kumtega huku nikiwa nimetuli kusikiliza.
"Nani mwenzangu?" sauti iliuliza upande wa pili.
"Jamani shem acha utani ina maana kutumia namba nyengine ndio sauti yangu ishabadilika? best ake Atuganile wa shule bwana."
"Anhaa nambie shem kitambo sana."
"Kweli meji, vipi Atu uko nae nini maana napiga namba yake siipati hapa tokea jana usiku."
"Daah! wee shem kwanza huyo rafikiako ndo sitaki msikia kabisa hata hilo jina nahisi linazidi kuukera moyo wangu!"
"Kwanini jamani shemeji?"
"Ina maana unajifanya na wewe hujui kitu?"
"Sio najifanya shem sijui hiko unachokizungumza unanitisha jamani nini tena kimetokea?"
"Atu mi nashindwa kumuelewa hadi sasa huko kwa mjombaake anasoma ama anashinda kwa wanaume, tena sio kushinda tu bali analala kwa wanaume. Nahisi ni uongo mtupu anavyonambia anatafuta chuo huko. Shemeji jana sikulala nimeumia sana, Atu si wa kunidanganya kiasi kile akumbuke wapi tumetoka. Nashindwa kuamini kabisa yaani sitaki hata kumsikia niliyomfanyia yote namuachia Mungu. Ila akae akumbuke hakuna mwanaume dunia hii atakuwa na moyo kama mimi kukaa na mwanamke pasipo kumuharibu tena akimsomesha kwa gharama zake kabla hata ya kumuoa. Ni uaminifu kiasi gani nilimuonesha Atuganilee eeeh! Shem kumbuka tokea Mbeya huku hadi anafeli nimetoa shilingi ngapi mimi kujazia pesa za ada baada ya kunambia mjombaake amejitolea mchango wa kumtafutia shule huko Morogoro? pesa ngapi nilikuwa namtumia kila mwisho wa wiki? Hivi kuna mwanaume wa karne hii kufanya yote hayo kwa mtu ambaye hata hajamuoa? Shem kuhusu mimi na Atuganile nadhani hapa imetosha kabisa. Asije kuniua tu! ila mwambie akikupigia kuwa aje kuchukua nguo zake hapa na hata mamaake nishamtumia meseji."
Jamaa alilalama kwenye simu hadi sauti ikabadilika na kilio kumponyoka katikati ya lalamiko lake na majuto ya nafsi. Hapo ndipo nilipochoka na kuhisi kizunguzungu.
Sikumbuki zaidi nini kilitokea zaidi ya kuja kustuka na kukuta nimezungukwa na watu chumbani huku dada zangu wakinipepea na mama akilia kwa machungu amechanganyikiwa.
"Onesmo mwanangu kwanini unataka kuniua mamaako jamaniii! eeeh Mungu kakosa nini mwana huyu? maaaaa wee Atuganile kumbe ulikuwa umetuvalia ngozi ya kondoo lakini ndani chui? pole baba ila hilo sio jambo geni duniani wala wewe si wa kwanza kufanyiwa hivyo..Usichanganyikiwe mwanangu." Alinifariji mama. Nikainuka baada ya kuhisi fahamu zangu zimekaa sawa ingawa kichwa bado nilikuwa nakihisi kuuma.
Kwa mara ya kwanza nilimchukia Atuganile siku hiyo.
"Kumbe kuna mtu mwengine anamsomesha? Eti huku kwangu anasema ni kwa mjombaake! Mimi kweli ni mjombaake? Aaaah! mke wangu hata kama ni uongo lakini sio kihivi! Ina maana hasemi ukweli kama yeye ni mke wa mtu? Tena ndoa yetu haikufungwa kwa siri bali ni dhahiri kabisa?" Nilijiuliza maswali kedekede kwa muda mfupi huku kichwa kikikubali ila moyo ukikataa na pale moyo unapokubali kichwa kilikataa. Nilikaa kwa mama mpaka mchana wakati huo dadaangu akiendeleza upekupeku kwa yule jamaa ambaye naweza kuthubutu kusema ni mtendwa mwenzangu ingawa mimi nilizidi ilikuwa si kutendwa tu bali ni kutendwa janga. Majirani walikuja kujua kulikoni hususani waliposikia muda ule walipoisikia sauti ya mama akilia na kunung'unika. Hakika kila aliyeambiwa aliachama kinywa na kutoamini kama huyo binti niliyemuoa tena yule waliomtambua wao ndie amenifanya hivyo! eti amenitoroka? tena imethibitika kuna mwanaume mwengine naye alikuwa anamuhudumia? Ilikuwa ngumu kuamini.
Penye wengi pana mengi. Alifika shemeji yangu mmoja ambae alizaa na dadaangu mmoja ingawa hajamuoa lakini tulishamzoea hivyo. Huyo ndie alikuwa na mtoto ambae nilipanga nimsomeshe baada ya kufeli darasa la saba.
Alinivutia pembeni na kuanza kunipa maneno mbalimbali ikiwemo ya kufariji na jinsi ya kuishi na wanawake.
"One shemeji angu, wanawake ni wazuri tu kama utawaweka kichwani mwako na kuwachukulia kwa kuwasoma kuwa wana mapungufu makubwa katika fikra. Ukiamini hilo hakika huwezi kumchukia mwanamke wala kugombana nae pia hatoweza kukuumiza maisha yote hata itokee aondoke ghafla. Lakini kama ukiishi na mwanamke ukamuweka akilini kuwa kichwa chake kinafanya kazi katika fikra sahihi kwa asilimia mia hakika utaumia sana. Ubongo wao siku zote kama wa mtoto mdogo ingawa wana akili timamu lakini si katika kufikiri kwa harka. Fokasi yao iko chini sana. Kitu ambacho unaweza kukifikiria mwanaume na kukipatia jibu sahihi ndani ya masaa matano, basi kwa mwanamke kitu hiko anapaswa akifikirie ndani ya siku tano ndipo atapata jibu sahihi pasipo kuchanganya kitu cha ziada juu yake. Usiumie wala usioneshe udhaifu shemeji. Sisi ni wanaume tumeumbwa kuwa majasiri. Maumivu yetu yanaishia ndani kwa ndani wala si watu wa kuchanganyikiwa ovyo. Nakuhakikishia mkeo atarudi tu tena unaweza fikiria kaenda mbali lakini kumbe yuko jirani tu anasikilizia utachukua uamuzi gani kama siku akiondoka. Je, utamtafuta? pengine si kwamba hakupendi! hapana yule binti anazo ishara zote za upendo kwako, ila kuna kitu cha iada kipo nyuma ya maisha yake inapaswa utulize akili wewe ndie wa kumsaidia One. Kumbuka tayari yule mkeo na ndoa zetu wakristo hazivunjiki mngali hai. Huo ni muunganiko wa maisha hata naye anajua hilo. Mpaka amekubali kuolewa nawe jua kuna kitu cha zaidi amekipenda kwako kuliko hao wanaume wengine wote. Tuliza kichwa One ukichanganyikiwa wewe mama na dada zako wote watayumba na kuchanganyikiwa pia. Tuliza moyo wako..........."
Alinambia mambo mengi sana shemeji yangu huyu na kunifunulia mwanang mwengine. Na ndie yeye aliyenipa mbinu mpya ya kumpigia simu mamaake Atuganile akijifanya ni mkuu wa kituo cha polisi jijini Dar.
"Hallow! wewe ndiye mama Atuganile Mwakyusa?"
Aliigiza kwa sauti ya kipolisi shemeji baada ya kumpigia simu mamamkwe ambaye muda wote hakuonesha wasiwasi wa kuulkiza mara kwa mara tokea alivyostuka asubuhi nilipomwambia kuwa Atu hayupo. Alijibu mama mkwe huku nami nikisikiliza maongezi yao kujua shem atamwambiaje.
"Sasa unaongea na mpelelezi kutoa kituo kikuu Mabatini ambae nitaisimamia kesi ya kutoweka kwa binti ako endapo yatapita masaa ishirini na nne pasipo kurejea kwa mumewe ama kuonekana. Katika moja ya pelelezi nilizozianza awali kulingana na maongezi ya mumewe nimegundua wewe mama kuna kitu unakijua cha zaidi na utakuwa mshtakiwa namba mbili baada ya huyu namba moja mwenye namba 067506750675 ambae sauti yake imerekodiwa hapa kituoni akitoa maelezo pasipo kujua anaongea na kina nani! huyo ni kijana atayeeleza wapi alipo Atuganile ambae kwa sasa ni mke wa mtu. Maelezo yake yamekutaja zaidi ya mara moja na ameshakutumia ujumbe kuhusu kuumizwa na bintiyo lakini bado atabaki kuwa mkosaji sababu bintiyo ni mke wa mtu tayari. Sasa nakusihi sana mama chaguo ni lako kama umemficha bintiyo ama unajua alipo jua yakipita masaa ishiri na nne kufikia kesho saa tano asubuhi hatutakuwa na la ziada zaidi ya sheria kali kufata mkondo wake. Asante!"
Alikata simu shemeji na kunitazama huku akiwa ametabasamu na kunilazimisha nifarijike.
"Mkeo atarudi shemeji kama si usiku huu wa leo basi kesho asubuhi na mapema. Ninakuhakikishia kabisa mamaake anajua kila kitu. Mabinti hawawaogopi kabisa mama zao wala hawawafichi mambo yao kivile ingawa wapo wachache wanafanya hivyo. Sasa wee akikupigia simu mwambie nimeambiwa na polisi niende kesho saa nne kutoa taarifa kama amerejea ama laah! usioneshe kujua kama kuna simu imerekodiwa hata akikuuliza mamaake. Jifanyi hujui kitu wala ukweli uliofichika kuhusu mkeo. Mkeo bado binti mwenye moto sana kichwani mwake unapaswa kuishi naye kwa akili sana tena moyo wako utie ubaridi uwe kama wa plastiki jokofuni." Alinambia shemeji na kidogo hapo nikawa naanza kulilazimisha tumaini jipya moyoni mwangu ingawa haikuwa rahisi.
Nilikaa kwa mama mpaka usiku majira ya saa moja ambapo simu yangu iliita na kuipokea baada ya kuona namba ngeni kabisa.
"Halloow..Hallooow!"
Niliita baada ya kupokea simu na kuona ukimya wa sekunde kadhaa upande wa aliyenipigia.
"Ha...hall..hal.h.allow!" Sauti ya kisito sito niliisikia na kuupasua moyo wangu kama nimemwagiwa maji ya baridi alfajiri. Hakuwa na haja ya kujitambulisha yeye ni nani wakati tayari sauti yake iliishi kwenye mishipa yangu yote ya fahamu. Alikuwa ni mke wangu Atuganile..…
 
SEHEMU YA 20

"Mume wangu mi nimekuja kwa bibi huku temeke hakika naogopa sasahivi kuishi nawewe una hasira mbaya sana. Lakini mama amenifokea sana nimeelewa kosa langu sana hivyo naomba usifanye chochote huko polisi nalala leo ila kesho nitarudi. Pia sitaki kikao jamanii."
Hayo yalikuwa maneno ya mke wangu yaliyonishangaza na kunifanya nibaki kimya kwa muda kabla ya kumkubalia na kumtoa wasi juu ya hilo. Jamani kupenda ni ugonjwa m baya sana. Ingawa tayari niliona kila dalili ya picha mbaya kuhusu Atuganile lakini nilishindwa kufanya maamuzi ya utengano kila nilipoifikiria Ndoa yangu. Hakika ni jambo kubwa mbele ya Mungu na hatuwezi kulitania kwa kuivunja kirahisi rahisi hivi. Miezi miwili tu? Hapana. Tena mbaya zaidi sheria zetu wakristo ni kali sana kwenye ndoa. Hakuna kitu kinachoitwa talaka.
Nilijikuta napata wazo na kuwashawishi ndugu zangu usiku huo.
"Mama na dada zangu, nadhani kuna jambo kubwa tayari nimejifunza kuhusu mke wangu alivyo. Amenipigia simu yuko kwa bibiake Temeke, kesho atarudi mapema. Nami sitakaa nae muda mrefu pasipo kuja naye huku. Ila nawaomba sana dada zangu msije muonesha tofauti yoyote ile. Kumbukeni tayari huyu ni mke wangu na haya ni matatizo ambayo inabidi twende nayo taratibu ili kumfuta kila tabia mbaya ambayo tumeigundua ingawa nina hakika mke wangu ni mtulivu wala hajawahi kuwa mtundu kipindi chote anasoma hadi amemaliza form six. Namjua vizuri hana ujanja ila ana ujinga ambao inapaswa tumuelimishe taratibu. Natumai kwa kosa lake hili kumsamehe haraka itamshangaza na kumjengea maswali yatayomfanya ajirekebishe mwenyewe. Nawaomba sana."
Hizo ndizo zilikuwa nasaha zangu na ombi kwa ndugu zangu pindi mke wangu ataporudi tena nyumbani. Wazo langu lilipokelewa kishingo upande lakini hakukuwa na kipingamizi. Watafanyaje wakati mwenye mke nishasema? Na ukizingatia ni mke tayari wala si hawala. Basi na ikawa hivyo Atuganile alirudi na hakukuwa na kikao chochote cha kumkanya huku ndio kwanza nikizidisha upendo kwake.
Japokuwa roho iliniuma sana siku aliyorudi alikuwa amebeba zawadi ya kuku mzima aliyekuwa kwenye mfuko maalum sambamba na simu kubwa ya tachi aliyonambia amepewa na mamaake mdogo huko.
Nilimpigia mama mkwe kuhakikisha kama kuna mama yake mdogo Atu huko Temeke naye alikubali na kunisihi inapasa siku moja niende nikapajue kwani ndiye ndugu yao pekee aliyekuwa jijini Dar. Maneno ya mama mkwe kidogo yalinipa tumini ingawa naye moyoni mwangu nilishaanza kumtilia shaka hususani nikikumbuka maelezo ya yule jamaa fumanizi langu kwenye simu ambaye alibwabwaja kuwa naye alichangia kumsomesha Atuganile.
"Mume wangu mi naona kabisa siwezi kukaa bila kusoma, kama shule hakuna tena naomba niruhusu nirudi nyumbani nikapate hata msaada wa kanisa nikasome kwanza chuo maana hali zetu hapa mbaya." Alinambia mke wangu wiki hiyo hiyo aliyorudi baada ya kunitoroka. Moyo ulisononeka na kuumia na kauli ile lakini sura ikaficha na kumshika viganja Atu na kumuelewesha kwa upole.
"Mke wangu kuhusu kusoma ni ahadi yangu ambayo sina budi kuitimiza. Sijawahi kukudanganya Atu wangu. Wiki ijayo utaanza chuo ondoa shaka kabisa."
Alifurahi baada ya kumwambia hayo na kunirukia akinikumbatia na kunibusu. Vitendo vyake vilionesha kuwa anapenda sana kusoma kwani hata nyumbani anapokuwa hana kazi muda mwingi alikuwa anaonekana akiandika andika. Lakini utata unakuja kwanini anashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani? Hususani ile ya mwisho ambayo ndiyo muhimu zaidi?
Kichwa kilinipasua lakini moyo ulinipa matumaini juu ya mke wangu huku nikiamini kila ndoa ina matatizo yake na inapaswa kupambana nayo. Kitu ambacho Atu hajakijua ni kuhusu kuuza kiwanja changu. Siku zote alikuwa na wasiwasi wapi nitapata pesa ya kumsomesha ihali maisha yetu aliyaona ya kawaida sana.
Nilifanikiwa kuuza kiwanja kabla hata wiki haijesha kama nilivyomuahidi siku hiyo nikamchukua na kumshangaza baada ya kwenda mjini kuulizia ada ya chuo. Tulizunguka karibu vyuo vitatu mpaka tukafika chuo kimoja kinaitwa STATE HEALTH.
Tulifika pamoja mpaka ofisi ya mapokezi na kuulizia taratibu za pale jinsi ya kujiunga na mambo mengineyo. Mke wangu alionesha kushangaa na kufurahishwan sana na mazingira ya chuo kile. Baada ya maongezi marefu na kusoma vipeperushi vya masomo yanayotolewa pale hususani kuhusu afya kama ambavyo alipenda mke wangu kwa kuwa siku zote ndoto yake alitamani kuwa muuguzi kama si daktari.
"Ada yetu ndio kama hivyo, milioni moja na laki nne kwa mwaka nje ya hosteli. Ila milioni mbili na laki mojua sambamba na hosteli."
Aliongea kutuma maelekezo bwana aliyetupokea.
Atuganile alishangaa sana na macho yake yalionesha kukata tamaa pindi aliposikia zikitajwa milioni kirahisi rahisi vile. Ilibidi tutoke faragha kwanza kujadili hilo kabla hatujarejea tena ofisini.
"Mume wangu mbona pesa nyingi sana? tutazitoa wapi jamani?"
"Usijali mke wangu kama umepapenda milioni moja na laki nne si kitu mbele ya elimu. Jua ukipata diploma ndani ya miaka miwili ni sawa na milioni mbili na laki nae ambayo si kitu mbele ya faida kubwa utayopata."
"Etiii eeh! halafu mume wangu ujue masomo ya afya kazi nyingi sana ni rahisi pia hata kujiajiri kama una uwezo."
"Kweli basi kama umepapenda tufanye taratibu za malipo leo hii."
"Eeeeh! jamani waoooo kumbe unazo pesa mume wangu aaah i love you so much."
Alinikumbata na kunibusu huku akifurahi.
Tulirudi na kulipia laki saba kama kianzio ada na kupewa risiti. Siku ya pili yake nilimfanyia shopping ya nguvu Atuganile wangu nikizidi kujipa moyo wa imani kuwa ni mke wangu na yote ni haki yake kumtimizia. Niliamini siku zote matendo mazuri humkumbusha mtu kulipa wema pasipo kujua kuwa binadamu ni wepesi sana kusahau wanapotendewa wema kuliko kusahau wanapotendewa ubaya.
Kwanini malipo ya wema wote nilioufanya katika ndoa yangu yamekuwa adhabu?
Aaaaah! Atuganile mke wangu kwa gharama zote nilijitoa kwake pasipo kinyongo mbali ya kero na mambo ya ajabu aliyoanza kunionesha ndani ya miezi miwili tu ya ndoa. Sikujali wala sikuogopa kumsomesha tena kwa mara nyengine. Niliamini kuwa yupo kwangu na mimi ndiye mumewe. Hakika nilijivesha moyo wa naironi pasipo kujua kumbe nimezama ndani ya moto mkali.
Mungu si Athumani Atuganile kwa mbwembwe na bashasha alianza rasmi chuo. Kila siku asubuhi nilikuwa namsindikiza hadi jirani na jengo lao ndipo narudi ili apate kupazoea. Hata jioni wakati wa kutoka huwa namsubiri kituo cha basi na kurudi naye kama alivyodai ili azidi kupazoea.
Kumbuka kipindi hiko sikuwa na kiwanja pia hata madeni nililipa kuanzia kule ofisini na pale nyumbani nililipa kodi ya mwaka mzima ingawa nilishindwa kuongezea mtaji wowote wa biashara kutokana na pesa kuzidi matumizi.
Ilikuwa ni mwezi wa tisa tayari. Miezi mitatu baada ya ndoa yangu.
Safari hii nilianza kuiona furaha ya ndani ya ndoa ambayo niliitarajia muda mrefu toka kwa mke wangu. Ingawa pia muda wa kuwa nae ulizidi kuwa mchache hata kwenye haki ya tendo la ndoa, baada ya kuanza tu chuo alizidi kukaza huku akinisihi hajazoea kusoma na kufanya mapenzi anaweza kunogewa na kufeli upande wa shule kwani hataki afeli tena maana pesa zinamuuma pia.
Kauli zake za kuonesha anazihurumia pesa nitoazo kwaajili yake kidogo zilinipa imani ya kujali na faraja ya kusubiri.
Siku zilisonga hatimaye mwezi ulifika tokea Atuganile wangu aanze chuo. Kila siku ilinitoka elfu tano ya nauli na matumizi yake ya chuo achilia mbali pesa ya kula na mengineyo ya nyumbani. Hakika nilijitahidi sana kuhangaika katika mitiksi yangu ya 'game' na mambo mengine ili kuhakikisha haikosekani elfu tano ya kumpa mke wangu kila uchwao anavyoenda chuo. Kuna siku nyengine nilikuwa tayari kushinda njaa ili kumtunzia mke wangu elfu tano ya chuo.
Lakini kweli aso fadhila ahafadhiliki. Mwezi mmoja tu baadye ambapo ilikuwa mwezi wa kumi, chuo kilifungwa kwa likizo ya wiki moja.
Ndipo siku hiyo mke wangu aliponambia.
"Mume wangu kipenzi. Nakuomba uniruhusu niende kumsalimia mama Mbeya nimemkumbuka sana."
Kauli ya Atuganile aliyoitamka akiwa ameegsha kichwa chake kifuani mwangu siku hiyo usiku baada ya kufunga chuo.
 
SEHEMU YA 21

Kwa kweli jibu halikuwa jepesi kabisa kumkubalia aondoke ihali nilijua gharama zitakuwa kubwa zisizo na msingi. Yaani hata kama kummiss mama ndio ndani ya miezi mitatu tu? tena kila siku anaongea naye kwa simu? Hii haikuniingia akilini haraka lakini pia moyo wangu ulikuwa haupendi kabisa nimuone mke wangu anakosa furaha. Hakika nathubutu kusema kwake nilikuwa zoba. Nilimpenda na kumuamini sana huku nikijifariji kuwa ipo siku kila mtu atanisifu kama walivyonisifu kabla sijamuoa. Niliamini Atuganile huenda kufeli masomo ni vitu vilivyoongeza chachu ya akili zake kutotulia.
"Mke wangu! kwanini usitumie muda huu wa likizo kujisomea zaidi ili uzidi kufanya vizuri kuliko kwenda kwa mama! tena unaona hali yetu kwa sasa haiko vizuri."
Nilimshawishi lakini kauli yangu haikumuingia kabisa Atuganile.
"Kwani tatizo nini baby? nauli?"
"Hilo nalo tatizo mke wangu, nauli ya kwenda na kurudi huko kama tutaitumia kwa nauli za kwendea chuo unadhani tungeokoa sh ngapi? Kwa mama tutaenda wote kumsalimia mwisho wa mwaka."
"Hamna baby kweli siwezi mume wangu halafu kuhusu nauli wala usijali baby ninayo ya kwenda inatosha mama lazima atanipa ya kurudia baby kweli nakuomba my mume One!"
"Mke wangu hiyo nauli umeitoa wapi jamani?"
"Mume wangu mimi ni mwanamke lazima niwe naweka akiba katika pesa zilezile unazoniachiaga na kunipa nauli za chuo nilikuwa nabania kwa dharula nikijua si kila siku utakuwa unpata mume wangu."
"Mh! haya lakini..."
"Jamani lakini nini baby mbona unakuwa mgumu jamani nipe nafasi ili nikirudi nisome kwa amani kweli tena nimemkumbuka sana mama."
Alinihadaa na kutilia mkazo azma yake Atuganile. Moyo ulijilazimu kuhadaika kwa kumkubalia lakini akili zangu zilipinga na kujisikia vibaya.
Mwishowe nilijikuta nikikubali yaishe kwa kumpa ruhusa ya kwenda kukaa siku tano tu. Alifurahi na ndipo maandalizi ya safari yakaanza hadi siku ya siku nilipomsindikiza kituoni wakati huo nilishazungumza na mama mkwe kuhusu safari hiyo.
Lakini kwa upande wa mama na dada zangu walinipinga na kunilaumu sana kumruhusu Atu asafiri tena kurudi kwao ilihali tumeoana hata miezi sita bado. Lakini kuna muda sijui kwanini nilijikuta nakuwa mkali hata kwa dada zangu pindi wanapomsema vibaya mke wangu mbele yangu ama wanaponipumbaza.
"Kaka, mwanamke amekutawala kabisa! yaani juzi tu katoroka leo tena unamruhusu kwenda kwa mamaake? huyo si mwanamke kakaangu dawa yake kama kang'ang'ana kwenda huko mchukue mwanamke yeyote akija amkute hapo ili atie adabu." dadaangu mmoja alinipa ushauri ulionikera sana.
"Hivi dada nyie mna akili kweli? Kumbukeni ninyi ndio mlionishawishi kwa nguvu na kunisihi kuwa endapo sitamuoa Atuganile basi sitopata mwanamke mzuri aliyefundika kama yeye! halafu leo tena mnasema ooh! si mwanamke? Nilishawaambia kuwa haya matatizo hatuna budi kupambana nayo kwani si tabia za mke wangu, lazima kuna kitu kinamsumbua tu kama si mchezo wa mtu ili kuitibua ndoa yangu. Naomba msimseme vibaya mke wangu namjua vizuri kwa muda mrefu hana mazoea ya wanaume hivyo na mimi ndiye mwanaume wake wa kwanza na ndiye mumewe na pia mkumbuke dini inatwambia nini."
Niliwaka na kutilia msimamo na huo ukawa mwanzo mwengine wa kuanza kuyumba mahusiano ya upendo wa dhati baina yangu na dada zangu ambao tokea wifi yao atoroke kwa mara ya kwanza nao walijenga chuki na kukata mguu kwangu.
Siku zikasogea tangia mke wangu asafiri kwenda kwao huku mawasiliano yakizidi kuwa magumu siku mpaka siku. Mara nikipiga simu haipatikani na nikiuliza naambiwa chaji ndio tatizo, mara network inasumbua, mara inaweza kuita tu isipokelewe.
Yaani muda wote moyo wangu Atuganile aliuendeesha kama gari bovu. Muda wote matukio yake ya zamani ndiyo yaliniumiza sana kichwa. Atuganile alijawa kila aina ya tabia nzuri. Atuganile alionesha moyo wa kweli wa kupenda na kuhitaji. Wapi ninapokoea mpaka anabadilika tokea nimuoe? Wakati ndoa ndicho kitu alichokuwa anakihitaji hata yeye mwenyewe? Alinichanganya sana hasa nikimfikiria mbona nilimkuta bikra? Lini kaanza hiyo michezo hadi awe hivyo? Hapana, kiukweli ilikuwa ngumu sana kuniingia akilini na mara zote nilikuwa nafikiria huenda kuna michezo ya kishirikina inafanyika ya kumzingua akili mke wangu.
"Au Sulu huko kwao kaenda kumroga nini ili yatimie maneno yake? Maana waislamu na mambo ya uganga uganga ndio wenyewe. Mmh!" Mawazo yangu yalienda mbali zaidi na kumfikiria rafiki yangu kipenzi wa zamani. Yeye hakuwa mkristo kama mimi lakini utofauti wa dini zetu haikuwa sababu ya kutufanya tusiwe marafiki tulioshibana hadi pale urafiki wetu ulipolega na kufa huku chanzo kikiwa huyuhuyu mke wangu Atuganile.
Wiki ilikatika pasipo Atuganile kurejea wala kunambia anarejea lini. Moyo uliniuma zaidi kwa kukosa mawasiliano ya karibu na mke wangu. Yaani kila siku mimi ndiye nilikuwa wa kuwatafuta wao. Hakuna aliyeonesha kunijali kwao yaani hata mama mkwe? Yaani kwa muda huu mfupi tu ndio wamenisahau kabisa kuwa mimi ndiye nilikuwa naugawa mshara wangu kwaajili yao? Nimewakosea wapi!? Ina maana upendo wangu wa kweli ndio umegeuka adhabu? Ina maana kumuonesha mtu mapenzi ya kweli ni dhambi? Mbona binaadamu tuna mambo ya ajabu kwa binaadamu wenzetu? Kila mtu anahitaji kupendwa lakini kwanini wengi wanaooneshwa huo upendo wa dhati wanawaona wanaowapenda mabwege, wajinga, washamba, watwana... aaaah! kwanini?
Niliumia sana hata kula ilianza kuwa tabu. Wengi wanaume wanaooa nawaonaga wakinenepa miaka ya mwanzo kwenye ndoa zao. Lakini ndoa yangu daaah ndio kwanza ilizidi kunifanya nikondeane.
Chuo kilifunguliwa huku Atuganile akiwa hajarejea wala kunambia lini anarejea na zidi ya hapo zilishakatika siku nne wote wakiwa hawapatikani hewani, si yeye wala mamaake. Niliumia na kuumiza sana kichwa.
Siku hiyo nikiwa natembea mdogo mdogo barabarani mawazo yakiwa yamechukua nafasi kubwa kichwani mwangu mara tumbo lilianza kuninyonga na kukata. Kwa yule ambaye anayajua maumivu makali ya tumbo utakuwa unaipata picha kiasi gani tumbo linauma. Hakika maumivu yalikuwa ya ghafla na makali mno. Hata kutembea nilijikuta nashindwa ghafla na kuchuchumaa pembeni ya barabara huku nikianza kuhisi hadi kizunguzungu. Nilijitahidi sana kujikaza ili nisonge mbele walau nifike kituo cha daladala lakini nilijikuta nikishindwa kabisa. Maumivu hayakuwa ya kwaida. Watu walipita na kunishangaa huku wengine wakinitazama kwa huruma lqakini wakishindwa kunisaidia. Machozi yalianza kunitoka huku jasho likizidi kunilowanisha pale nilipochuchumaa. Nilitamani kulala kifudifudi lakini nilijikuta nashindwa kutokana na sehemu yenyewe ilivyo na pilika za watu. Maumivu yalizidi na kuzidi hata nikajikuta naachama mdomo ingawa sikulia kwa sauti. Nilitembelea magoti na kujiegamiza pembeni karibu na msingi wa barabara huku nikikata tamaa na kujiona sasa nakufa. aaaah! tumbo linauma jamani asikwambie mtu. usiombe upatwe maumivu makali zaidi ya tumbo hakika utajuqa nikisemacho ila kiufupi elewa kuwa tumbo linapochachamaa kuua ni shida sana. Nikiwa katikati ya mateso huku nuru ya macho ikianza kufifia mara nilimuona mtu akiniinamia mbele yangu na kuniita kwa sauti ambayo niliisikia kwa mbali kama niko ndani ya maji. Kumbe tayari nilikuwa nimelala na kujikunja pasipo kujitambua. Sauti ya mtu yule haikuwa ngeni masikioni mwangu wala sura yake haikuwa ngeni kabisa machoni mwangu.
Huo ndio ulikuwa msaada ambao sikuuomba wala kuutarajia. Ama kweli mwenyezi Mungu hutoa mitihani na nusura ili tujifunze katika maisha.
"One rafiki yangu vipi ndugu? Mungu wangu!"
Kauli hii ilikuwa ya mwisho kwa muda ule kuisikia kabla ya kuzinduka mara nyengine nilipojikuta hospitalini. Sultani Rwambo hakika alikuwa rafiki wa kweli ambaye nilishampoteza kwa sababu ya Atuganile. Yeye ndiye alitokea kama chemchem jangwani punde nilipokuwa taaban barabarani na kunikimbiza hospitalini akitumia gharama zake binafsi huku akiweka kando kabisa kinyongo kwangu tofauti na moyo wangu ulivyochukulia. Daaah! hakika maisha niliyopita kwenye ndoa hii sitamani kumuona mwengine anapitia. Natamani mimi ndiye niwe wa mwisho kuonja mateso haya mabaya. Lakini tatizo mapenzi ni uchizi na udhaifu jamani. Kama unavyoweza kuniona mimi ni dhaifu na mjing kwa kuwa mwenzangu uko nje ya mchezo ulionikuta. Lakin kama ungeuweka moyo wako ndani ya nafsi angu hakika nawe ungepofuka na kunihurumia kwanza. Hata sasa nikumbukayo ndoa yangu naamini kwabisa kweli mimi sikuwa mfano wa kuigwa kama mwanaume. Hakika nilikuwa bwege, mjinga mbele ya mwanamke huyu wa ndoto zangu. Lakini mwenzangu alikuwa mpumbavu kabisa asiyejitua mpaka siku ya mwisho ataposaga meno mbele ya bwana Mungu wetu.
Aaaaaaaaaaaagh! Ndoa yanguuuuuuuuuuuu!!
 
SEHEMU YA 23

Baada ya huduma muhimu na kufanyiwa vipimo hatimaye niliruhusiwa huku nikiambiwa tatizo langu kubwa la tumbo ni vidonda vinavyoushambulia utumbo kwa kasi sana. Madaktari walinisihi kuwa miongoni mwa sababu ya vidonda kunishambulia kiasi hiko ni msongo wa mawazo na kutokula vizuri.
Nilipewa vidonge na ushauri kabla ya kuruhusiwa na moja kwa moja Sulu alinisindikiza mpaka nyumbani.
"One kaka vipi mbona ndani kupo shaghala baghala hivi eeh! nini tatizo ndugu yangu?"
"Daah! kaka wee aha tu! kwanza naomba unisamehe sana kwa kauli zangu za kipindi kile."
"Achana na stori hizo One sisi ni wanaume hatunaga mambo ya visirani. Mi nishasahau hayo na ukimya wangu kwakuwa tu nilisafiri nje ya nchi na juzi tu ndio nimerejea na nilipanga kuja kukuona."
"Nashukuru sana Sulu kwa moyo wako lakini mwenzako ukweli nimekanyaga kaa la moto kwenye ndoa yangu."
"Kivipi tena?" aliuliza Sulu huku akikaa vizuri. Ilibidi nimuhadithie mwanzo mwisho yote yaliyojitokeza kabla na baada ya kumuoa Atuganile. Nilieleza hadi machozi yakawa yananitoka. Sulu alisikitika sana na kunitazama kwa huruma na kunishika bega huku akisema.
"Sikiliza One ndugu yangu. Hayo yanayokutokea wewe sio mapya kabisa wala si matatizo makubwa kuliko yaliyowahi kuwatokea wengine. Kujitesa kwako kwa kushinda njaa na mawazo havitakusaidia chochote wala havitamuumiza mkeo bali utajiumiza mwenyewe mwishowe ufe watakulilia kwa muda mfupi kisha mkeo ataolewa na mtu mwengine maisha yataendelea kama kawaida."
Nilituliza akili pindi Sulu alivyokuwa anaongea safari hii huku nikimtazama na kutazama chini kupata utulivu zaidi ya kusikia maneno yake ambayo sasa niliyaona kuwa yana faida sana.
"Kwa ufupi nimegundua kuwa Atuganile bado ana ulimbukeni kwenye kichwa chake unaomfunga hisia za moyo wake. Na si kwa maana hakupendi? hapana Atu anakupenda sana kama nawe unavyompenda ila kuna kitu kimoja unapaswa ukijue siku zote. UNAWEZA KUPENDWA NA ULIYEMPENDA LAKINI BADO HITAJI LA MOYO WAKE UKAWA SI WEWE." Aliongea kwa msisitizo Sulu na kunyamaza kwa sekunde kadhaa akinitazama kabla hajaendelea.
"Cha kwanza, Atu ameonesha dalili zote kama ni mnafki. Kwetu waislamu tumefundishwa dalili kuu za mnafiki ni tatu. akisema hasemi kweli, akiahidi hatimizi na akiaminiwa hufanya hiyana. Na hayo yote kayatimiza Atuganile kwako. Amekuwa muongo, ameshindwa kutimiza ahadi zake na amefanya hiyana hata ulipomuamini. Sasa kwa kukuhakikishia One Atuganile amekubali kuolewa nawe si kwakuwa alihitaji! hapana ila alipenda tu kukuridhisha."
"Mh! Sulu mbona unanichanganya unaposema ananipenda uko wapi upendo wake sasa?"
"Upendo wake upo ila uhitaji wake haupo kabisa kwako. Ila nataka nikuhakikishie kama moyo wa Atu haupo pamoja na wewe wala hakutaka kuolewa kutoka moyoni mwake. Nipe namba yake nikuoneshe mchezo sasa hivi."
alisema Sulu na kumpa namba ya Atu huku nikiwa na shauku ya kuuona huo mchezo wenyewe. Aliaandika kwenye simu yake na kuipiga. Tofauti kabisa na pindi nipigapo mimi simu ya mke wangu inachelewa sana kupokelewa hata isipokelewe kabisa. Lakni alipopiga Sulu namba ambayo hakika hakuwahi kuwa nayo Atuganile, simu ilipokelewa haraka huku 'earphone' moja akinivisha sikioni mwangu Sulu na kusikiliza kila alichokuwa anazungumza na mke wangu.
"Halloow Atuganile mama hujambo?" alibadili sauti Sulu na kuongea kwa rafudhi ya kinyakyusa kidogo.
"Sijambo, nani?"
"Aaaah! ina maana hata sauti ya mwalimu wako umeisahau? kweli umekuwa sasa."
"Aii! jamani Ticha Alex ninii?"
"Enhee nambie Atu mama nimesikia kuwa umeolewa mama uko Dar unakula maisha."
"Hamna ticha bwana, wee kakwambia nani maneno hayo?"
"Atu mama, mtu hukunyima tonge la ugali lakini si neno."
"Mh! sasa kama nimeolewa mbona niko Mbeya sasa?"
"Weee! upo Mbeya?"
"Ndio nipo hapa na kuna ufadhili ushatokea ndio tupo katika harakati za kufanikisha ili niendelee na masomo ya chuo."
"Mmmh! Atuganile hebu nambie ukweli sidhani kama uliwahi kuwa muongo hapa shuleni. Hivi ni kweli kabisa hujaolewa? Maana aliyenambia ni mtu mkubwa na ni mtumishi wa Mungu?"
zilikatika sekunde kadhaa kabla sauti ya mke wangu haijasikika tena akibonga huku masikio yangu yakitulia ingawa moyo ulizidi kwenda kasi kwa maneno ya Atuganile.
"Ni kweli ticha Alex niliolewa lakini sio kwa matakwa yangu. Ugumu wa maisha na ahadi za kusomeshwa vilifunga ukweli wa moyo wangu na kuamua kumkubalia tu yule kaka lakini sikutaka kabisa wala sikuwa tayari na maisha ya ndoa. Halafu kitu chengine baada ya kuanza maisha kumbe naye hakuwa na uwezo kama sisi yaani alitumia uongo wa kuahidi kunisomesha lakini kumbe nia na uwezo huo hakuwa nao na nikaishia kuwa mama wa nyumbani tu na mbaya zaidi ndani hakukuwa a amani wala utulivu. Anavuta bangi mume mwenyewe mlevi kila siku maugomvi mara kunipiga hadi kunitishia kuniua. Daah! yaani Ticha nikajaribu kuvumilia na kumsihi lakini wapi mwishowe hata akawa anakuja na wanawake zake nyumbani mi ndio nikashindwa kabisa. Nikamwambia mama akanitumia nauli ndio nikaamua kurudi huku na mpango si kuishi tena na yule bwana heri niendelee kutimiza ndoto zangu."
Almanusura niropoke kwenye simu kumjibu Atuganile kwa maneno ya uongo uliokithili aliokuwa anaongea huku sauti yake ikiwa imejaa huzuni.
Sulu aliwahi kukata simu kwanza na kunishusha presha iliyoanza kunipanda huku macho yakiwa yamenitoka na machozi kunivuja.
"Sulu? Mimi! Mimi navuta bangi? mimi jamani mimi nakunywa pombe na kumpiga mke wangu? aaaaaaah! eeee Munguuuu wangu daaaah!"
nililia kwa kweli huku kwikwi ikinikaba lakini ujasiri wa maneno ya Sulu ulinifanya nijikaze na kutulia ingawa kwikwi haikuniisha huku macho yakiwa mekundu.
"Sikia Sulu wewe ni mtoto wa kiume na hawa ndio wanawake. Kuna kitabu niliwahi kusoma kiliandikwa na Mtoto wa Becker ambacho kwa nje kimeandikwa kwa swali lililoulizwa 'WANAWAKE NI WAUAJI?!' jibu linaweza kuwa ndio ama sio kulingana na maono na maelezo yako mwenyewe. Lakini pia mwenyezi Mungu katika qur'aan ametusihi wanaume na kutukumbusha kuwa tuishi nao kwa akili sana wake zetu. Maneno ya Mungu yana hekima pana sana kama utayajaza kwenye imani. Sasa hupaswi kuchanganyikiwa kwa maneno ya Atuganile wala usiijenge chuki kwake kwa uongo alioutengeneza ila unapaswa kuelewa kuwa Atu ameyasema yote hayo kukusingizia ili asimame katika ukweli wa hitaji la moyo wake. Sasa ngoja nichati naye kwa ujumbe wa maneno."
Aliongea Sulu lakini kabla hajafanya hivyo simu yake iliita na aliyekuwa anapiga alikuwa Atuganile mke wangu.
"Vipi Ticha mbona simu ilikatika ghafla?"
"Iliisha vocha Atu hivi ndio nilikuwa kwenye mpango wa kumtuma mtoto dukani. Enhee!"
Maongezi yaliendelea huku Atu akizidi kuthibitisha msimamo wake wa kutorejea kuishi nami tena zaidi yuko tayari kwenda hata kuomba kanisani kuwa ndoa ivunjwe ili awe huru katika masomo yake akisisitiza zaidi kuwa tabia zangu za ulevi, kumpiga na umalaya ndio vimemkifu zaidi ukichagiza na kutomtimizia ahadi ya kumsomesha na vitisho vya kumuua.
Kipindi maongezi yakiwa yanaendelea Sulu alinambia kwa ishara kuwa nimpigie mke wangu simu muda huo huo kipindi wakiendelea na mazungumzo.
Nilifanya hivyo huku nikiambiwa kuwa simu nipigayo inatumika. Nikarudia rudia zaidi ya mara tano mpaka walipomaliza mazungumzo.
"Umeona One! sasa huu ndio mwanzo wa kujifunza rafiki yangu usije kuwa mzembe tena. Sasa usimpigie sasa hivi uone kama atakupigia ila baadae mpigie na umwambie kuwa unaumwa na hali yako si nzuri. Hii ndiyo tabia ya mkeo ambayo hukuwahi kuijua One. Mkeo kwanza ni mwepesi kudanganyika na ni mtesi wa upendo. Pole sana rafiki yangu ila itabidi upambane acha mawazo tayari kashakuwa mkeo angalia utafanyaje katika kuinusuru ndoa yako. Mi nitakuja kesho asubuhi na mapema kukuona rafiki yangu maana niko nje ya muda hata shemejio naona kashaanza kusumbua."
Aliniaga Sulu na kumsindikiza hadi barabarani ambapo alinisihi sana sana kuwa niache mawazo, nile na nichukulie kawaida huku akiniahidi kuwa pamoja nami siku zote.
Kwa kweli ingawa nilinunua chakula na tayari nilikuwa nishaanza dawa lakini sikusikia ladha wala hamu ya kula chakula kile kila nilipokumbuka maneno ya mke wangu niliyoyasikia mwenyewe kwa masikio yangu. Atuganile? daaaaah! niliitazama tazama simu yangu mpaka muda huo hakukuwa na simu ya Atu wala meseji ya tafadhali nipigie.
"Ina maana hata missed calls hakuziona?" Nilijiuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa rahisi tu kuwa si kweli na ukizingatia mara ya mwisho yeye ndiye alimpigia Sulu.
Niliandika meseji kwa upole na upendo wa maumivu nikimwambia.
'Mke wangu Atuganile, nimekukumbuka sana baby na chuo washafungua mbona siku zinaenda mamy nini tatizo? pia mumeo naumwa sana sina hali hapa nilipo leo ndio nimeruhusiwa hospitalini mke wangu. rudi tafadhali nateseka mumeo.'
Niliandika ujumbe huo ambao ulinitoa hadi machozi mwenyewe na kulia kwa uchungu sana. Moyo uliniuma na kuniuma sana. Ndoa yangu bado ingali changa sana. eeeh! miezi mitatu tu? ooooooooooooh! Atuganileee!
Nusu saa ilikatika tena pasipo ujumbe wangu kujibiwa. Niliamua kumpigia tena Atuganile huku nikijikaza asijue kama nilikuwa nalia. Na hapo ndipo simu ilipopokelewa lakini aliyepokea hakuwa Atuganile! Daaaaaaaaaaah!
 
SEHEMU YA 24

Alistuka Atu na kujichekesha kabla hajakaa mkekani na kunisalimu.
"Jamani baby mbona ghafla hivyo?" alinena nami huku akiwa hajiamini amini pale chini nami sikutaka kumuonesha dalili zozote mbaya wala kustushwa na muonekano wake.
"Usijali baby nimekuja kukuona baada ya kusikia unaumwa lakini nashukuru kwa ninavyokuona tu upo poa eeh!"
"Mh! we acha tu baby niko poa jioni hii ndio nikawa nafanya maoezi ya kuzunguka mitaa ili kesho nianze safari ya kurudi kwetu nilikumiss sana mume wangu." Bila haya Atu alinena na muda ule simu yake iliwaka mwanga kuonesha ilikuwa inaita lakini haikutoa mlio zaidi ya kuvibrate. Aliitazama pasipo kuipokoea.
"Mbona hupokei baby?"
"Haah! achana nae Mery huyu wa chuo nikipokea ataanza maongezi malefu wakati sasa hivi niko nawe baby wangu." Alijibu Atuganile maneno ambayo nilihisi wazi kuwa ni uongo mtupu. Moyo uliniuma kwa kweli sio kidogo japo nilijitahidi kutabasamu na kuficha usoni.
"Hebu nione simu yako mamyto." nilijikuta uvumilivu ukinishinda na kutamani kuona ushahidi zaidi wa mke wangu kiasi gani amenichoka na kunisaliti mbali ya kutotaka kuwa nami tena.
"Jamani baby ya nini tena badala tuendelee na mazungumzo mume wangu."
"Sasa unaninyima mumeo simu ambayo nilikununulia mwenyewe?"
Nilimuuliza swali kwa sauti tofauti kidogo ambayo sikupenda itoke lakini iliniteleza kutokana na vuguvugu la joto hasira kuzidi kutafuna kifua changu.
"Haya basi isiwe ugomvi." Alinisogezea simu na kunyanyuka kuingia ndani akionesha wazi hakupenda hata kidogo. Sikujali zaidi ya kuanza kutazama 'inbox' ya ujumbe aliokuwa anatumiwa na upande wa ujumbe aliokuwa anatuma.
Asaaalaaaleeee! jamaniii! macho yalihakiki kile nilichokuwa nakisoma huku akili ikinukuu na moyo kusoma kimya kimya.
'Inbox' ya mke wangu zilijaa jumbe za mapenzi mapenzi tena kutoka kwa namba tofauti zengine zikiwa zimehifadhiwa kwa majina tofauti ya kuvutia. Miongoni mwa majina yaliyokuwa na jumbe nyingi yalikuwa MY MUME, MY LOVE SHEBBY, BABY T, MY JOHN, R BODABODA, na mengine ambayo hayakuseviwa majina zaidi ya namba tupu. Niliumizwa mno na jumbe nilizosoma huku nyengine zikionesha wazi kuwa mke wangu alikuwa akitembea nao kimwili kama huyo 'My Love Shebby' na 'My Mume' ambapo jumbe yake moja ilisomeka.
'Atu baby hakika wiki moja tu uliyonipa mapenzi umenifanya usiku wa jana kuuona mlefu sababu yako. Nakupenda sana sina budi kufanya hima nikuoe mpenzi ili nijifaidie raha zako kila siku.'
Niliumia sana hata kwa upande wake alivyokuwa ameujibu ujumbe huo akiahidi na kusisitiza.
'My love, wewe ndie kila kitu kwangu. Nakupenda sana natamani iwe kesho baby.'
Chozi lilinitoka ingawa sikuweza kulia. Muda huo wote mke wangu hajatoka tangia aingie ndani pindi aliponikabidhi simu yake iliyojaa uchafu.
Ujumbe mwengine waliokuwa wanatumiana ulikuwa wa aibu sana hata kuunukuu. Mke wangu alionesha kiasi gani kakubuhu kwenye mambo ya wanaume.
Sikuwa na hamu ya kuendelea kusoma jumbe zake zilizokuwa zinaninyima amani na kuniumiza moyo zaidi niliamua kuandika namba yangu kwenye simu yake kuona ameihifadhi kwa jina gani kama majina yote ya kimahaba yamehifadhiwa kwa namba nyengine?
Hapo ndipo nilipokutana na jina 'MJOMBA' likitokea kwenye kioo cha simu ya mke wangu pindi nilipoipiga namba yangu.
"Hapa sina mke." Moyo ulinambia na muda huo mama mkwe alikuwa asharejea pasipo kugundua na akawa amekaa mkekani akinitazama jinsi nilivyokuwa nimechoka machoni na kukosa nuru ya tumaini usoni.
"Baba! enhee vipi hali zako?" sauti ndiyo iliyonigutusha na kujieka sawa huku nikitoa kiitambaa na kuyakagua vizuri macho yangu yaliyokuwa yameshaanza kudondosha machozi mepesi mashavuni.
"Mama, hebu naomba tuambiane ukweli nini kinaendelea kuhusu mke wangu?" Uzalendo na uvumilivu vikanishinda. Swali nililomuuliza mama mkwe lilimfanya akae vizuri huku akiwa na nyuso ya mshangao.
"Kwanini baba umeuliza hivyo?"
"Hapana mama kuna nyendo siku baada ya siku ananionesha mwanao zinanisikitisha sana nahisi kama hakuwa tayari kuolewa nami."
"Mh! ina maana Atu ameshakuwa na tabia mbaya?"
"Mama, hebu tazama simu ya mwanao halafu kama mzazi hebu kaa upande wangu uyaone maumivu niliyo nayo." Kwa sauti ya mtetemo nilimpa simu mama Atu kusoma jumbe za mwanae alizokuwa anatumiana na hao wanaume zake awapendao.
"lool! tena afadhali babaake naye alikuja jana inabidi haya mambo tuyazungumze sasa."
Aliongea mama Atu na muda huohuo alimwambia yule mwanae mdogo aende akamwite baba yao mdogo yule aliyekuwa anaishi Iringa.
Alinyanyuka mama mkwe na simu mkononi kisha nae akaingia ndani alipokuwa mke wangu ambae aliganda kabisa huko pasipo kutoka. Sijui alikuwa anajifikiria nini au alikuwa anajipanga nini lakini hata mama mkwe naye alichelewa kutoka hadi waliposikia sauti ya baba akisalimiana nami pale nje mara baada ya kufika nao wakatoka huku Atuganile akiwa amebadilika kimavazi na kuvaa nguo za heshima.
"Enhe vipi baba maisha yenu salama?" alifungua maongezi baba mkwe baada ya kusalimiana na wote kukaa mkekani.
"Salama kiasi baba tunamshukuru Mungu."
"Mbona unanitisha ukiasi gani huo baba? tena ujio wako wa ghafla inaonesha kuna tatizo." Aliuliza baba mkwe na kabla sijamjibu mama mkwe alidakia na kuweka mambo wazi.
"Ni kweli baba Atuganile mtoto wetu ameshakuwa kikwazo kwa mumewe kwa maelezo ambayo hata mimi yamenishangaza sana nimjuavyo Atu tokea yungali tumboni na maadili yote tuliyompa lakini safari hii naona ameenda kutuaibisha na kututusi kwa mumewe. Hebu eleza baba kama ulivyonieleza."
Kauli ya mama mkwe ilinipa uhuru kiasi fulani lakini cha ajabu nilijikuta nikizungumza machache huku mengine hususani kuhusu jumbe za simu nikishindwa kumwambia baba zaidi ya matukio machache kama ya kupeleka bidhaa dukani, kuondoka pasipo kuaga na lile tukio la kutoroka. Sijui hata kwanini ulimi wangu ulikuwa mzito kuzungumza yale muhimu zaidi ya kunipa point.
"Sawa baba pole sana kwa namna moja. Enhee Atuganile mwanangu hebu nawe tueleze maisha yenu na kuhusu tabia zako alizozungumza mumeo."
swali liligeuka kwa Atuganile aliyekuwa ameinama muda wote huku akinitazama kwa macho makali pindi nilipokuwa nazungumza na kunibedulia midomo.
Alipopewa nafasi naye kweli aliitumia nafasi na kwa mara ya kwanza uso kwa macho niliweza kuyaona makucha ya Atuganile yule niliyekuwa namuona mpole, ana nidhamu, ana hekima, lakini kumbeeee daaaah! Atu alinimaliza mbele ya wazazi wake kwa maneno makali ya uongo uliokubuhu.
"Baba kiukweli tangia nimeolewa sikuwahi kuwa na maisha ya furaha hata siku moja zaidi ya siku ile ya harusi. Ilifika wakati nilijuta kwanini nimeolewa na pia nilijitahidi kuvumilia na kumtunzia siri mume wangu sikuwahi kuwaambia haya lakini sasa inabidi. Kwanza kabisa One mnamuona hapa tu baba lakini ni mlevi sana, kila siku alikuwa anarudi amelewa ndani hakuna amani matusi na kunipiga pasipo sababu za msingi. Pia simu yake muda wote anazungumza na wanawake nakutana meseji za wanawake zake na kipindi hiko mimi nimemsevu mume wangu yeye akawa amenisevu 'Shangazi' hapo ndipo nilipoumia zaidi na mimi nikamsevu 'Mjomba' kwenye simu yangu kama alikuwa hajui hata sasa hivi nikikuonesha nimefanya hivyo kwa hasira. Kuna mengine baba aliyokuwa ananilazimisha mume wangu kunifanyia naona hadi aibu kusema. Halafu anavyonihisi namsaliti ndipo ananiumiza zaidi baba muulizeni hata mwenyewe hadi ananioa amenikutaje? sikuwahi kuwa na mwanaume yoyote wala kujihusisha na mapenzi kama kweli nilikuwa na tabia mbaya mbona sikumsaliti kabla hajanioa halafu nije msaliti ndani ya ndoa kweli? Au yeye kunilazimisha kuniingilia kinyume nilipomkatalia ndio aliona sahihi? Eti simsikilizi?.."
"Baba? hapana wee Atuganile mke wangu muogope Mungu aaah!" nilijikuta uvumilivu ukinishinda na kuingilia kati.
"Sasa mbona mwenzio alinyamaza ulipokuwa unazungumza baba! muache mwenzako naye aseme amalize." Mama Atu alidakia kunikatisha huku baba Atu akitoa ishara ya mkono kumwambia Atuganile aendelee kusema.
"Mungu namuogopa sana ndio maana nasema ukweli. Kuhusu hata Chuo ilikuwa tabu kunipeleka hadi nikatoroka na ndipo alipokubali lakini hata ada ameshindwa kunilipia kumbe aliomba awe anatoa kidogo kidogo na kila nikienda chuo naulizwa na mwalimu na kujisikia aibu hata wengine wakinicheka. Nasoma kwa aibu pasipo uhuru na nikaambiwa kama chuo kikifunguliwa pasipo kumaliza ada basi nisiende. Mi nimechoshwa na tabia zake ingawa nilikuwa tayari kurudi kesho hata asingelikuja lakini maisha haya nimeyaweka moyoni yakiniumiza nikishindwa jua nifanyeje aaah!"
Aliongea huku akilia Atuganile. Moyo uliniuma kupita kiasi, machozi yakatabaruku uso wangu huku kamasi nyembamba nazo zikibisha hodi puani. Nilijuta kumfahamu Atuganile. Alinimaliza huku ananiangalia usoni pasipo kunihurumia hata kidogo. Alinionesha kiasi gani yeye jasiri kuliko hata muindaji aliyepania kumuua nyani muharibifu wa mazao. Nilitamani nami niseme yote sasa hata meseji zake za wanaume lakini wakati wangu ulishapita. Nilishachelewa na nikakosa pointi. Nilijutia hata kumfata pale. Kweli Mbwa koko anapokuwa kwao hupata nguvu ya kumbwekea hata Simba. Yaani leo hii Atuganile ananichinja hivihivi? Mimi yuleyule aliyeniita 'my everything?' Aaaaah! kosa langu lipi kubwa? wema wangu tangia akiwa bado shuleni? kumsomesha kabla hata kumuoa? upole wangu na hekima? upendo wangu wa dhati? ina maana kumpenda mtu kweli na kumuonesha ajue ni dhambi kwa watu? aaaah! Yako wapi mapenzi ya dhati? Niliyaona malipo ya wema wangu, thamani ya mke wangu, na ukarimu wangu vyote vikawa mizigo ya moto kwenye ndoa yangu. Hii ndio fadhila niliyooneshwa na mke wangu hata miezi sita ya ndoa bado. Yaani amesahau kwa muda mfupi hivi?
Baba mkwe alitikisa kichwa na kunitazama kabla hajazungumza.
Nafsi ilishakufa ganzi hata hamu ya kulala pale haikuwepo kabisa. Nilitamani nigeuze muda huohuo kwa gharama yoyote nirudi kwetu.
Lakini maneno aliyosema baba mkwe mdogo nayo mmmmh
 
SEHEMU YA 25
"Kwa maelezo yenu kuna kitu nimegundua kinawasumbua nyote hasa kwako baba. Kitu hiki ni wivu. Wivu haupaswi kuzidi ndani ya nyumba japo katika mapenzi ya kweli lazima wivu uwepo. Pia kitu chengine baba tabia ya ulevi na ugomvi si njema kabisa katika maisha. Nimesikitika sana kwa hilo ninyi bado vijana tunawataraji muishi vizuri mje kutulea wazee wenu. Sasa kwa hali hii ya ulevi na kupigana nini hatima yake unadhani? Tatu kuhusu chuo kama alivyoeleza mwenzio kama hali si njema kwako si vibaya kama tukisaidiana kwa hilo tukatafuta hata wafadhili kwa muda akaenda chuo hadi atapofikia ngazi fulani basi tunataraji nyote mtakuwa mmejifunza na kujirekebisha hivyo amani itarudi tena kwenye ndoa yenu na mtaendelea na maisha mazuri. ila kwa sasa nadhani ni vyema tukatazama upande mwengine wa kumsaidia mkeo asome na kupunguza mawazo huku nawe ukijipanga kujirekebisha kitabia na maisha mengine ya ndoa baada ya mapito haya ambayo naona amani kwa sasa haipo kwenu nyote."
Kabla hajamaliza baba mkwe mama Atu nae alidakia.
"Kwa kweli mkwe wangu nilimpenda sana na kumuamini siku zote! lakini kwa kitendo cha kumfanya mwanangu ngoma kimeniuma sana. Kweli baba kajirekebishe kwa hilo kuhusu chuo acha tufanye mpango wa ufadhili walau kwa mwaka mmoja ili mwenzio naye kichwa chake kiwe sawa. Siko radhi kwa sasa kwenda wote yasije yakatokea makubwa zaidi aaah!"
Maneno yao sikutaka kuyapinga hata kidogo. Niliwakubalia huku nikipiga moyo konde. Nafsi ilikubali matokeo ingawa iliumia. Sikutia neno lolote la hoja zaidi mwisho wa siku nilikubali walichopendekeza wao kuwa Atu wanamtafutia ufadhili ili asome chuo kwa sharti kuwa ataendelea kuwa mke wangu kama kawaida lakini nimuache walau kwa mwaka mmoja ili nijirekebishe ulevi na tabia mbaya baada ya hapo tutaendelea na maisha kama kawaida.
Ilikuwa kama hadithi za Abunuasi. Nilijua sasa ndio nanyimwa mke rasmi. Lakini pia kwa alichonionesha Atuganile hata mimi sikutamani kurudi naye tena.
Baada ya maongezi hayo ndipo kiliandaliwa chakula ingawa sikuwa na hamu kabisa ya kula lakini walinibembeleza sana na kula kishingo upande.
"Kula baby." Sauti ya unafki ya Atuganile haikuisha kuwa mstari wa mbele kunibembeleza. Niliumia sana nilitamani hata nimzabe kibao lakini nilishindwa. Kiliandaliwa chumba kwa niaba yangu na tulilala pamoja na Atu ambaye alikuwa ananukia vizuri mwili mzima. Kwa kweli hata mule chumbani nilitamani nitapike kwa maumivu makali yaliyonikaba kooni kuona unafiki wa ajabu nikitendewa na wakwe zangu. Niliumia zaidi juu ya safari yangu ambayo kwetu hakuna aliyejua na kilichonipata nilijuta kwenda.
Usiku huo nikiwa nimelala macho Atuganile hakuisha kunishika shika kimahaba akijifanya kuonesha mapenzi ya huba.
"Baby nimekumiss jamani nisamehe kama nimekuudhi mume wangu lakini ukweli napenda sana kusoma nakuahidi nitakutunzia tunda lako hakuna wa kulimega zaidi yako baby wangu." Aliongea kwa kudeka akijaribu kunibusu lakini nilimuondoa mikono na kumsogeza pembeni pasipo kumjibu kitu chochote.
Moyo ulizidi kwenda mbio mawazo yakaenda mbali sana na kukumbuka ni heri ningekubali kumuoa binti aliyenitafutia mama wa kulekule Daresalama kuliko maradhi niliyoyafata huku.
Atu unafiki wake ulikuwa wa ajabu sana. Yaani kama si yeye aliyenipakazia maneno ya uongo wa kero na kunipaka tope la unyama lakini eti chumbani tupo wawili anataka kujifanya malaika.
"Atu, niache nilale alfajiri nina safari ya kurudi kwetu."
Hilo ndilo jibu la mwisho kumjibu Atuganile usiku huo kwa sauti ya ukali kidogo ambayo naamini ilipenya hadi chumba cha pili alipolala mama mkwe. Na hapo ndipo alipotulza mzuka Atuganile ambaye alikuwa mtupu muda huo kama alivyozaliwa akijaribu kunitia mitegoni tufanye mapenzi lakini kwa jinsi moyo ulivyotibuka sikuwa na hamu kabisa.
Saa kumi alfajiri nilikuwa tayari nimeamka na kujiandaa kwaajili ya safari. Hata sikumbuki kama nilinawa ama kuoga kwani hata kulala kwenyewe sikulala kabisa. Nilijitahidi kutabasamu na kuwaaga huku mama mkwe akiwa ameamka na nyuso ya upole zaidi akinisisitiza walau ningeshinda siku hiyo kwa kuwa nilifika usiku.
"Mama Mungu akipenda nitakuwa nakuja mama usijali aa nyumbani."
Nilimjibu na muda huo basi pekee ya kudamka iliokuwa inaenda moja kwa moja Kyela ilifika eneo lile na kuisimamisha tayari kwa safari.
Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwangu kukanyaga kijiji cha Mtakuja huku nikijiapiza njiani kutorudi tena. Nilisafiri moyoni nikiwa na manung'uniko mpaka nilipofika Dar ambaponjiani nilikuwa nawasiliana na Sulu aliyenisubiri kituo cha basi kunipokea na hata usiku huo tulilala wote nyumbani kwa maongezi zaidi juu ya mkasa wa ndoa yangu.
Nakumbuka njiani muda mwingi niikuwa napokea ujumbe wa maneno wa Atuganile akiniuliza nimefika wapi, mara akinitakia safari njema, mara akipiga na kuniomba nimsamehe bure tu. Mwishowe niliamua hata kuibrock namba yake kwa muda nikifikiria kile kilichotokea ambacho kiliniuma vilivyo. Kunikana mbele ya wazazi wake?
Baada ya kumuhadithia Sulu kilichotokea alinipa pole sana na kunihakikishia kwa kusema.
"Umefanya vizuri kuwakubalia kile walichokwambia One kwani hiyo ni mipango ambayo ilikuwepo kabla hujafika pale. Tayari Atuganile kashakuchoma mengi sana nina wasiwasi hata babaake wamempanga wao kukuchafua. Ndugu yangu wanaume tunakutwa na mengi sana kwa sababu ya wanawake hivyo chukulia huo ni mtihani wa mpito tu. Chaguo la moyo wako kama utamsubiri Atuganile ama utaoa mwengine au itakuwaje."
"Sulu ndugu yangu kuhusu Atuganile mimi basi tena! nishasamehe kila kitu sitaki kabisa namuachia Mungu hata habari ya wanawake basi acha nifanye mambo mengine. Moyo wangu mteke sana nisije kufa bure."
Huo ndio ukawa msimamo wangu kuanzia hapo. Ingawa niliumia sana zaidi ya sana lakini moyo ulikufa ganzi japo nlikuwa bado nampenda sana na kumuhitaji Atu.
Kesho yake mapema nilienda nyumbani kwa mama na sikuwa na jinsi zaidi ya kuufikisha msimamo wangu mpya juu ya Atuganile na kuwaelezea kila kitu kilichotokea. Kwa mara nyengine tena mama alishindwa kuyazuia machozi kwa kile alichosikia kunikuta huku dadaangu nae akinipasha habari nyingi kuhusu ile namba ya mtu aliyekuwa bwanaake Atuganile kuwa ni daktari huko Kyela na Atu alivyorudi alipita huko kumuomba msamaha na wamesameheana.
Niliumia tena kwa habari zile na kuzidi pata picha kiasi gani Atuganile alikuwa mapepe.
"Mi nakwambia kaka yule binti nyoka alikuzidi akili." dada mwengine akadakia.
"Mama na ndugu zangu mimi nimewaelewa na sitokuwa nae tena Atuganile nimesamehe kila kitu kuhusu muda niliopoteza na gharama zangu zote namuachia Mungu atanilipa. Ila kuwanzia sasa sitakiwa suala la mke tena." Nilisisitiza msimamo wangu ambao kwa upande mmoja niliungwa mkono lakini upande wa pili nilipingwa na mama akisema.
"Mwanangu One, sio kila mwanamke atakuwa shetani kama Atuganile na dawa si kukaa bila mwanamke kwani haitakuwa rahisi kumfuta kichwani huyo jini Atuganile. Kuna binti anaitwa Rose mtoto wa rafiki yangu tokea shule nilikutana naye kipindi kile nilipokwambia kuna mchumba ukakataa nami sikuwapelekea jibu tena wala hawajajua kama ulioa. Sasa nadhani ndio muda muafaka mwanangu tufanye taratibu uishi na Rose. Ni binti mzuri tena kuliko huyo Atuganile na pia hana mambo mengi zaidi yeye ni fundi kushona. wazazi wake watu wa kanisa ni wastaarabu sana. Nashauri mwanangu kama utamuoa Rose utakuwa umemfuta Atuganile na Mungu atakulipa machozi yote yatakoma."
Maneno ya mama yaliungwa mkono na ndugu zangu lakini yaliniweka katika mtihani mgumu mno.
"Nioe tena? Mmmmh! hapana... hata Atuganile mlisema hivihivi mwanzoni. Hapana!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom