Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,177
- 34,444
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA 07
Akiwa ameongozana sambamba na mamayake Atu alisogea hadi kitandani nilipolala. Nilitamani ninyanyuke ila nilishindwa. Lakini cha ajabu kwa mara ya kwanza sauti ilitoka ingawa kwa shida sana lakini midomo ilinyanyuka.
"A-TU-GA-NI-LE" Niliita kwa kisitosito lakini nilifanikiwa kumwita binti yule huku machozi ya kutoamini yakizidi kunitoka. Hakika moyoni niliiona faraja na tumaini ambalo sikujua wapi litokapo. Atuganile alishindwa kujizuia na kujikuta naye machozi yakimdondoka.
"Mungu atakusaidia usilie...utapona mume wangu!" Aliongea maneno hayo huku akinishika kiganja cha mkono wa kulia na kulihisi joto lake likipenya kwenye maungo yangu mithili ya dawa iliyokuwa inaingia mwilini kuniponya na kunipa nguvu mpya.
Hakika nilishangaa leo Atu ananiita mume kama vile alivyoniita kwenye ndoto ile ya ajabu iliyotokana na tukio la mazingara.
Watu waliendelea kuingia na kutoka lakini si Atuganile. Sikutaka kabisa atoke. Niliona kama ndiyue mtu anayeweza nisaidia kupona haraka kila nilipomuona pembeni yangu. Mama Atu nilimsikia hata akimuaga mwanae ambaye hakutaka kabisa kuniacha mwenyewe. Nilishangaa kuona Atuganile ananionesha upendo wa ajabu ambao sikutaraji kuupata tokea aliponikatia simu siku ile.
Kitu ambacho sikukijua kumbe siku ile niliyopata matatizo ambayo ilikuwa jana yake. Habari zilipofika shuleni kwa kina Atuganile, ilimbidi atoroke na kuja kijijini kujua mengi zaidi kutokana ilibaki wiki moja tu shule kufungwa na walishamaliza mitihani.
Alijua fika Atuganile kuwa nampenda sana na kumbe tabia yake ilizidi kuwa kivutio moyoni mwake pasipo mwenyewe kujua lakinio sifa zangu zilimfikia.
Muda wa kuona wagonjwa ulipoisha Atu alibaki kama muhudumu wangu aliyekuwa akinipa uji na kunifutafuta. Hakika alinionesha upendo wa wazi na kuwaaminisha hata mafundi wenzangu kuwa kweli yule binti tunaendana sana na pia nina bahati mno kupendwa vile na binti mzuri, msomi na mwenye heshima.
Jioni ya siku hiyo hiyo mama sambamba na dada zangu wawili walifika wakiwa wametokea Dar huku wakiwa na nyuso za wasiwasi. Wote hawakuamini kunikuta nikiwa bado mzima. Walimshukuru sana Mungu ingawa nilishindwa kuzungumza vizuri lakini kushinda kwangu na Atu kulisaidia kunifanya ninyanyue mdomo kusema maneno machache kama kuitika salamu na mengineyo ingawa niliumia sana lakini nilijikaza nisionekane dhaifu mbele ya Atu wangu. Usiombe kupenda!
Kwa mara ya kwanza mama nilimtambulisha Atuganile kwa ishara kuwa ndiye binti niliyemwambia nimempata kwaajili ya Ndoa. Na hakika mama alipata faraja sana kutokana na heshima waliyooneshwa na Atuganile kwa kuwasalimia huku akikunja goti kabisa na alipotambulishwa kuwa ni mamaangu mzazi alisalimia tena kwa kupiga goti kabisa. Hakika ilipendeza na kufariji sana. Moyoni nilisali na kumuomba Mungu nipone haraka na ajaalie suala la Atu kuwa wangu wa maisha.
Usiku huo mama wakiongozwa na Atu walifanya maombi makubwa kuniombea. Hapo ndipo kikaonekana kipaji chengine cha Atuganile na kubainisha kuwa alikuwa mchamungu mzuri kumbe. Aliomba kwa imani hadi machozi yalimtoka.
".....Baba katika jina la Yesu tunakuomba na kukutumaini... Hakika kama ulivyotuahidi na kutukumbusha kuwa tusichoke kukuomba nasi usiku huu tunajiweka mbele yako muokozi wetu.... Utulinde na kumuondolea maradhi haya ya ajabu kijana wako baba.... Naiita nguvu yako kuu iweze kupenya na kuuleta uzima kwa kijana wako Onesmo. Hakika mbele ya Nuru yako hakuna giza lenye kuiziba....Navunja pepo la maradhi yehova.....Roho mtakatifu shuka na utende muujiza...Navunja mapepo ya maradhi na kuyachoma kwa moto wako mkuu baba... Uwajaalie watu wako wote wanaoteseka na pepo la maradhi ili wapone haraka warudi kukutumikia wewe muokozi.....Baba katika jina la Yesu tunaomba na kushukuru...Ameen" Yalikuwa ni baadhi ya maneno ya Atu katika maombi yale usiku ule. Imani ilizidi kunishiba nafsini kwa maombi ya Atuganile. Upande mmoja nilihisi kweli nuru njema ikijaa nafsini mwangu. Hakika kama ni maombi tu ya Atu basi muujiza wake ulianza kutendeka palepale hospitalini.
Kwani baada ya maombi usiku ule walielekea kulala kwenye nyumba ya daktari mmoja wa pale aliyekuwa ndiye daktari wangu na huku nyuma nikabaki na fomeni wangu usiku huo na dariri njema zilianza kuonekana. Kwanza niliweza hata kukaa na kutingisha viungo vyangu mwenyewe, kitu ambacho sikuwa naweza. Ingawa sikuweza kutembea wala kusimama mwenyewe lakini asubuhi yake niliweza kusema pasipo kuhisi maumivu makali ya koo kama ilivyokuwa awali.
Hiyo ilizidi kuwa chachu kuu ya kumpenda zaidi na zaidi Atuganile. Na si kwangu tu bali hata mama na dada zangu waliofika na kumuona.
Zilifika siku nne nikiwa hospitalini Kyela tokea nipatwe tatizo. Nilirudiwa kufanyiwa vipimo vyote lakini bado majibu yalisoma niko sawa asilimia zote sina ugonjwa wowote kisayansi. Hapo ndipo kila mmoja alichoka. Maombi ya Atuganile hayakukoma. Kila siku tulifanya sala pamoja tukiomba na kushukuru. Sindano nazo hazikukoma. Lakini kila nilivyochomwa sindano nilijisikia hali mbaya sana na hata kuhisi kama zitaendelea basi zinaweza kunimaliza kabisa. Safari hii niliweza kuzungumza ingawa si kwa sauti kubwa lakini pia hata maumivu hayakuwa makubwa kama awali.
"Mama! kama majibu yanaonesha siumwi sasa kwanini bado nipo hapa na hizi sindano ni za nini? Jamani mi sizitaki tena sitaki kuchomwa sindano." Niliongea siku hiyo ya nne na ndiyo siku niliyogoma kabisa kufanyiwa matibabu pale. Madaktari walinilazimu na kunisihi lakini mimi nilichoamini kinachonipa nguvu si sindano bali ni maombi ya Atu ambayo yalisikiwa moja kwa moja na Mungu. Na hapo ndipo nilipoletewa faili langu na kuambiwa kama sitaki basi nitie saini yangu ili waniruhusu. Bila kisto wala hofu nilikubali na kutitia sahihi. Na hiyo ikawa siku yangu ya mwisho kulala pale hospitali ingawa sikuwa na nguvu za kutembea mwenyewe lakini nilishikwa kila upande mpaka gest. Tulisindikizwa na Atuganile sambamba na mamaake aliyekuwa anakuja kila siku ingawa bintiye alilala na mamaangu pamoja na dadazangu wakishirikiana kuniuguza na kunifariji. Habari ya kugomea kwangu matibabu pale Kyela kila mmoja aliipokea kivyake. Wengine waliniunga mkono huku wengine wakinilaumu. Kampuni ililipa gharama zote na kuniingizia mshahara wangu wa mwezi ili uweze kunisaidia pamoja na laki moja kwaajili ya nauli ya kurudi Dar kwa matibabu zaidi kama tulivyodai.
"Vipi Atu mwanangu si tutaenda wote nawe ukamuuguze mwenzio na kuendelea kumfanyia maombi eeeh!" Mamaangu alimuuliza Atu huku akimuomba.
Atu hakubisha zaidi alikubali ingawa alidai kuwa kwakuwa anaingia kidaqto cha nne basi shule zitapofunguliwa tu itamlazimu arudi haraka kuendelea na masomo.
"Hilo halina tabu mwanangu." Ndipo hapo mamaangu walipozungumza na mamaake Atuganile ambaye kwa sauti ya huruma alisema.
"Mwanangu Atuganile nilipenda sana likizo hii aitumie kujisomea kwaajili ya kupambana na kidato cha nne ili asifeli.Ila hakika kijana wake Onesmo ni kijana wa tofauti sana na nimeona kiasi gani wanapendana na mwanangu ingawa sipendi kuona wanaingia kwenye mahusiano kwa sasa. Najua Atu bado mtoto ila One tayari anajua kila kitu. Hivyo nakuomba mama One, kwa dhamana yako namruhusu mwanangu muende naye ila ninachokusihi msiwape uhuru wa kulala pamoja pindi One atapopata nguvu na ahueni inaweza kutokea ya kutokea halafu ndoto za mwanangu zikafia njiani. Ila nimekubali One awe mkwe wangu hapo badae pindi Atu akimaliza shule."
Maneno ya mama Atuganile yaliungwa mkono na mama. Kesho yake asubuhi na mapema mama Atu ambaye naye alilala gesti moja nasi, alitusindikiza mpaka kituo cha basi na kupnda basi pamoja na Atuganile ambaye sikuamini muda wote kama sasa anaenda kwetu kama mke wangu mtarajiwa. Hakika moyo ulifura furaha huku nafsi ikiyaona matumaini. Matumaini ya ushindi wa kupata mke bora aliyekamili kuanzia sura, umbo, mpaka tabia.
Lakini doooh! sikujua kama Ndoa yangu inaweza kuwa Nuru iliyobebwa na nafsi ya kiza.
Atuganileeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!???