Ndoa yangu ipo ICU !dah

Kwa alipofikia unatakiwa kusimama sasa kama mwanaume na sio mtu wa kawaida.
Mpeleke mpaka mbele ya wazazi wake waeleze hiyo hali na muache huko kwa kumpa uhuru, yaani akitaka muendelee asimame kama mke wa mtu na si vinginevyo ila kama hataki mwambie kila la kheri.
Mke akifikia hatua hiyo muachie Mungu wake atamfunza adabu na siku akija kugundua makosa yake itakuwa ushapata ahueni ya moyo.
 
Mkuu pole sana. I know kwako sio rahisi kukubaliana na ukweli. Nadhan unaamin kuwa huyo mwanamke hawez kuku cheat na ndo maana ulivogundua ulikaribia kumuua, sasa hii ya sasa inataka kukutoa roho kabisa. Hutaki kuamin kuwa mkeo hakutaki tena na hawez kuishi na ww tena.

Mimi nakushauri, tafuta muda mtoe outing sehem nzuri, ongea nae kuhusu hatima ya ndoa yenu. Mwambie kuwa unahitaji abadilike ili muweze Ku move on. Kwa sbb now Mme stack. Kama atasema muachane au ataomba taraka. Please be a man mpe anachotaka. Mpe nafasi afanye anachotaka.

Ukiendelea kulazimisha mambo yatakupata ya kupatwa, unaweza kuwaacha watoto wakiteseka. Unaweza usiwe na nafasi tena ya kuongelea wanao . Nakwambia hiv with experience. Wanawake achana nao. Usipompa chance atatafuta mwenyewe hiyo chance.

Please kwa faida yako, ya watoto wako na kwa faida yake pia. Kama unampenda na unawapenda watoto wako, mpe anachotaka ili pia uipe nafasi ya kupumzika nafsi yako.

Hicho unachongangania ni hatari na hakina tija kwako, kwake wala kwa watoto wako. Utakuja kulia machozi ya damu.
 
Yaani akishajua tu you cant live without her anakuwa na kiburi sana, she can do anything akijua huwezi mfanya chochote (boya) sasa ikifikia hatua kama hiyo inatakiwa uanaume wako uonekane, ishawahi kunitokea situation inafanana kama hiyo yaani ilikuwa mwezi wa kwanza mwanzoni watoto ndio nimetoka kulipia ada (wako watatu) shule za kizungu mapicha picha yakaanza eti anataka kurudi kwao kachoka tu kuishi na mimi, nilichofanya mimi ni kumkatia tiketi ya ndege yeye na wanae sikujali kama nimeshawalipia ada ya mwaka mzima, matokeo yake kaenda kwao kakaa mwezi mmoja karudi mwenyewe. Ushauri wangu piga chini tuu atajifunza na atakukumbuka tuu
 
Huyo mwanamke hakuhitaji dhahiri kwa sasa ila naamini kulingana na umri wake kadanganyika sehemu mpaka anakuona sio kitu sio lolote ila ukimuacha tu akili itamrudi ila itakuwa too late atajuta
 
Najiuliza kama huyo mke wako akiwa ni member wa jf au awe anapitiaga huku alafu kaona huu uzi na mipango yote itakayofuata, hapo si anaweza akavaa ngozi ya kondoo kwa mda ili uone amebadilika na ughairi ulichopanga kufanya.
But pole sana bro kwa hiyo changamoto unayopitia, Mungu akuongoze ufanye maamuzi sahihi.
 
Na wewe huwa unasema unachepukaga kiaina so kumshauri mdau amuache mkewe ni kama unajiadhibu nawe pia haaaaaa
 
ingekua mimi hata kama tumefunga pingu za dhahabu na tunawatoto sota ningebwaga manyanga tu,kwa nini uishi wa stress wakati wanawake wa kuoa wako wengi tu,piga chini move on,hutakua wa kwanza wala wa mwisho kuacha/kuachwa na mwanamke,upata stroke kwa ajili ya stress
 
Pole sana mkuu, mara nyingine uhuru mwingi huleta matatizo, naweza sema kosa kubwa ni pale ulipomruhusu kwenda kuishi morogoro pekeyake.

Muhimu ni wewe kujitafakari na kufanya kile nafsi yako inaweza himili.

Ndio maana wengine hulka zao mke humfuata mke mwiko kuishi mbalimbali.

Uislam husema kukiwa na mwanamke na mwanamme peke yao (ambao sio ndugu au mke na mme) watatu wao ni shetani. Sasa ulivyomwacha aishi mwenyewe alikuwa huru kuwa na wanaume wengine ambao wamemchanganya mpaka akuone huna maana na ndio kisa cha kudai talaka maana anaona unam'bana. Anasahau akiwa huru huyo anayempatia kibri hatamwona wa thamani tena (vya wizi vitamu kisaokilijia).

Pole sana kaka ukiligundua tatizo ni mwanzo wa kupata ufumbuzi.
 
"Feel Irie"

How long shall you carry that burdens on your shoulders
How long shall those tears keep running down your beautiful face?
We all have troubles now and again, know what I'm saying
No matter how hard you try trouble will find us one way or another

People had troubles since the pope was an altare boy
People had worries from when the dead sea was only critical

Hear those drums rolling and listen to those guitar skanking

[Chorus:]
Put a smile on your face don't let the troubles get you down... shoop shoop doooo
Put a smile on your face don't let the troubles get you down...

Let me tell you how we feel... we feel irie... irie we feel irie... irie... we feel irie... irie
We feel so irie... irie

Do you feel like we do? (tell me) do you feel like we do? (I say) do you feel like we do?

No man can hide from his fears since they are part of him, they always know where to find him
Come on walk tall and keep your head high. I tell you again and again...

[Chorus]
 
Aise,hapo unamloga. Ila,sikatai ni mawazo tu. Unajua,binadamu ni mpana sana. Tena sana. Na ujue,mtu anapoamua kuweka mambo yake hapa,mazito kiasi hicho,lazima kuna jambo.
Waafrika tuna tabia mbaya,inayopelekea visa kama hivi. Si nyingine,bali kubembeleza bembeleza tu.
Mleta mada,narudi kwako. Siku hizi ukiangalia,iwe muoaji au muolewaji,wengi wao hasa wanawake wanapenda sherehe iwepo,ndugu wafurahie,wale wanywe. Ila,sidhani kama kweli wanajua wanakoenda na wanachoenda kukifanya. Ni kweli inauma. Tena sana. Ila,nakushauri,wewe ni mwanaume jikaze tu. Usije mgombeza mwanaume mwenzio kisa kakumegea. Kapewa kihalali kabisa. Na kama imefikia hapo,mwenzio hakutaki. Labda wazazi au ndugu uaite kuwaeleza maamuzi yako na sababu za maamuzi hayo,ila swala la kuwasuruhisha achana nalo. Kama hujawa chanzo cha yeye kubadilika,basi limbukeni. Wanasemaga zombi hashibi damu. Usidhami uhuni kaanza leo. Hivyo,jipange upya. Kama utamtafuta mwimgine sawa,kama watoto utawaletea housegirl,poa,ila mtu wa hivyo using'ang,ane kabisa. Yaani mke,wa ndoa tena,anakwambia tuachane? Hana adabu huyo
 
Muulize tena kama kweli anataka muachane. Akisema ndio mwambie akuambie sababu. Usijali juu ya majibu atakayo kupa, mwambie aende balaza la kata then mahakamani aombe yeye talaka hii itakurahisishia kwenye mgawanyo wa mali hata pata lolote la maana then from there move on. Uking'ang'ania utagia usingizini kwa shinikizo la damu. Mi yalinikuta nikapiga chini, nilikonda nikaisha ila sasa burudani napambana kupunguza uzito kwa raha zangu.
 
Pole sana mkuu,grandpa aliwahi niambia siku utakapooa ndipo siku utakapokuwa umenunua kisu cha kujichoma mwenyewe...


Ni muda sasa wa wew kukaa kimya na kujaribu kuwa busy na wanao...

Jifanye huna time nae....
 

Vikao muda mwingine ni kupoteza muda na kujichoresha hasa kwa ndugu wataishia kukwambia vumilia....
 
All these are very alarming statements. Sio za kupuuzia hata kidogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…