Ndoa yangu ipo ICU !dah

Ndoa yangu ipo ICU !dah

Unataka kufa? Wewe ni wa muhimu zaid kwa nduguzo na watoi, be ingenuine bro. Utakufa siku c zako
 
Mateso unayopitia ni makubwa kwa kweli Kuna ndoa naifahamu walikua hawaelewani Kama hivi ila baadae mambo yaka change siku hizi wanapendana balaa.naomba nitumie namba yake ya WhatsApp namtumia hii link akisoma nadhani atajiongeza anaweza kubadilika huwez jua
We jamaa nina wasiwasi na ww,naona kama unataka kuifanya fursa hii?
 
Dah umenkumbusha wakati nipo na mrembo fulani hivi ambae nilimpenda kupita maelezo but kupewa tu offer ya kwenda kusoma,akaanza kuchange na ndani ya miezi 6 tu akanipotezea mazima,nakumbuka nilimtamkiaa neno moja tu"UTANIKUMBUKA"basi miaka mi 4 ijayo napokea simu yake but skumjua akajitambulisha kwa jina lingne best yake basi ile kumeet ni yeye dah kachoka vibaya mno,na anakatoto juu kazalishwa na mruga ruga gani sjui,basi nkaongea nae fresh na kumsamehe then nkatoa simu nkaivunja vunja na line nkaichoma na kibiriti cha gesi pale pale then nkaondoka zangu.
Last 4 weeks walimzika sababu ya kunywa sumu kwa msongo wa mawazo
Wanawake huwa wanadanganywa mno kwa mambo madogo tu ambayo hufanya kuumiza wenzao but mwisho wa siku maumivu hurudi kwao na kuwaumiza mara elf
 
UPDATES....

Habari ndugu zangu JF...
Jumapili tulivu nikitokea church hapa misa ya kwanza kabisa...niliwahi na huyu mwanangu mdogo...nikasahau kumchapa pampers mana niliamka na mzuka wa kazi nikamwambia dada wa kazi aniandalie nguo tu na maji
Ntamuogesha mwenyewe nk ...kanikojolea usingizin church mpaka nimeishiwa pozi ase...hahaha ila burudani alipoamka kakaza sura namwambia umejikojolea kakana kwa sauti huku kanuna sijakojoa mimi😂...

Back to the topic...
Wakuu mimi ni mwanadamu na pia nina mengi kujifunza katika hili na nakiri kwa asilimia kubwa sana kubwa sana ushauri wenu umenisaidia sana tena sana kukubaliana na ukweli maana amini nawaambia tunaweza tukasema yote ila naamini kuna wengi mmenitangulia na ushauri mnaotoa ni from vivid life example...

Kuna mda week hii ninawaZa hivi labda aliteleza sijui (kutokana week hii namuona kakosa amani anajitahid kuniongelesha n.k na hata kutuma mesej za kawaida namjibu short tu mana tangu nimemblock whatsapp ni tabu)..ila nikikumbuka wadau ushauri wenu humu kwamba haya mambo yapo nisijitie kipofu na mawazo basi kidume nasali tu Mungu naomba nimalize salama hili natafuta zangu usingizi sebleni mdo mdo...

Anajua navyopenda mpira na huwa na enjoy sana kucheki boli indoor afu dak ya 80 huwa ndo natoka kuumalizia maeneo na washikaji...sasa safar hii boli kuanzia preview analysis linanikutia nje...jana mchana nilitoka kwenda kuchek la man u...nikarud nikapita saloon kunyoa nivorud nikamkuta nikasalimia nikapitiliza bafuni nikaoga nikajiandaa nikatoka mapema tena nikamwambia naenda mpirani(game la liver)
Nimetoka tu akanipigia mbona mechi bado haijaanza naona hapa ndo kwanza wana discuss..nikajibu tu nataka kubeti nasikiliza watabir !akashangaa!tangu lini nikamjibu badae kidog nikakata(yani inshort sasa hivi tangu nimeanza kukubaliana na hali halisi najihisi moyo unapumua vizur na najitahid kumuepuka sana...

Mlitoa ushauri wa kuwa makini naweza hata tiliwa sumu wadau mimi nimuoga sana wakutangulia kizembe ni waache wanangu...bas sikuiz jion nabeba kitu namwambia dada anipike chap nikirejea au nakaangiza mwenyew...

Maamuzi niliyofikia ni kwamba krismas hii ntamrudisha kwao...nimeshaongea na pande zote mbili la msingi sitotaka familia upande zote mbili sishauri tuvumiliane wakati mwanamke katamka sana tuachane...

Nafanya hivyo kuka na familia kwasababu wakuu nilioa huyu bint kihaki kabisa nilikabidhiwa kabisa ntamtudisha kama hivyo kiungwana.

ILA... Sitaki wanangu awachukue.
Nataka atoke aende zake na kila kitu akitakacho ntampa ila sio watoto(hata nyumba akijiwehua kulopoka mana akili zake anazijua mwenyew kwa sas)...

Mimi ndo last born kwetu nina kaka zangu wawili
Mama alifariki nikiwa na miaka minne tu..mzee wangu alishauriwa sana aor aligoma kwakutuonea huruma bado wadogo esp mimi...na hakuoa mpaka anafariki...aliniambiaga kitu utakapo maliza shule ndo ntaoa(alikua na mpenz wake tunamuita mamdogo kwemye family gathering walikua pamoja nk ila hakuwahi kulala nyumbani nadhan walikuwa wanahook up kwa mamdogo )i was too young to analyse ila kaka zangu ndo niliwasikia wakiwa wana anyicipate scenerio zote...
Nilipoanza kaz mwaka wangu wa kwanza kazini natimiza ndo nikapata mchumba huyu mzee akaandika barua ilatukatoa mahali nk akafariki...
Ila he was very happy mana alisema adi wewe unaoa mie sijaoa ase kweli sasa kazi yangu duniani imeisha nikapumzike na mwenzangu peponi (utani utani kweli )

Nasema haya namini wanangu ntawalea vizuri sana Mungu atanipigania hili na hata marehem baba yangu alipo atafutahi na kuamini i am everything like him as i wished when it comes to being aparent.

back to the topic
Huyu sas hivi naona anajivisha sana ngozi ya kondoo sijui anaona maneno yake yanataka kutimia nk
Ila ndo nimeamua
Kama ananiona sifai kwa sasa aniache tu i will reach for the stars in Gods favor...

Yani nilianA kuzeeka najiona ase
Inabidi niji pimpu maana am very very on point ase😎😎😎...

Guys thanks alooot...
Mmefanya kazi ya Mungu
Na ndugu zangu tuliokutana PM
Mbarikiwe sana laMa tukeep intouch na mbarikiwe sana kwa moyo mmoja
Hamjanuangusha na kuniacha nipotee mlipohis nalegeza kamba.

Nikihisi sielewi taswira au nalegeza kamba ntawakimbilia mnipe muongozo
 
Mkuu..... Kwanza nikuhakikishie...

UMBALI UNAUA MAPENZI....ni mwanamke pekee mwenye sifa izi hatoruhusu umbali umharibu
ASOKUNYWA POMBE.... Utafiti umethibitisha kua Mnywaji wa Pombe nirahisi sana kusaliti.
MCHAJI WA MUNGU
ukuoa dem ambaye hamjui wala hamchi Mungu........Utagongewa tu
ASOPENDA STAREHE
mwanamke anayependa starehe kiasi cha kuipenda Outing et namashoga ,Huyo ni Kipindupindu.

NINI UFANYE MKUU???

Kuanza Upya sio ujinga...... Ipo ivi MOYO WA MWANAMKE UKISHABADILIKA, BASI HAPO HAMNA NENO LA MWANADAMU LITAKALOKAA LIMBADILISHE HATA SIKU MOJA.

Ni MUNGU PEKEE AU MWANAMKE MWENYEWE KUAMUA KUBADILIKA.

ANZA UPYA ... How????
Mpe Nafasi , mpe nafasi aone umuhimu wako, mpe nafasi ajue Umuhimu wa Ndoa.

Si mmezaa???? NIAMIN, HUYO MCHRPUKAJI WAKE NI ANATAKA KUMTUMIA TU WALA HATOKAA AMUOE HATA KAMA MTAKUA MMEACHANA, SABABU ANAJUA KAMA AMEWEZA KUKUACHA WE MLOZAA WATOTO WAWILI, ATASHINDWA NN KWAKE?????? LKN PIA ANAJUA NI HAWEZI KUOA MWANAMKE MWENYE WATOTO WAWILI.

nini kitatokea????? ...Jamaa atamtumia, kuna wakat atachoka na usikute uyo jamaa naye anafamilia, mwisho atamuacha...HAPO NDO MKEO AKILI ITARUDI NA KUJUA UMUHIMU WAKO NDANI YA NYUMBA..HUO NDO MUDA ATAKAOKUMIS NA KUKUHITAJI, HUO NDO MUDA ATAKAOWAMIS WATOTO NA KUHITAJ KUWAONA WAKIWA MBELE YAKO.

KAMA UNAMPENDA.... USIVUNJE NDOA....bali amua kama mwanaume, kuka na wanao tu, kisha ukate mawasiliano naye, ndioooo ukate sababu 'Anakazi na mshahara na anayempa kiburi".

Kwasababu ninaamin 100% ATARUDI....ndo sasa itakua nafasi nzuri kabisa ya wewe sasa kumfanya unavyotaka,ukitaka naww umuumize niww.

NIAMIN, ATARUDI MKUUU....IPA ATAKAPORUDI NIWW UAMUE UNAVYOTAKA.

USIKAE UKANYWA POMBE, POMBE HAIONDOI TATIZO BALI INATOA MAELEZO YA UONGO KUA TATZO HALIPO NA NIKWA MUDA MFUPI.

RUHUSU HII CHANGAMOTO IKUPE ROHO NGUMUUUUUUUU ...AISEEEE UTAJIKUTA IMEKUA NA MAISHA YA FAIDA.

ACHA KABISAAA KUFIKIRIA MAZURI YAKE, ACHA KABISAAAAAAAAAAA, NIHERI YA KUUKUBALI UBAYA USOKUUMIZA, KULIKO UZURI UKUUMIZAO.
 
Dah wadau ngoja nipumzike
Mana natype nalia natype nalia
Yan kama mtoto vile
Mmmh hatayote wazazi hawajui? Pole ntapata picha unavyoumia, kabla hujapata ngoma, achana nae, wajuze wazazi wake kwanza, pili chukua watoto wako rudi dar, piga kimya.
 
Hapo ndugu chukua maamuzi magumu. Pengine kuna makubwa zaidi yatakutokea ukiendelea kumng'ang'ania.

Kisicho riziki hakiliki. Utaokota na matatizo ambayo hukuwa kuyafikiria bure
 
Dah Unatafuniwa msela, Inauma sana Ila naweye umekaa tu? Kama ni mimi tayari ningelikua nishamfua rinda
 
Kaka mapenzi hasa hisia hazilazimishwi yani hapo unaweza pata matatizo zaidi ,kama mwanamke mwenyewe kakuonyesha hivyo vyote ,chukua hatua achana naye we sepa na wanao
 
we muache kama asemavyo ila nakuambia atarudi tu huyo mwenyewe na utashangaa sasa itakuwa kazi kwako kuendelea nae au kumpoteza.......! ila nakushauri pia hata kama ukamuacha usichukue mwanamke mwingine karibuni hii coz utachagua mwanamke sababu ya hasira tu au kukulelea wanao ila si kwa kumpenda......remember most women have the eyes but they don't see.....have the ears but they don't hear and understand
 
Pole brother ,Mungu akiwa upande wetu ni Nani aliye juu yetu,Bibilia inasema Hakuna.
Brother,endelea kuwa mpole na kuendelea kufanya majukumu Kama baba wa Familia.
Note.Endelea kumpenda mke wako vizuri kabisa mwisho wa siku,Mungu atamrejesha na huo uovu wake.
Kitu ambacho unateseka nacho ktk kipindi hichi unapoona mwanamke Hana utii Maana wanaume wengi wanapenda utii kutoka kwa wake zake.

Turudi kwenye maandiko ya Neno la Mungu kidogo.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Efeso5:------
HALLELUYAAAA....
 
kwanza nikupe pole sana mkuu kwa unayopitia maana inaonesha hata huu ujumbe umeandika kwa uchungu sana...sasa kama we ni mfuasi wa yesu kristo rejea kwenye maandiko pale yesu aliposema na mume asimuache mke isipokua tuh kwenye swala hasa la uasherati au uzinzi kwa maelezo yako inaonesha wazi kabisa mke wako ni pepo la uzinzi na uasherati ndo linamsumbua ndo sababu kubwa za kukupotezea kwa kifupi amekuchoka yanii sasa hapo cha msingi usikumbatie uvundo utakunukia mwisho wa siku..mi nikushauri tuuh mkanye ukiona hakanyiki piga ngoma chini kwani sh ngapi..?watoto sepa nao ila usizuie mahusiano baina ya watoto na mama yao kutembeleana ruksa..
Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka mine na tumebarikiwa watoto wawili. Changamoto zilianza mke alipohamishwa kikazi mwaka juzi kutoka Dar kwenda Morogoro.

Kutokana na ukaribu nikawa najituma sana kutwa kwenda halafu isitoshe huyu mtoto wa pili alikua mwaka mmoja. Umbali ukasababisha mimi niwe mnywaji kidogo kuondoa upweke kuliko niwe nachepuka. Nikawa napunguza safari za kwenda weekend na yeye akazidisha mahusiano ya simu na mfanyakazi mwenzie(sijui kama walitembea ila nilijua wana uhusiano baada ya kunasa chat maana ilifika kipindi anajua weekend nalala ndo anakua busy kwa simu wakiongea na huyo mpaka nilivyombana na chats aka admit wanamahusiano via simu na huyo mtu yupo Dar).

Siku moja nikaenda Moro ghafla nikakuta anachat nae bado na isitoshe kuna mwingine wa Moro; nilimdunda hatari. Tukasuluhishwa na familia baada ya hapo kila tukikwaruzana kidogo anakimbilia kusisitiza tuachane yaani ndo ukawa wimbo.

Sasa nikaona kuondoa usumbufu na yeye kuhamia Dar aligoma kwa kusema maisha nafuu Moro nikatafuta kazi Moro nikahamia(nilipata kazi half the pay ya Dar) ila nilimweleza la msingi tuwe pamoja tuweze nusuru ndoa.

Sasa tangu tumeamua kukaa pamoja mambo hayajawa mepesi. Mimi na-cover basic needs kama kawaida yangu na napambana na biashara ila mwenzangu amekuwa amepotea kabisa kimapenzi. Tangu mwaka huu tunaweza kuwa tumesex si zaida ya mara 15 am sure maana mwenzangu hayupo kabisa anaona nimembana sana.

Kila kitu anatupia lawama nivomdundaga na matatizo ya nyuma. Nimejitahid kumpa space sana ila naona kitu kidogo anakimbilia kutaka talaka.

Sasa kilichonipelekea kuandika uzi huu ni majuzi nilimwambia naenda Dar maana alikua yupo moody sikujua ni sababu yangu au lah. Nikamwambia tu nina safari ya Dar week nzima; aisee alifurahii sana.

Safari ilikuwa ya siku mbili nikarejea jioni nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei alivyotoka kibaruani. Jirani yetu ni mfanyakaz mwenzie akarudi tukapishana nikamuuliza vipi shoga yako akasema tumeachana amesema anapita sokoni mara moja (nikaona very rare kutorudi na shoga yake).

Wife akanitumia meseji akasema ametoka outing na shoga zake. Nikasema fine mimi nikanyuti nje mtaa wa pili kuona nani angerudi nae.

Kuna gari ikaja ikapaki kwa jirani ikakaa dakika kama 15 akashuka halafu gari ikaondoka. Alivyoingia ndani nami nikamfwata kwa nyuma
akashtuka sana. Nikamuuliza nani akasema rafiki yake tu walienda pata wine.

Nikamwambia naomba uwe makini tu kuna maradhi. Kama tumefikia huko naomba basi uwe na amani ufanye yako na si hapa kwangu na isitoshe tuna watoto wadogo usilete jazba kwenye haya mambo(maana tulivoingia ndani akaanza kuwaka kama simuamini alivyosema yupo outing nikamweleza outing sio issue ishu umetoka huko mkaweka kambi kwenye gari mie nawaona tu mnapiga story hamkumaliza huko outing)

Nimegundua hana mapenz kwa sasa na nimevumilia sana vituko vyake ila nawaza niwashirikishe wazazi wake na wadhamini wetu nataka niwachukue wanangu nirudi Dar nimpe nafasi tu.

Mkewangu ananiuma sana kila nikikumbuka nilivyompata, mahusiano yetu nk. Yeye ndo alikuwa kipaumbele kunitia sana moyo pale nilipokwama au kusita jambo(hii naandika kwa majonzi sana)

Umri wake haujazidi 30 bado na kuna muda naamini alingia ndoani akiwa mdogo sijui kuna mambo hajafanya? Ila mimi ni mtu wa kuwa huru sana namwambiaga nishirikishe nikupe kibali sina hiyana wala nini cha msingi ni imani tu kwamba hatavuka mipaka.

Suala la uwezo sijalitilia uzito maana yeye binafsi ana kazi na mshahara wake kwakweli huwa simgusiagi hata kidogo anafanya atakavyo. Mimi nina nyumba Dar ndo nimepangisha kuja kuishi naye huku. In short majukumu yangu nayajua na nayamudu.

Suala la kitandani lilikuwa zuri tu sote tunafurahi nk. Mwaka huu lilianza kususasua penzi la kubembeleza yeye ata enjoy ila mpaka nimemuandaa nimemconvince mbona shughuli.

Kwa upande wangu sio mnywaji sana na anajua. Nikinywa tu wine nikiwa nae ntajitahid kumueleza kiu yangu juu ya mambo ambayo hanitimizii hapo nae atarukia "si uniache"bas mkibishana atasema mlevi tatizo.

Weekend ndo tunakaa na kujadili mambo ila mara chache sana maana katikati ya wiki akirudi home yeye kachoka ni kula kulala tu.

Mimi ni mwanadamu pia naweza kuwa na mapungufuyangu ila all i know kuachilia mbali kila jambo nimekuwa nikijitahid kuomba msamaha ninapokosea nk.

Ndugu zangu ndo wanaona nimekamatwa kwelikweli ila nakuwa najitahid niishi ki maadili maana mke mwenyewe mmoja.

Nimesali sana mpaka nimeona kama ni watoto hata nikisema nimpotezee nitahitaji kuwaona wanangu ambapo itapelekea nimwone labda na yeye kitu ambacho mda mwingi kinaniwia ngumu kuvunja familia. Ila nikisema nibebe watoto(namjua kwa sasa majibu yake atasema nenda nao tu la msingi tuachaneee nk) nitabeba ila nataka niombe nisingependa kusikia pua yake na wakwe ndo watakua gia ya kuwaona. Ninataka full right ya wanangu nina uwezo wa kuwalea vizuri. Yani naumia sana ila naona ndo best option kwa sasa.

Naomba ushauri wenu wakuu
 
Mkuu...hata mimi kuna my friend kahamia dodoma huku mke wake akimwacha dar..sasa kila siku ana wasiwas kua jamaa watamla
 
Back
Top Bottom