Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Kwan ww ulikuwa una mpango wa kuoa kwa kutegemea michango ya watu?!
Hapana ila na mimi nimeumbwa cjachongwa, kwa vile nilijitahidi kudonate lazima nitarajie kitu from my friends pia
 
Mkuu kwenye ishu ya kuoa kwa kweli usitegemee marafiki hata kidogo. Kwenye haya mambo ndugu wa karibu ndio huwa msaada mkubwa. Kama baba yako , mama yako , kaka zako na dada zako. Kama hujajaaliwa kuwa na ndugu hao wa karibu wenye uwezo aisee ni bora hata kuahirisha harusi. marafiki siku hizi ni mkia wa fisi tu , marafiki hawana lolote. Wao waalike mkanunuliane bia. Ila sio michango ya harusi au mambo ya maana
 
Nenda kanisani funga ndoa wewe...tatizo mnapenda sherehe kuliko ndoa...na hii ndio chanzo cha wanaume kuendekeza uzinzi..

Sherehe sio lazima...
Una bahati nimeoa! Ningekuoa haswaa
 
Nenda kanisani funga ndoa wewe...tatizo mnapenda sherehe kuliko ndoa...na hii ndio chanzo cha wanaume kuendekeza uzinzi..

Sherehe sio lazima...
Nikimpata wa kuolewa,bila harusi nitaaoa kesho kabisa..!
 
Kadi yako ninayo kijana, lakini je wewe umeandaa kiasi gani?
 
Dah....eti Jana nimeungwa kwenye kundi LA sherehe ya ndoa ya 65m...
Nimecheka usiku kucha....hiyo bajeti haiwezi kujenga zahanati kule ikwiriri kweli?[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hahahahaahaah
 
Mkuu hiyo buku 35 ongezea hapo 65 jumla laki.nunua faru john 2,maji makubwa mawili,soda creti moja,lipia vyeti na zile ada zingine za kanisani/msikitini,chenchi inayobakia nunua mchemsho wa 15 weka kwenye sinia moja kiroho safi sherehe imeisha na imenoga ..kumbuka ndoa halisi na sherehe halisi ni ile ya pale ndani kanisani/msikitini wakati watumishi /shehe akiwaunganisha...naomba kuwasilisha mkuu
 
Watu siku hizi wanapanga michango
Double 70
Single 50
Na maisha haya ya magu unategemea nini?
Tuache kuigiza.
Mpe kadi mtu ajipimie mwenyewe.
Tena utapata nyingi hizo 30 kuliko hata hao unaotaka wa 70
Mimi nimewaalika harusi tu bila ya kuonyesha nataka mchango kiasi gani
 
NENDA KANISANI NA MKEO NA WASIMAMIZI!!
FUNGENI NDOA YENU KWA IMANI ZOTE!!

TURUDI KWENYE SHREHE SASA
HIYO 35,000
UKIONGEZA 65,000 AMBAYO NAJUA KWA MWONEKANO WAKO HUIKOSI!!
JUMLA UTAKUWA NA LAKI!!
NENDENI KFC MNAPATA KUKU MIPAJA MIKUBWAA NA CHIPS ,WATAWAPA NA GUSODA NUNUENI SPRITE IKIFUNGUKA HUWA INALIAA PSIIIIIII KAMA CHAMPAGNE!!
BEST MAN AWE NA KAMZINGA KA NYAGI MFUKONI!!

MTAUNYWA KWENYE UBER WAKATI MNARUDI HOME KULALA!!
Mimi ni ndoa ni masjid
 
Kama ulichangia harusi ni haki na wewe uchangiwe na wenzako tena kiasi kile kile ulichotoa!
Hawa nafanya subra kidogo nikuona kimya nawapigia wanilipe nilichowachangia la si hivyo nitawashtaki
 
Endelea na mpango wa sherehe bila kuhesabia pesa uliyotegemea kutoka kwao.. ikija basi ni vizuri kwako. Cha muhimu ni usiwaalike kama hawatachanga.. na poa usiwe ul>wategemea wao wakufanyie harusi.. fanya ya kukupa furaha na ndugu zako, ila ikiwa ulitaka makubwa na kujionyesha pole yako.

Haya endelea bila kuwahesabu wao kwa sasa ujipe amani moyono mwako.. ila pole aiseeeeee ndio maisha.. utakuwa umejifunza mengi.. moja ukitoa usitegemee pia hivyo hibyo kwako.. toa nenda zako
Hawa ni lazima niwaalike na table yao hakiamungu naweka maji ya kandoro tu.
 
Mkuu kwenye ishu ya kuoa kwa kweli usitegemee marafiki hata kidogo. Kwenye haya mambo ndugu wa karibu ndio huwa msaada mkubwa. Kama baba yako , mama yako , kaka zako na dada zako. Kama hujajaaliwa kuwa na ndugu hao wa karibu wenye uwezo aisee ni bora hata kuahirisha harusi. marafiki siku hizi ni mkia wa fisi tu , marafiki hawana lolote. Wao waalike mkanunuliane bia. Ila sio michango ya harusi au mambo ya maana
Noted
 
Waswahiliwalisema"tenda wema wende zako, usingoje shukurani".

Katika maisha, usifanye wema kwa kutegemea kulipwa.

Fanya wema kwa sababu ni jambo jema tu.

Utajiondolea headaches kibao.
Sawa bhana nimejifunza kitu katika hii harusi yangu ..mipango si matumizi
 
Habari zenu wakuu.
Natumai ndani ya huu mwezi nitajiunga rasmi katika lile chama la watu wazima (nachukuwa jiko) ili na mimi niweze kupata utulivu wa nafsi. Chakushangaza ni kwamba hadi sasa nimepokea mchango kutoka kwa friend mmoja tu, tena na yeye amenipa shilingi 35,000/=. Hivi tuseme marafiki zangu wamesahau michango niliyowapa wakati wa ndoa zao au ndo vyuma vimekaza? Ama ni vipi wakuu nyinyi ambao mmeshaowa michango mlikuwa mnapokea kama siku ngapi kabla ya harusi? Maana kwa kweli zimebaki siku chache mno na sioni sms ya tigo pesa, au naonekana mimi ni tajiri kutokana na muonekano wangu hivyo sihitaji sapoti.


Achana na hii dhana potofu na ya kijinga, kua uoe wewe kwanini watu wakuchangie? Kama hauko tayari kuoa usilazimishe michango, fanya kazi na usevu hela zako kwa ajili y harusi yenu/yako. Nikuchangie uoe, je nikiomba kulala na mkeo utanipa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom