Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Unajuwa sometime mtu unaweza kuwa na kauwezo kidogo ila ukikumbuka ulichangia pia sasa zamu yako unajiuliza mbona kimya au ndo ni vyuma vimekaza
Mie nikitoa mchango nimemaliza wala siweki kumbukumbu maana itakuja kukuumiza kama hivi. Na hali ya maisha inabadilika ulikuwa na kitu leo kesho huna hivyo hivyo kwa upande mwingine.

Funga ndoa yako achana na kusubiri hela hujui utaipata lini. Kikubwa chukua fedha uliyonayo tengeneza budget alika wachache mwisho omba amani furaha upendo vitawale kwenye ndoa yako
 
FANYA HIVYO HIVYOOOO!!
ONDOA TU HAKO KA NYAGI HAPO CHINI MDOGO ANGU!!
THE REST!!
COPY AND PASTE!!

TENA KWANZA WALA USIWE MBINAFSI!!
ALIKA HATA WATU 30,MLE CHAKULA PAMOJA!!

KWENYE HIYO LAKI!!
NYAMA KILO TANO -30,000
MCHELE KILO 20- 30,000
MAFUTA CHUPA MBILI -6000
VIUNGO VYA PILAU-10,000
CABBAGE 2 -4000
NYANYA-3000
KUNI -10000
MAJI YA KUPIKIA -MADUMU 5 KILA DUMU 300=1500
PILIPILI-500
NAULI YA KWENDA NA KURUDI SOKONI-5000
JUMLA 100,000

SINIA ,SUFURIA,MIKO WATALETA MAJIRANI,MATOFALI YA MAFIGA (HAMMA SITE JIRANI HAPO?
HUJAOA TU RAFIKI??
Yani umemuwekea na bajeti kabisa.

Safi sana.

Matatizo mengine ni ya kujitakia zaidi.

Kazini kuna msela aliondoka likizo ya wiki chache. Kasema anaenda kuoa Hawaii.

Jamaa hana makuu.

Hajapitisha mchango. Hakukuwa na tangazo kubwa.

Mchizi kaenda Hawaii. Kajiolea kimwana. Karudi kazini.

Anarudi kinamama wanamzonga.

Jay umeshaoa? Anasema ee, tayari nimeshaoa. Nitawaletea picha.

Hakuna shobo wala mchango wa harusi.

Na jamaa ka enjoy kichizi na mkewe ndoa beach za Hawaii.

Wengine kama vipi anaweza kuwaalika dinner mmoja mmoja akipenda.
 
Kwahiyo Mkuu zeshchriss hutaki michango yetu siku ya ndoa yako??[emoji3][emoji3]
Sitaki shida Mimi kwanza me muislamu so nimeshatoa taarifa nyumbani kwamba nitaolewa SAA mbili ya usiku kimya kimya ni Mimi na mume wangu...shekhe..mashahidi mshenga pamoja na wazazi full stop ....sipendi sherehe hata kidogo na nikialikwa hata bila michango sikanyagi nitatafuta sababu yoyote ile nisiudhulie hiyo sherehe
 
Hali ngumu, na sio formula kwamba kila uliyemchangia atakuchangia! By the way mtu akioa hata kampan inabalika, hope urafiki ulikufa ndo mana hawajachanga.
Ila wiki mbili za mwisho ndio za kupokea michango kwa fujo.
 
Kuna michango utapokea baada ya ndoa wabongo huwajui wewe. Kama ulichanga ili wakuchangie desg imekula kwako na kifuatacho ITV ni kufa hata kwa urafiki uliopo. Ndo maana mi nachangiaga misiba tu
 
Ndo zimebaki kama wiki tatu tu mkuu
 
Kuna michango utapokea baada ya ndoa wabongo huwajui wewe. Kama ulichanga ili wakuchangie desg imekula kwako na kifuatacho ITV ni kufa hata kwa urafiki uliopo. Ndo maana mi nachangiaga misiba tu
Sawa tutakutana kweny harusi za watoto wao au rambi rambi
 
Mie nikitoa mchango nimemaliza wala siweki kumbukumbu maana itakuja kukuumiza kama hivi. Na hali ya maisha inabadilika ulikuwa na kitu leo kesho huna hivyo hivyo kwa upande mwingine.

Funga ndoa yako achana na kusubiri hela hujui utaipata lini. Kikubwa chukua fedha uliyonayo tengeneza budget alika wachache mwisho omba amani furaha upendo vitawale kwenye ndoa yako
Kwa kweli najitahidi kusahau nifanye kama ilikuwa sadaka ila duuuh kamoyo kanagoma kabisa nahisi kama nimeonewa sana.
 
Nenda kanisani funga ndoa wewe...tatizo mnapenda sherehe kuliko ndoa...na hii ndio chanzo cha wanaume kuendekeza uzinzi..

Sherehe sio lazima...
Na wanawake kutaka kuolewa ili watimize sherehe za maisha Yao
Na kuwaringishia Wengine.
 
Sitaki shida Mimi kwanza me muislamu so nimeshatoa taarifa nyumbani kwamba nitaolewa SAA mbili ya usiku kimya kimya ni Mimi na mume wangu...shekhe..mashahidi mshenga pamoja na wazazi full stop ....sipendi sherehe hata kidogo na nikialikwa hata bila michango sikanyagi nitatafuta sababu yoyote ile nisiudhulie hiyo sherehe
Interesting, what a comment!!🙌
Isingekuwa kuoa mke wangu wa nne mwaka jana ningekuja kukuposa haraka sana.
Hongera
 
Nenda kanisani funga ndoa wewe...tatizo mnapenda sherehe kuliko ndoa...na hii ndio chanzo cha wanaume kuendekeza uzinzi..
.

Mkuu una wasahau sana jinsia yako. huo uzinzi wanaume wanafanya na Mbuzi au?
 
Hata Jf huna marafiki wa kukuchangia au hukutangaza mapema?
 
Aliyemtoa bikra hajagharamikia chochote, wewe ndoa tu unataka gharama kibao pole!! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
KWENYE HIYO LAKI!!
NYAMA KILO TANO -30,000
MCHELE KILO 20- 30,000
MAFUTA CHUPA MBILI -6000
VIUNGO VYA PILAU-10,000
CABBAGE 2 -4000
NYANYA-3000
KUNI -10000
MAJI YA KUPIKIA -MADUMU 5 KILA DUMU 300=1500
PILIPILI-500
NAULI YA KWENDA NA KURUDI SOKONI-5000
JUMLA 100,000

Mkuu agiza Biskuti ya mia mbili nitapita kulipa, umempa jamaa BonGe la Bajeti.
Nitakualika kama mwanakamati kwenye harusi yangu.
 
Hivi tuseme marafiki zangu wamesahau michango niliyowapa wakati wa ndoa zao au ndo vyuma vimekaza? Ama ni vipi wakuu nyinyi ambao mmeshaowa michango mlikuwa mnapokea kama siku ngapi kabla ya harusi? Maana kwa kweli zimebaki siku chache mno na sioni sms ya tigo pesa, au naonekana mimi ni tajiri kutokana na muonekano wangu hivyo sihitaji sapoti.

Hizo SMS za tiGo pesa adimu sana kipindi hiki mkuu,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom