mimi sikupokea mchango wwt kutoka kwa rafiki zangu..sio kwamba ni tajiri,wala si kwa sabb sitoagi,wala si kwa sabb nina roho mbaya n.k...bali kwa sabb nilifikiria nikaona mm nfo naenda kufurahi,kwann nisumbue watu..hivo sikugawa kadi za michango.ila niliweka wazi "mtu akitaka kutoa na atoe,asiyenacho aje"(niliwapa kadi za mualiko)..
lkn wkt nafikiria kufanya hayo yote,nilijiandaa na kichwani nikasema "kitaliwa chochote hata ugali,kwani chakula ndio kinaoa?" hakuna wa kunilaumu ht wakikuta ugali,kwa sabb hakuna niliyemdai mchango..
hayo yalikuwa ni malengo yangu kabla na niliyapanga,nikimtegemea MUNGU anisaidie kufanikisha na si watu wanisaidie,basi ikiwa MUNGU atanisaidia,basi yeye(MUNGU) atanichagulia hao watu wa kunisaidia..
namshukuru MUNGU nilifanikiwa,tulichanga watu wa 5 tuu,na wote ni wa hali ya chini sana,kula kwao tuu kwa shida,lkn walitoa kwa moyo na watu waliokuja kuona NITASHINDWAJE wakaja kuona kinyume chake na wakaniambia walikuja kuona ningefanyaje na "umasikini" wangu....
*Usitegemee watu