Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Sherehe wanawake wengi ndio hupenda
Namaanisha anayeolewa. Wewe cha kufanya kafunge ndoa kanisani/ msikitini. Kitendo hicho hufanywa bure na aliyepewa mamlaka ya kuozesha. Kama upande wa pili wanataka sherehe waambie wafanye sherehe upande wao ila wewe huendi.
 
Watu siku hizi wanapanga michango
Double 70
Single 50
Na maisha haya ya magu unategemea nini?
Tuache kuigiza.
Mpe kadi mtu ajipimie mwenyewe.
Tena utapata nyingi hizo 30 kuliko hata hao unaotaka wa 70
 
Yani michango inaboa sana ,,mtu anataka mchango mkubwa

Mimi harusi yangu niliwaambia ulichonacho nichangia,,na sikua na pesa ,,aliyenichangia Kubwa alichanga elfu 40, wengi elfu 20,,nikapokea kiroho safi,, tukaoana wakaja tukafurahi mpaka sasa tuna amani. Ila Nina kadi saba sasa za mchango zote nimepangiwa nichange single 50 double 70-80. Mnaudhi sana
 
Endelea na mpango wa sherehe bila kuhesabia pesa uliyotegemea kutoka kwao.. ikija basi ni vizuri kwako. Cha muhimu ni usiwaalike kama hawatachanga.. na poa usiwe ul>wategemea wao wakufanyie harusi.. fanya ya kukupa furaha na ndugu zako, ila ikiwa ulitaka makubwa na kujionyesha pole yako.

Haya endelea bila kuwahesabu wao kwa sasa ujipe amani moyono mwako.. ila pole aiseeeeee ndio maisha.. utakuwa umejifunza mengi.. moja ukitoa usitegemee pia hivyo hibyo kwako.. toa nenda zako
 
NENDA KANISANI NA MKEO NA WASIMAMIZI!!
FUNGENI NDOA YENU KWA IMANI ZOTE!!

TURUDI KWENYE SHREHE SASA
HIYO 35,000
UKIONGEZA 65,000 AMBAYO NAJUA KWA MWONEKANO WAKO HUIKOSI!!
JUMLA UTAKUWA NA LAKI!!
NENDENI KFC MNAPATA KUKU MIPAJA MIKUBWAA NA CHIPS ,WATAWAPA NA GUSODA NUNUENI SPRITE IKIFUNGUKA HUWA INALIAA PSIIIIIII KAMA CHAMPAGNE!!
BEST MAN AWE NA KAMZINGA KA NYAGI MFUKONI!!

MTAUNYWA KWENYE UBER WAKATI MNARUDI HOME KULALA!!
 
Ndio stress za kuchangia watu ili uje uchangiwe, upuuzi moja wapo uliopo Tanzania
 
Mkuu, kwanza nikupongeze kwa kutoa michango na kushirikiana na wengine, mchango wa harusi au sherehe ni kama deni, hivyo, uliowachangia wanao wajibu wa kukuchangia pia. Mwisho, ndoa siyo gharama ingawa ktk ndoa za kikristo, sherehe ina uzito wake kwa kuwa, ndyo tukio la kiimani kubwa zaidi la mwisho kulifanya ukiwa hai, sherehe inayofuata ni msiba ambao ww hutokuwa hai. Kwa upande wa waislamu, sherehe siyo kitu cha muhimu sana kwa kuwa unaweza kuoa leo, kesho ukaoa mwingne na mwingine hadi wanne, na ukapiga talaka ukaoa tena
 
Kikwazo kikubwa kwenyw haya mambo ni jinsia KE. Hawapo tayari kabisa kufunga ndoa na kurudi nyumbani kula ugali mlenda.

Mashoga zake hawatamwelewa, itakuwa aibu kubwa sana. Na mambo mengine mengi yakipumbavu.

Wanawake badilikeni jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom