Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

Ndoa yangu inakaribia ila michango kutoka kwa marafiki hakuna

vposterior

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2018
Posts
732
Reaction score
1,232
Habari zenu wakuu.
Natumai ndani ya huu mwezi nitajiunga rasmi katika lile chama la watu wazima (nachukuwa jiko) ili na mimi niweze kupata utulivu wa nafsi. Chakushangaza ni kwamba hadi sasa nimepokea mchango kutoka kwa friend mmoja tu, tena na yeye amenipa shilingi 35,000/=. Hivi tuseme marafiki zangu wamesahau michango niliyowapa wakati wa ndoa zao au ndo vyuma vimekaza? Ama ni vipi wakuu nyinyi ambao mmeshaowa michango mlikuwa mnapokea kama siku ngapi kabla ya harusi? Maana kwa kweli zimebaki siku chache mno na sioni sms ya tigo pesa, au naonekana mimi ni tajiri kutokana na muonekano wangu hivyo sihitaji sapoti.
 
Pole. Kufunga ndoa haicost chochote. So we nenda kafunge tu. Sherehe mnaweza mkaifanya kama ka get together nyumbani tu. Keep it simple

This is why I tell people, msitegemee sana michango kwaajili ya sherehe. Kwasababu it's just that, michango. Inaweza ifike malengo au la. Kama mtu una event yoyote unataka kufanya na ungependa watu wakuchangie, basi atleast kuanzia 60 - 75 percent ya expenses unauhakika wa kufinance mwenyewe. Hizo percent zingine zilizobaki ndo unaweza ukaacha wengine wachange. Otherwise either mtu afanye kasherehe kadogo au kama anataka event kubwa, a start saving for it kuanzia kabla.
 
Kitendo cha kufungishwa ndoa kinagharimu shilingi ngapi, nadhani ni bure na kama ipo basi ni karibu na bure. Nenda kafunge ndoa yako mambo ya kunywa na kula utayafanya baadaye.
Naunga mkono, hoja yeye cha kufanya atafute wasimamizi na wafunge ndoa. hiyo buk 35,000 inawatosha kabisa na kama anakunywa pombe siku hiyo apige faru john ili kupunguza gharama
 
Nenda kanisani funga ndoa wewe...tatizo mnapenda sherehe kuliko ndoa...na hii ndio chanzo cha wanaume kuendekeza uzinzi..

Sherehe sio lazima...
HEhehe bora umemwambia bila kupepesa macho, wanapenda sana show off zisizokuwa na sababu
 
Kuna nsela wangu anaoa mwezi wa 10 mchango single elfu 50 nimewaza sana hii hamsini ntaishia kula kipapatio cha kukua ambacho thamani yake ni kama buku,pilau robo,ndizi mzuzu moja na tubia tuwili twa buku 3,nishaghairi sichangi ntampa elfu 10 tu akanunue kreti LA soda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom